Thomas Mwadeghu

Full name

Thomas Ludindi Mwadeghu

Born

1953

Post

Parliament Buildings
Parliament Rd.
P.O Box 41842 – 00100
Nairobi, Kenya

Email

wundanyiconstituency@yahoo.com

Email

Wundanyi@parliament.go.ke

Telephone

0724-285347

All parliamentary appearances

Entries 101 to 110 of 604.

  • 4 Oct 2016 in National Assembly: Nashukuru Mhe. Spika kwa kunipa nafasi hii niomboleze rafiki yangu wa dhati Mhe. Litole. Nilibahatika kuwa naye katika Bunge la Kumi. Naomba nichukue nafasi hii kutuma rambirambi kwa familia yake na jamii yake kwa ujumla. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 4 Oct 2016 in National Assembly: Nilipata nafasi ya kuandamana naye hadi nyumbani kwake na tukapata nafasi ya kuhudhuria ibada ya misa takatifu pamoja naye. Ni Mbunge niliyemfahamu na nikamjua. Nilipata nafasi ya kumwalika katika eneo langu la Bunge. Akaja hadi Taita na akawajua watu wangu. Nilimjua Litole kama Mbunge aliyeshughulikia watu wake kwa taaluma na azma nzuri. Ningependa kuchukua nafasi hii kuitakia familia yake uponyaji wa kiroho wakati huu wa majonzi. Naomba Mungu ailaze roho yake pahali pema peponi. view
  • 4 Oct 2016 in National Assembly: Ndiyo, Mhe. Spika. Nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ili niweze kutoa mchango kwa Mswada huu, ambao umezua hisia tofauti miongoni mwa wananchi na Wabunge. Kama tunavyojua, michango imeisaidia nchi hii, haswa wanafunzi na wagonjwa. Harambee zimetoa mchango wa kutosha katika nchi hii. Shida inatokea mchango unapochukuliwa kuwa kigezo cha uongozi bora, haswa inapodhaniwa kwamba kiongozi ambaye anazunguka nchini akitoa michango mingi ni kiongozi bora kuliko viongozi wengine, bila ya watu kufikiria kuhusu mahali ambapo kiongozi huyo anazitoa fedha hizo. Kuna uzuri wa michango. Ningependa kusema wazi kwamba katika eneo la Pwani, miradi mingi imefanywa kupitia michango. Shule nyingi zimejengwa kupitia ... view
  • 4 Oct 2016 in National Assembly: za vifo na wanafaa kusafirisha miili ya ndugu zao kutoka Nairobi hadi Mombasa au miji mingine. Mara nyingi tunaitisha michango. Tukiupitisha Mswada huu na kuharamisha michango, tutafanya nini? Sio familia zote zina uwezo wa kugharamia au kufidia gharama za matanga, na ujenzi wa shule na hospitali. Tukifunga michango kwa sheria basi tutawanyima watu hao nafasi ya kusaidiwa na wale ambao wana uwezo. Mara nyingi watu wanakutana na kuchanga kiasi kidogo cha pesa kwa muda fulani, na mwishowe wanaweza kumudu gharama iliyokuwa inawatatiza. Maoni yangu ni kwamba Mswada huu urekebishwe ili watu ambao watachangiwa kwa sababu moja au nyingine waweze kuwajibika ... view
  • 4 Oct 2016 in National Assembly: Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Naomba kutoa mchango wangu kwa suala la Shirika la Ndege la Kenya (KQ). Imekuwa tabia ya wanaotarajiwa kuyaongoza mashirika ya Kenya kuhakikisha kuwa yamefilisika. Labda wengine wenu hapa hamna uzoefu, The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 4 Oct 2016 in National Assembly: lakini nataka kuwaarifu kuwa miaka iliyopita, KENATCO iliingia katika shida hiyo. Shirika la Kenya Re wakati mmoja liliingia katika shida hiyo. Shirika la Kenya National Assurance nalo likazamishwa hivyo. Jusi tuliona National Bank of Kenya (NBK) nayo inataka kuzama. Kumbuka NBK ilitumiwa wakati ule wa kahawa za Chepkube. Shirika la Kenya Petroleum Refinery Limited limeuzwa hivyo hivyo kiholela na limeenda. Shirika la Kenya Cashew Nuts limeenda. Shirika la Kenya Meat Commission (KMC) mpaka sasa hatujui liko wapi. Mashirika kama Kenya Planters Co-operative Union, Kenya Farmers Association, orodha ni ndefu yamefilisika, na wale ambao wamehusika mpaka sasa wako na tunawajua. Naomba ... view
  • 31 Aug 2016 in National Assembly: Ahsante. Mhe. Spika. Nami nimesimama kuiunga mkono Hoja hii kwa maana kikao cha Kamati inayohusika na Shughuli za Bunge jana kilijadili utaratibu utakaofuatwa na kuamua kwamba litakuwa jambo la busara tuwe na kikao kesho asubuhi ili tupate nafasi ya kuishughulikia Miswada muhimu ambayo iko mbele yetu, na ambayo tunahitajika tuikamilishe kabla hatujaanza likizo ambayo inatarajiwa kuanza Ijumaa. Kwa hivyo, tunawaomba Waheshimiwa mkubali ombi hili ili tupate kumaliza shughuli hizi. Naliunga mkono ombi hili, Mheshimiwa Spika. view
  • 31 Aug 2016 in National Assembly: Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, ningependa kutoa shukrani kwa wakati huu ambao nimepewa kuunga mkono Mswada huu. Ni maoni yangu kuwa pale ambapo kuna vipengele ambavyo vinahitaji marekebisho, vifanyiwe marekebisho ili angalau tupate sheria ambazo zitadumu. Wakati umefika kwa sisi kuangalia kuwa wakati wa uchaguzi, wale ambao wanafanya dhambi wakati wa uchaguzi nao pia waadhibiwe vilivyo. Ningependa kuunga Mhe. Millie Odhiambo mkono kuwa lazima tuhakikishe tunapofanya mchujo, atakayepewa tiketi ya chama akifanya makosa lazima ahusishwe katika dhuluma ambazo zimetajwa na vipengle hivi ili aadhibiwe kwa mujibu wa sheria. view
  • 4 Aug 2016 in National Assembly: Asante, Mhe. Spika. Ninaomba nitoe maoni yangu kuhusu Hoja hii ya mchezo wa kamari. Ni mchezo ambao umezua hisia mseto kwa wananchi wa Kenya hasa ikibainika waziwazi kuwa watu wengi wamepoteza fedha kupitia mchezo huu. Nchi hii ilihalalisha mchezo wa kamari kitambo kwa madhumuni ya kusaidia shughuli kadhaa wa kadhaa za nchi na hasa wale ambao hawana nafasi nzuri ya kujiendeleza aidha kimasomo, kikazi au kibiashara. Baada ya muda, imebainika waziwazi kuwa mchezo huu umechukua mwelekeo mpya na umekuwa tatizo kwa familia nyingi kwa sababu umekuwa sasa ni uraibu. Watu wamefungwa vifungo vya ajabu na mchezo huu kwa sababu ya ... view
  • 4 Aug 2016 in National Assembly: Tukiendelea kuiwacha nchi hii ivamiwe na watu wa kila aina, watu wafanye biashara za kila aina vile wanavyotaka, tutajikuta katika shida na baadaye tutakuwa hatuna taifa. Tuna majukumu kama Bunge kuangalia kuwa tunawalinda vijana wetu na kupitisha sheria za kulinda nchi hii na fedha zake. Uraibu huuanza kimchezo. Huenda ikawa ni kunywa pombe, kuvuta sigara au kucheza kamari na baadaye inakita mizizi katika fikira zako kiasi kwamba ukikosa kulifanya hilo jambo, hauna raha na amani na hata katika familia italeta kero. Ombi langu ni Bunge kupitia Kamati hii, lifikirie kwa makini jinsi litakavyo chambua kwa undani na kubainisha chanzo cha ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus