6 Jul 2016 in National Assembly:
Ahsante, Mhe. Spika. Naomba kuunga mkono Kamati hii ya Uteuzi vile ilivyosomwa na mwenzangu ili ikaanze kufanya kazi yake haraka iwezekanavyo. Uteuzi wa Kamati hizi saa zingine unachangamoto zake. Ni ombi langu kwa Waheshimiwa wahakikishe wamebainisha ni akina nani wanaweza kuwa kwa Kamati hizi. Mara nyingi, inabidi uangalie vile utakavyosambaza wenzako katika Kamati mbalimbali. Kamati ya Ratiba za Bunge ilionelea haya majina yaletwe mbele ya Bunge hili ili Wabunge wafikirie na kuyaweka maanani, ili yaidhinishwe na uteuzi huu uweze kufanya kazi. Kwa hayo machache, Mhe. Spika, naomba kuunga mkono uteuzi wa Kamati hii.
view
6 Jul 2016 in National Assembly:
Mhe. Spika, ninaunga mkono Hoja hii. Tumemsikia Mhe. Gumbo vile alivyotoa maoni yake kuwa inabidi tuweke wasomi katika Kamati hizi. Mhe. Spika, nimesikia mara nyingi ukitoa mwongozo hapa Bungeni kuwa Wabunge wote wako sawa mbele ya Bunge, wawe wamesoma au bado hawajasoma, mradi tu wananchi wameona waje Bungeni. Wana haki yao ya kuwawakilisha watu wao katika sehemu wanayotoka. Ijapokuwa nimemuelewa Mhe. Gumbo yale anayoyasema kuwa angependa kuwaona wasomi peke yake, ninamuomba arudi pale tumeanzia. Kama wananchi wataona inafaa walete watu ambao kisomo chao, kulingana na Mhe. Gumbo, ni hafifu na hakilingani vile Mhe. Gumbo anavyoona, basi mimi kama mmoja wa ...
view
6 Jul 2016 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Spika. Naomba kuunga mkono Kamati hii ya Haki na Sheria ambayo kusema ukweli ilikuwa hapo awali, lakini kwa sababu moja au nyingine ikabidi wanakamati wa CORD watolewa kwa muda. Tuliyaweka na kuyachukulia maanani maamuzi yako. Wakati mwingine lazima tupewe mwelekeo. Tumekubali hawa wanakamati wajiunge na wenzao wa upande ule mwingine ili wapate kutimiza majukumu yao.
view
6 Jul 2016 in National Assembly:
Kamati hii naiona ni ya wasomi kwa maana wengi wao ni wana sheria. Nina imani kwa sababu itakuwa ikiangalia mswala kadhaa ya sheria. Kama, ujuavyo sheria inavipengele vyake ambavyo mtu asipo vitafsiri vizuri vinaweza kutuletea sisi Wabunge shida. Tumejaribu tuwezavyo na ni ombi langu kuwa kamati hii itaendelea na kazi yake mahali ilipokuwa imefikisha. Hivi sasa kuna kazi muhimu ya kuangalia mambo ambayo yasipoangalia vizuri yanaweza kuelekeza nchi hii vibaya.
view
6 Jul 2016 in National Assembly:
Kamati hii kwangu ni ya umuhimu sana. Naomba mwenyeketi wake, Mhe. Chepkong’a, awakubali wenzake waendelee na kazi. Awajibike ya kutosha kuwaelezea yale walitimiza wakati walikuwa nje kidogo ili washike dau pamoja na kumaliza kazi bila shida yoyote.
view
6 Jul 2016 in National Assembly:
Mhe. Spika naomba kuunga mkono.
view
6 Jul 2016 in National Assembly:
Asante, Mhe. Spika. Wakati mwingine cheche zinazoletwa hapa Bungeni na wenzangu huonekana kuwa mambo yanayomtoa mtu hadhi. Sikulenga mtu yeyote katika barua yangu au matamshi yangu yawe ni ya kuudhi mtu yeyote. Mhe. Chepkong’a amefanyiwa kazi na dadangu kwa muda mrefu sana na tumejuana tangu hapo awali. Ameniudhi mara nyingi lakini sijawahi kusema. Leo hii, amekiri kuwa amefanyiwa kazi na mmoja wetu. Tumemhudumia kwa muda mrefu na asingeweza kupanda iwapo hatungemsaidia. Mhe. Chepkong’a ni rafiki wangu na tunaweza kuyatatua mambo haya bila shida yoyote iwapo The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version ...
view
6 Jul 2016 in National Assembly:
ameathirika. Sisi ni watu wazima. Mtu huomba msamaha iwapo ameelezwa kuwa umemuudhi mwenzake na kama ameudhika, basi haikuwa nia yangu kumuudhi. Ni uanadamu wako umekufanya ukaudhika. Natumai tumeyamaliza haya.
view
6 Jul 2016 in National Assembly:
Nimeeleza kuwa mambo haya yameisha. Mhe. Spika, shida ya Kiswahili ni hio. Hapakuwa na nia yoyote kumuudhi. Yaliyopita si ndwele, tugange yajayo.
view
22 Jun 2016 in National Assembly:
Asante Mheshimiwa Spika kwa kunipa nafasi hii ili nami nitoe mchango wangu kwa Mswada huu. Wakati uliopita, niliomba mjadala uahirishwe kwa sababu Wabunge hawakuwa wa kutosha Bungeni. Ndio maana nikaomba angalau tusubiri mpaka siku The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view