25 Oct 2022 in Senate:
Bw. Naibu wa Spika, je, ni haki ndugu yangu, Sen. Kinyua, kuleta hoja nyingine ambayo haiuhusiani kabisa na Hoja ya nidhamu? Umemsikia alivyosema na mimi ninaomba uamuzi wako. Ilikuwa hoja ya nidhamu ama mambo ya Kaunti ya Meru? Kama ni mambo ya Kaunti ya Meru, anatakiwa alete Hoja maalum hapa tuijadili.
view
25 Oct 2022 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
25 Oct 2022 in Senate:
Asante, Bw. Spika wa Muda. Kwanza nampa kongole Seneta wa Kitui kwa kuleta hii Taarifa. Pili, ni ukweli kabisa, mimi nikiwa kama shahidi kwa sababu nilikuwa katika ile Kamati ya Labour and Social Welfare na bado nipo. Kwa hivyo, ninaongea ukweli kwamba jambo hili lilijadiliwa kwenye Kamati hiyo.
view
25 Oct 2022 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, nitetee kwa sababu huyu Mmaasai ananiingilia.
view
25 Oct 2022 in Senate:
Asante, Bw. Spika wa Muda. Pili, ukiona madiwani waliokuwapo zama hizo, utawaonea huruma. Wale wezi wao wako sawasawa ilhali wale waliofanyia wananchi kazi kisawasawa waliopoteza viti vyao. Ukiwaona ni watu wanaoishi “mahai” yaani maisha ya uchochole. Hawana mbele wala nyuma. Utashangaa kama walikuwa madiwani walioheshimika wakati huo. Mwisho, ni ukweli kuwa tulipitisha ridhaa ya Kshs200,000, lakini hizo si pesa nyingi. Nina imani ya kwamba, Taarifa hii ikipelekwa kwa ile Kamati ya Leba na Maslahi ya Jamii, basi wale watakaoketi kwa hiyo Kamati, hawana haja ya kufanya kama
view
25 Oct 2022 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
25 Oct 2022 in Senate:
Sen. Olekina alivyosema, kuwa akimbie kwa marafiki zake kule Bunge la Kitaifa kuwatongoza. Tuko na uwezo katika Kamati ya Leba na Maslahi ya Jamii, kuchukua hatua na kusema kuwa ile pesa ya ridhaaa iliyopitishwa ilipwe. Tuko na Mawaziri wapya waliochaguliwa. Tuna imani kuwa yule Waziri wa Leba hataanguka ukaguzi. Ripoti yake ikiwa safi, ataanza kazi haraka iwezekanavyo. Kuna umuhumu wa kuwapatia hawa madiwani wazee walioanzisha serikali za ugatuzi heshima yao. Bila hao hatungeweza kusimama hapa leo hii na kusema kuwa tunataka seriakali za ugatuzi ziendelee vipi. Wao ndio waliotengeneza Serikali za mashinani ndipo sisi tukachukua kutoka kwao tukasema hizo zitakuwa ...
view
19 Oct 2022 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Kwanza, ninampa kongole dada yangu, Sen. Kibwana, kwa kuleta taarifa hiyo. Pili, ninakubaliana na yote aliyosema. Tuliona picha za huyo mtoto katika magazeti, akiwa na uma jembe kichwani mwake. Ninaunga mkono ya kwamba madaktari walichelewa kumhudumia yule mtoto. Hata hivyo, hilo silo jambo pekee. Kulikuwa na ukosefu wa madaktari katika hospitali za kaunti lakini wakaandikwa lakini sasa inaonekana wamezembea kazini. Miezi miwili ama mitatu iliyopita, Bunge la Kitaifa lilimpoteza Mhe. William Kamoti, ambaye alipata ajali katika barabara ya Mombasa-Kilifi. Alipelekwa hospitali saa mbili usiku lakini madaktari walikuja saa nane. Hiyo ni baada ya masaa sita. Hospitali ya ...
view
19 Oct 2022 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
19 Oct 2022 in Senate:
Bw. Spika, madaktari kutofika hospitali katika masaa yanayotakikana ili kuokoa maisha ya wagonjwa, ni jambo ambalo linaonekana linaanza kupata moto kila mahali. Huu utepetevu unatendeka maeneo ya Kisumu, Kilifi na pia hapa Nairobi. Ninaomba hiyo Taarifa ijumuishwe pamoja na ya Mhe. Kamoti ili ziangaliwe pamoja. Ni kwa sababu gani madaktari hawakuwa kazini na kama walikuwa kazini, ni kwa nini walichelewa kumhudumia mheshimiwa. Na pia yule mtoto ambaye Sen. Kibwana amemzungumzia? Itakuwa vyema hii kesi ya mheshimiwa ijumuishwe na mtoto Travis.
view