Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 761 to 770 of 2266.

  • 26 Oct 2022 in Senate: Ni vyema Sen. Murkomen ajue ya kwamba, wakati atapoketi katika Wizara akiendeleza utendakazi wake, watu wa pwani watakuwa wanamuangalia. Tumetazama Serikali zilizopita, kutoka wakati wa Uhuru mpaka hivi sasa, ambapo Serikali inaongozwa na Mhe. Rais Ruto. Wakati watapokuwa wanafikiria kutengeneza barabara za pwani, wasifikirie tu mambo ya utalii. Hilo ndilo lilikuwa lengo la hizo serikali zingine. Tuanze kufikiria kwamba watu wa pwani pia wako na marikiti, masoko makubwa na ni wakulima ambao wanahitaji barabara ili waweze kwenda vitongoji, kule wanapoishi. Hiyo itakapotendeka, hata sisi tutaweza kupata maendeleo kama kaunti zingine za Kenya. view
  • 26 Oct 2022 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 26 Oct 2022 in Senate: Najua ya kwamba Sen. Murkomen ni kiongozi thabiti na ataendeleza kazi yake ya kutumikia Wakenya kiukamilifu. Namutakia kila la heri katika shughuli zake za Uwaziri. Mungu amubariki. Asante. view
  • 25 Oct 2022 in Senate: The two of you can have the Floor. view
  • 25 Oct 2022 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika kwa kunipa nafasi hii. view
  • 25 Oct 2022 in Senate: Ninawakaribisha wanafunzi na waalimu. Najiunga nawe pia kuwaambia, “karibuni ndani ya Bunge la Seneti”. Jambo la muhimu ni kwamba wamekuja kujionea jinsi Seneti inavyofanya kazi na kuweza kuona viongozi wao wanavyotekeleza wajibu wao baaada ya kuchaguliwa. view
  • 25 Oct 2022 in Senate: Bw. Naibu Spika, la muhimu ni kwamba Nduundune, nilivyoambiwa na ndugu yangu Sen. Maanzo, ni shule nzuri iliyopitiwa na vigogo wa nchi hii yetu. Nawatakia kila la heri. Kuja kwao hapa imewawezesha kuona vile kazi inaendelea ndani ya Seneti. Nina uhakika kwamba mmoja au wawili wao wameguswa. Nina imani kwamba wengine wao watasimama siku moja na kusema kwamba waliona viongozi wao wakifanya kazi katika Seneti na hao pia wanaomba mwenyezi Mungu awasaidia kufika hapa. view
  • 25 Oct 2022 in Senate: Nawatakia kila la heri katika shughuli zao ili waweze kujifunza. Watakaporudi nyumbani, wawe na mioyo na ari ya kuja hapa watakapomaliza masomo yao baada ya sisi kuondoka. \ view
  • 25 Oct 2022 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika. view
  • 25 Oct 2022 in Senate: On a point of order, Mr. Deputy Speaker, Sir. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus