18 Oct 2022 in Senate:
wanasiasa ama wabunge wa Bunge letu la Kitaifa la Bunge la Seneti hujumuika pamoja, tukaenda kucheza michezo mbalimbali inayoweza kusisimua misuli.
view
18 Oct 2022 in Senate:
Hata dada zetu pia wanaweza kujiunga na mambo ya mbio, ya kuvuta kamba na mengineo yanayoendelea katika ushirikiano huo. Bi. Spika wa Muda, kunao umuhimu kuweka kamati maalum ambayo inaweza kuangalia zile taratibu zimefuatwa vyema. Sababu kuu ni kuona ya kwamba wale wanataka kupigania hivi viti, kujihusisha ama kuchaguliwa kutuwakilisha katika lile Bunge la Afrika Mashariki wameweza kupitia kwa Kamati.
view
18 Oct 2022 in Senate:
Kuna umuhimu wa sisi kama Bunge la Seneti kuweza kukaa chini na kuchagua Maseneta ambao tunafikiria wana umuhimu sana katika ile kamati. Hao wataweza kuchunguza taratibu ili waweze kutuchagulia watu ambao watakuwa sawa sawa kwenda katika lile Bunge la Afrika Mashariki.
view
18 Oct 2022 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, katika hiyo Kamati, tumesomewa majina. Katika hayo majina, sisi tumeonelea ya kwamba wote ambao wamechaguliwa wanafaa kabisa katika zile nyadhfa. Wote waliochaguliwa pia wanao uwezo wa kutuwakislisha sisi kama Bunge katika Kamati ndogo itakayochunguza. Kwa hivyo, nina imani na yule aliyechaguliwa kama Mwenyekiti. Ni wakili aliyebobea, ndugu yetu Sen. Maanzo, Seneta wa Kaunti ya Makueni, na anayo tajriba ya kuifanya ile kazi. Vile vile, amekuwa akijihusisha sana na Korti la Afrika Mashariki. Amekuwa huko na amekuwa akifanya hizi kazi na zingine zinazohusiana na Bunge letu la Afrika Mashariki. Katika ile hali, tumeona yeye ana tajriba ya ...
view
13 Oct 2022 in Senate:
Asante, Bwana Naibu Spika. Kwanza ningetaka kuafiki Hoja na kusema kuwa nawaunga mkono Maseneta wanne waliochaguliwa kwenye orodha kwa kuwa iko sawa kabisa. Ningetaka pia kutaja kuwa kutoka Bunge hili la Seneti lianzishwe 2013, hakuna shida tumepata katika kuchagua Maseneta hawa wanne wa Jopol la Spika kwa sababu tumekuwa tunaachia jukumu hilo Bwana Spika mwenyewe. Kuanzia wakati huo mpaka hivi hakujakuwa na mjadala kwamba kuhusu Seneta atakayekuwa wa kwanza, pili, tatu au wa nne. Hili ni jukumu la ofisi ya Spika. Sioni kama kutakuwa na tashwishi katika hao Maseneta ambao wamechaguliwa. Kwa maoni yangu, wote watajukumika na wako na taaluma ...
view
13 Oct 2022 in Senate:
Thank you, Mr, Deputy Speaker, Sir. I second this Motion to approve the names of the Senators to serve in the Procedure and Rules Committee. The Senators mentioned here; Sen. Sheikh Mohammed Abass, MP, Sen. Joseph Nyutu Ngugi, MP and, Sen. Beth Kalunda Syengo, MP, are very capable Senators who can handle this Committee. I believe they will do a good job. I second.
view
13 Oct 2022 in Senate:
Mr. Deputy Speaker, Sir, I would like to second this Motion in the sense that the six persons named herein, who will be sitting in the Powers and Privileges Committee, are capable of handling this docket. In my humble view, all of them were selected after consideration by both sides of the divide. It is in this regard that our side nominated two and the other side nominated four and I believe that they will do a good job. I am confident that they will stand firm in their undertakings.
view
13 Oct 2022 in Senate:
Asante Bw. Naibu Spika. Kwa sababu ya kazi ambazo ziko mbele yetu, nitajaribu kufupisha mazungumzo yangu kidogo. Jambo la kwanza, ningependa kusisitiza ya kwamba katika hizi kamati zote 14 ambazo zimeteuliwa za kudumu, zote ni muhimu. Hakuna hata kamati moja ambayo tunaweza fikiria ya kwamba haitafanya kazi yake ama sio muhimu. Tuna imani kwamba katika wale Maseneta ambao wamechaguliwa katika hizi kamati tofauti, watatuonyesha utendakazi wao na ukakamavu wao. Ninaamini ya kwamba wataweza kuifanya hii kazi. Kuna hizi kamati 14 za Bunge hili letu la Seneti na kila Seneta hapa amewekwa katika ile kamati ambayo pengine alikuwa ameitaka ama ana ...
view
12 Oct 2022 in Senate:
Asante Bw. Naibu Spika. Kwanza nataka niunge mkono yote aliyosema ndugu yangu, Sen. Cheruiyot, kuhusu mjadala huu. Mjadala huu ni muhimu kwa sababu unaweza kuweka ratiba ya vile ambavyo tutaweza kufanya mambo yetu, majadiliano ndani ya Bunge hili la Senate kwa muda fulani ambao umewekwa kulingana na ratiba yetu. Bw. Naibu Spika, tunaona ya kwamba waliokuja hivi sasa katika Bunge la Senate wengi ni vijana na pia wamechanganyika na wazee kidogo. Itakuwa tena sio ile Bunge walikuwa wakisema wakati ule tulipoingia wakati wa 2013, kwamba hili ni Bunge la
view
12 Oct 2022 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view