Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 751 to 760 of 2266.

  • 27 Oct 2022 in Senate: Bw. Naibu wa Spika, ninasema yule aliyekuwa hapo awali, alikuwa afadhali kuliko Bi. Mengich. Bi. Mengich aje hapa Bungeni na tumhoji. Ikiwezekana, hili Jopo lake liondolewe ama lifutiliwe mbali kabisa. view
  • 27 Oct 2022 in Senate: Asante sana, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Taratibu za Bunge ni kwamba ikiwa alikuwa anataka kumueleza Sen. M. Kajwang’ kuhusiana na taarifa fulani, alifaa kukuambia kuwa siyo hoja ya nidhamu. Angesema anataka kumfahamisha ili aseme kama amekubali lakini hakumuuliza Sen. M. Kajwang' kama angependa kufahamishwa. Kwa hivyo, yeye ndiye amepotoka. Pili, Sen. M. Kajwang’ amesema jambo muhimu sana. Alisema kuwa Sen. Tabitha Keroche asisahau. Wakati tuko kwenye likizo fupi, ni muhimu kusisitiza kwamba Serikali inafaa kuwajibika kwa sababu serikali za kaunti zinahitaji pesa hizo. Tuko hapa kama Maseneta kwa sababu ya serikali za kaunti. Tunafaa kuwapelekea pesa ... view
  • 27 Oct 2022 in Senate: Asante, Bw. Spika wa muda. Jambo la kwanza, naunga mkono taratibu ya dada yangu Sen. Tabitha Keroche kwa kuona ya kwamba imefika wakati ingekuwa vyema Maseneta waenda likizo kidogo. Nina imani ya kwamba agizo la kwenda likizo kama hilo litasaidia pakubwa kwa wale maseneta ambao wameingia Bunge hivi sasa. Hii ni kwa sababu tumeona wakiwa na tabia ya kutembea hapa ndani na kuvuka upande huu bila kwenda pale mbele--- view
  • 27 Oct 2022 in Senate: Ndiyo, Bw. Spika wa muda. I am seconding the Motion. view
  • 27 Oct 2022 in Senate: Naunga mkono na pia ninaeleza ni kwa sababu gani tunahitaji kufunzwa tukienda likizo. Hii ni kwa sababu kuna taratibu ambazo tunafaa kufundishwa kulingana na yale ambayo yamefanywa hapa na maseneta. Najua ya kwamba ndugu yangu, Sen. (Dr.) Khalwale, atakubaliana na mimi. Yeye mwenyewe amesimama hapa akisema tabia kama hio sio nzuri. Seneta anafaa aenda pale, ainame, asimame, alafu aende upande ule anaotaka ama aingie ndani wakati Spika yuko kwenye kiti. Bw. Spika wa Muda, sio hiyo taratibu peke yake ambayo tunafaa kufundishwa. Kuna taratibu nyingi. Ni muhimu hawa ndugu zetu waweze kujua kile ambacho wanafaa kufanya wanapotaka kuongea wakati umeketi ... view
  • 27 Oct 2022 in Senate: Mr. Temporary Speaker, Sir, I would like to find out from our friends in the House. I wonder why the microphone of Sen. M. Kajwang’ went off when he was on a critical point. I want to imagine that it was a coincidence and not a deliberate move. view
  • 26 Oct 2022 in Senate: Bw. Naibu Spika, asante kwa kunipa nafasi hii. Jambo la kwanza, nampa kongole ndugu yangu Sen. Murkomen, kwa kuteuliwa kama Waziri. Hatimaye, Bunge la Kitaifa limepitisha kwamba anafaa na anastahili kuwa Waziri wa Barabara, Uchukuzi na Ujenzi. Nampa mkono wa buriani ndugu yangu Sen. Murkomen. Bw. Naibu Spika, kama ndugu yake mkubwa kwa umri, ningependa kumwambia kwamba wadhifa aliopewa ni mkubwa sana. Macho yote yatamwangalia. Watu hawataangalia umri bali wataangalia matendo ambayo atatenda ofisini. Namuomba ashike vizuri sana wasia ninayo mpa na ayafunge katika vidole vyake. Wasia wenyewe ni atumikie Wakenya wote kwa roho mmoja. Ninayo imani kwamba atawatumikia kwa ... view
  • 26 Oct 2022 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika. Wakati ule, ilikuwa ni lazima watu waonyeshe ubabe na kwamba wako na Ukenya ndani mwao. Ilikuwa ni jambo la kushangaza. Nampa mkono wa kongole kwa kujitolea kwa sababu kaunti yake ilikuwa inapata ilhali zingine zilikuwa zinapoteza. Alisimama na haki ya wale waliokuwa wanapoteza ili sote tupate maendeleo. Bw. Naibu Spika --- view
  • 26 Oct 2022 in Senate: Tafadhali, naomba dakika tano, Bw. Naibu Spika. view
  • 26 Oct 2022 in Senate: Hiyo ni sawa. Tafadhali, mweleze Sen. Cherarkey asije na hoja ya nidhamu. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus