Thomas Mwadeghu

Full name

Thomas Ludindi Mwadeghu

Born

1953

Post

Parliament Buildings
Parliament Rd.
P.O Box 41842 – 00100
Nairobi, Kenya

Email

wundanyiconstituency@yahoo.com

Email

Wundanyi@parliament.go.ke

Telephone

0724-285347

All parliamentary appearances

Entries 221 to 230 of 604.

  • 27 Oct 2015 in National Assembly: Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda, ninaomba nisikizwe. Jogoo likikutana na mwamba halizingatii kuvunja mwamba lakini huwa linazunguka mwamba. Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda ninaomba umfahamishe Mhe. Duale kwamba nasi pia tulienda shule na si yeye pekee alienda shule. Ninataka pia nikuambie, avumaye baharini ni papa lakini pia kuna nyangumi. Sio lazima kila wakati yale Duale amesema yachukuliwe kama Bibilia. Wakati umefika Mhe. Duale pia aambiwe kuwa ubabe wake si ule utakua unatupeleka kila mahali. view
  • 27 Oct 2015 in National Assembly: Mhe. Duale, ninaomba utulie. Ninasema hivi, wakati umefika ambapo wakati hizi sheria zinapopitishwa, jamani tuangalie tuone kama tunaweza kuahirisha kikao hiki. Kama kinaweza kuahirishwa, kiahirishwe ili tupate muda wa kuzingatia haya mambo ili tumalize hii sheria. view
  • 27 Oct 2015 in National Assembly: Asante, Mhe. Naibu Spika. Naomba nitoe mchango wangu kwa Mswada huu ambao umekuja wakati huu. Naunga mkono Mswada huu ijapokuwa kuna mapendekezo mengi muhimu ambayo yanahitajika katika Mswada huu ili unufaishe watu wa nchi hii. Kama tunavyojua, mafuta yamepatikana katika pembe nyingi za nchi. Mara nyingi watu ambao wanaishi karibu na maeneo ambapo rasilimali kama hii zimepatikana ndio wanaokuwa hawana chochote na hawawezi kujimudu, huku mafuta yakitolewa na kusafirishwa. Wale ambao wanapata faida ya mafuta hayo sio wenyeji wanaoishi mahali pale. Wenyeji wa maeneo hayo utawakuta hawana namna ya kuishi. Mapendekezo yangu wakati tutakapokuwa tunatoa marekebisho ni angalau jambo hili ... view
  • 27 Oct 2015 in National Assembly: Kama tunaweza kukumbuka,Tanzania iligundua gesi hivi juzi. Ilipogundua gesi, watu wa sehemu ya kusini mwa Tanzania walianza kukataa gesi hiyo isichimbwe kwa sababu walijua mara nyingi gesi ikichimbwa na kupelekwa nje ya jiji au kusambazwa nje, hawapati manufaa. view
  • 14 Oct 2015 in National Assembly: Asante, Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda. Ninasimama kuunga mkono kuondolewa kwa kipengele hiki, kwa sababu waandishi wa taarifa na mtu yeyote ana haki ya kupata taarifa zote. view
  • 14 Oct 2015 in National Assembly: Asante kwa nafasi hii, Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda. Kipengele hiki kinahujumu Wabunge vile kilivyo. Kuhusu nguvu zinazopendekezwa kwa maafisa wa usalama humu ndani, nina uoga na wasiwasi kuwa watatumia nafasi hiyo vibaya. Kwa hivyo, namuomba aliyeanzisha kipengele hiki, Mhe. Keynan, atafute mbinu ya kukiondoa ili ahakikishe kuwa kimerekebishwa ili kilete sera aliyoitaka katika sheria hiyo. Sikubaliani na hiki kipengle kabisa. view
  • 9 Jul 2015 in National Assembly: Ahsante sana Mhe. Spika. Ninasimama kuunga mkono Hoja hii vile ilivyopendekezwa na Mheshimiwa ambaye anaongoza upande wa Serikali. Tukiangalia sheria zetu, zinaturuhusu kuangalia kama Kamati zinaweza kuunganishwa ili tuwe na Kamati moja ambayo ina upande wa Seneti na upande wa National Assembly. Ni jambo ambalo limefikiriwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 9 Jul 2015 in National Assembly: na tunaomba Waheshimiwa walikubali ili tupate kuona kuwa maslahi ya Waheshimiwa wa Seneti na wa Bunge la Kitaifa yanatimizwa. Kwa hayo machache, naunga mkono Hoja hii. Ahsante. view
  • 9 Jul 2015 in National Assembly: Hon. Speaker, I second. view
  • 8 Jul 2015 in National Assembly: Asante, mhe. Spika. Nashukuru kwa kupata nafasi hii kutoa mchango wangu kuhusu Hoja hii. Kwanza, ningependa kumpongeza kakangu kwa kuileta Hoja hii Bungeni ili ipate kujadiliwa. Ninaomba kuwaheshimu Wabunge wote ambao wameweka sahihi za Hoja hii. Inamaanisha kwamba Wabunge hao walikaa chini na kutafakari kwa kina. Ndiyo maana wakaweka sahihi zao kwenye Hoja hii. Nimesikia mambo mengi ambayo yamesemwa. Nikatulia niyasikie na kuyafahamu. Ninawashukuru wenzangu kwa sababu wamekubali kwamba Prof. Kaimenyi ni mjeuri na hasikii. Ni mtu ambaye anafuata nyayo za mhe Duale za ujeuri na ubabe. Anaishi maisha ya ubabe na kuonyesha kuwa yeye ndiye mambo yote. Watu wa ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus