Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 781 to 790 of 2266.

  • 18 Oct 2022 in Senate: Bi. Spika wa Muda, kwanza, nawashukuru sana wale ambao wameleta hii ardhihali, wakiongozwa na Daniel Rakoko, kuhusu maisha ya watu wanaoshi kwenye visiwa kule Homa Bay. Tunaelewa kwamba watu hao hupitia hali ngumu ya usafiri. Watu hawawezi kutoka nyumbani wakiwa na mizigo ama wakienda shuleni au popote penye haja kwa sababu inawalazimu kuogelea ilhali hawawezi kufanya hivyo wakiwa na mizigo. Watu hao wanahitaji huduma za usafiri kikamilifu kama Wakenya wengine, jinsi view
  • 18 Oct 2022 in Senate: inavyotoa huduma za usafiri kwa watu wa Mombasa na pande zingine. Mara nyingi, kwenye visiwa, utapata kuna wakulima, wavuvi na wafanyabiashara mbalimbali. Wavuvi na wakulima huhitaji usafiri ili kupeleka bidhaa zao sokoni. Hali kama hiyo ni ngumu kwao. Ikiwa hali hiyo itaendelea, wakazi wa visiwa kama vile Mfangano na Rusinga wataendelea kuumia. Kwa hivyo, KFS inafaa kuchukua hatua kwa haraka. Kama kuna pesa, ni vyema Serikali yetu kuchukua hatua kwa haraka na kuhakikisha ferry zimepelekwa kule ili kusaidia watu wanaoishi kwenye visiwa. view
  • 18 Oct 2022 in Senate: Bi. Spika wa Muda, naomba dakika moja tu nimalizie. view
  • 18 Oct 2022 in Senate: Bi. Spika wa Muda, kwa kumalizia, ningependa kuhimiza wafanye haraka kwa sababu kuna wagonjwa, wafanyabiashara na watu tofauti tofauti wanaohitaji huduma za feri . Nasisitiza kuwa Serikali inafaa kuchukua hatua mwafaka haraka iwezekanavyo. view
  • 18 Oct 2022 in Senate: On a point of Order, Madam, Temporary Speaker. view
  • 18 Oct 2022 in Senate: Bi Spika wa Muda, katika Mjadala unaoletwa katika hili Bunge, singependa kukueleza utakavyofanya. Najua kazi unafanya kisawasawa lakini haki na utendaji kazi lazima uende pamoja. Upande huu una haki ya kuchangia. Nashangaa kuwa unaelekeza pande moja waongee na upande huu huapewi nafasi. Sitaki kukosoa uamuzi uliofanya, lakini kwa wakati mwingine tukipata fursa kama hiyo ingekuwa bora utoe nafasi upande huu ili usikize maoni yao sawasawa. Isiwe kuegemea upande mmoja na kuwacha mwingine. view
  • 18 Oct 2022 in Senate: Bi. Spika wa Muda, cha kwanza ni kuwa Bunge letu la Afrika Mashariki linafika mwisho wake ifikapo mwezi wa 12. Kuna umuhimu tuwe tayari kufanya mikakati ya kuona ya kwamba kunao Wakenya wengine tutakaowachagua sisi wenyewe hapa Bungeni ili waweze kutuwakilisha katika lile Bunge la Afrika Mashariki. view
  • 18 Oct 2022 in Senate: Kama unavyoelewa, Bunge la Afrika Mashariki ni muhimu sana linaloweza kuleta mikakati ambayo sisi kama wananchi wa Afrika Mashariki tutashirikiana. Hivi sasa tuko Kenya, Uganda, Tanzania, Burundi na Rwanda. Hivi juzi tumepata kitinda mimba ambaye pia amekubali kuingia katika Bunge la Afrika Mashariki naye ni Sudan ya Kusini. view
  • 18 Oct 2022 in Senate: Itakuwa kiungo muhimu sana kwa Wakenya kuona kwamba ndugu zetu wa Sudan ya Kusini wameingia katika ushirika huu na katika Bunge la Afrika Mashariki. Ndio sababu, kwa umuhimu wao, ikaonekana ingekuwa vyema michezo hii ambayo hufanyika kila mwaka, mwezi wa kumi na mbili ifanyike Sudan ya Kusini. Ni michezo ambayo view
  • 18 Oct 2022 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus