Thomas Mwadeghu

Full name

Thomas Ludindi Mwadeghu

Born

1953

Post

Parliament Buildings
Parliament Rd.
P.O Box 41842 – 00100
Nairobi, Kenya

Email

wundanyiconstituency@yahoo.com

Email

Wundanyi@parliament.go.ke

Telephone

0724-285347

All parliamentary appearances

Entries 111 to 120 of 604.

  • 4 Aug 2016 in National Assembly: imekita mizizi na wengi wanalifurahia na kuuona ndio mchezo wa kufuata? Wengi wako tayari hata kukopa pesa kwa benki kufadhili mchezo huu. Ninaomba kuweka tamati kwa kupendekeza kuwa ikiwezekana, Wabunge watunge sheria ya kutoa mwongozo katika mchezo huu wa kamari. Hivi sasa, sheria haziko, mradi tu mtu anapewa cheti, ako huru kufanya vile anavyotaka. Hakuna sheria ya kueleza kuwa ni mtu mwenye umri fulani ambaye anaweza kuingia katika mchezo huu wa kamari. Mradi tu uwe na uwezo na uamue kule uliko ukiwa mwanafunzi au mtoto mchanga, wao hawana haja ya kujua. Kuna sheria zinazowalinda watoto. Je, hivi sasa, vile hali ... view
  • 26 Jul 2016 in National Assembly: Nashukuru, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa nafasi hii nami nitoe mchango wangu kwa Mswada huu unaotoa mwongozo wa matumizi ya fedha za umma. Ijapokuwa umeshatoa uamuzi kuwa si muhimu tuwe na Ripoti ya Kamati ili kujadili Mswada huu, naomba nitoe mapendekezo kuwa lingekuwa jambo la busara sana kama Ripoti ya Kamati ingekuwa imejadiliwa Bungeni ili Wabunge wapate mwongozo na mwelekeo wa kuchangia kwa undani Mswada huu. view
  • 26 Jul 2016 in National Assembly: Nashukuru, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia mwelekeo. Kabla sijatoa mapendekezo yangu, wacha nifafanue kuwa niko na nia ya kugombea kiti cha ugavana katika Kaunti ya Taita Taveta 2017 lakini haimaanishi ningependa kupigania kiti cha ugavana wakati huo na sheria mbaya. Singependa niwe gavana na sheria mbaya ambayo itawafanya wafanykazi waendelee na wizi ambao ninauona. Ningependa niwe gavana ambaye atafuata sheria. Ndio maana ninapendekeza sheria hii ibadilishwe ili magavana wasiwe wanaweza kupunja na kutumia fedha za umma kiholela kama vile tunavyoona hivi sasa. Tukiangalia hali ilivyo hivi sasa, kuna mambo matatu ambayo ningependa nichangie kwa undani. Kwanza, vipengele vya ... view
  • 26 Jul 2016 in National Assembly: Mhe. Naibu Spika wa Muda, nikikumbuka mwaka jana katika zoezi hili la Mwongozo wa Sheria za Matumizi ya Serikali, tuligeuza na kusema kuwa Wizara ya Fedha ina idhini ya kutumia pesa kulipia ada ya mikopo yote kutoka nje. Ilipokuja mambo ya ‘Euro Bond’, hawa mabwana walihakikisha kuwa zile fedha zilipoingia, badala ya kuleta hapa Bungeni vile zilivyo, The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 26 Jul 2016 in National Assembly: walizitumia kulipa ada zingine huko nje. Walipoulizwa kilichotendeka, walisema kuwa wamezitumia. Tulipouliza kwa idhini gani, walisema kuwa tulikuwa tumeipitisha sisi wenyewe. Kipengele hicho kiangaliwe na wanyimwe hiyo ruhusa ili wasikope pesa na kuzitumia huko nje. view
  • 26 Jul 2016 in National Assembly: Wenzangu wamechangia kwa undani kuhusu upotovu, kukosa nidhamu na jinsi magavana wanavyotumia pesa za umma. Ugatuzi ulikuja ili tuwe na usawa na watu wasaidike mashinani. Lakini yanayotendeka ni kuwa kandarasi zinapeanwa kiholela na hakuna makadirio ambayo yanafuatwa. Ya kusikitisha ni kuwa kuna kodi ambayo ilikuwa inachukuliwa tangu hapo awali tulipokuwa na mabaraza ya miji. Fedha hizi zilikuwa zinaonekana waziwazi. Kwa mfano, katika Kaunti ya Taita Taveta, tulikuwa tunachukua Ksh140 milioni kutoka Soko la Taveta, lakini tangu ugatuzi uingie, ada imeshuka hadi Ksh80 milioni. Shiling milioni sitini zimeenda wapi? Wanaajiri wafanyikazi na kuwalipa Kshs18,000 kwa mwezi na wanaleta kodi ya Ksh3,000. ... view
  • 26 Jul 2016 in National Assembly: Nikimalizia, ningependa sheria hizi zigeuzwe ili tuhakikishe usawa na haki. Kuna ndeni ambalo litawachwa na magavana wakati huu, kwa sababu katika makadirio yao, wanaweza kutoa kandarasi lakini hawatailipia. Wataipeleka mbele kwa makadirio ya mwaka ujao. Kwa hivyo, kila wakati kuna deni na hili deni linaendelea kukua. Hii nchi itajikuta iko katika matatizo na imejitia kitanzi. Ndiyo maana naunga mkono Mswada huu. view
  • 6 Jul 2016 in National Assembly: Nakushukuru, Mhe. Naibu Spika, kwa kunipatia nafasi hii ili nitoe maoni yangu kuhusu Ombi ambalo limeletwa na Mhe. wa Igembe Kaskazini. Kitengo cha wanyama wa pori kinachoitwa KWS kimekuwa na tabia na uzoefu wa kuingilia ardhi za umma na kusongesha ardhi kiholela. view
  • 6 Jul 2016 in National Assembly: Nasahihishwa kuwa ni Mhe. wa Igembe ya Kati, samahani. Kitengo cha ndugu zetu ambao wanashughulika na wanyama wa pori kinauzoefu wa kujisongeshea ardhi kiholela. Kwa mfano, kule Taita, kutoka Maungu hadi Voi, upande wa chini wa reli, katika mwaka wa 2009, KWS ilijisongeshea ardhi ambayo ni ya wananchi. Watu wa sehemu hiyo wamepitisha ombi lao na litakuja kwa Spika. Ukienda Tsavo, pale ambapo watu walishambuliwa na Simba wakati wa kujenga reli kuu, KWS imefanya dhuluma hizo. Pia, imefanya dhuluma katika sehemu za Taveta. Tukienda Kishushe, wameweka ua ambalo sila stima lakini wameliingiza ndani ya ardhi ya wananchi. Hawakuweka ua upande ... view
  • 6 Jul 2016 in National Assembly: Wakati umefika Bunge liingilie kati lione kuwa ardhi ya wananchi imerudishwa na wanyama wasionekana kama ndio wanahitaji ardhi kuliko wananchi. Haya maombi yote yako jiani. Niko katika Kamati ya Ardhi na nimemsikia Mhe. Makali kuhusi bodi cha mashamba. Tulimuita Waziri ambaye anahusika na shughuli za mashamba na bodi, na alituhakikishia kuwa bodi zitarudishwa na Wabunge watahusishwa wakati watu wanapoteuliwa kwa hizo bodi. Namshukuru mwenzangu, Mhe. wa Igembe ya Kati kwa kuleta Ombi hili kwa niamba ya watu wake. Ombi langu la Wataita pia liko njiani. Limefika Bungeni na tunatarajia hivi karibuni pia nalo litasomwa. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus