8 Jul 2015 in National Assembly:
Mhe. Spika, aisifuye mvua imemnyeshea. Kama huyu shangazi amependezwa na Duale na ubabe wake ni sawa; sina shida naye.
view
8 Jul 2015 in National Assembly:
Mhe. Spika, ninaomba kumfahamisha mwenzangu kwamba ukizoea wa nazi, wa samli huuwezi.
view
8 Jul 2015 in National Assembly:
Mhe. Spika, ninamheshimu sana ndugu yangu Kaimenyi kwa sababu ametimiza majukumu yake, lakini kuna mambo ambayo yamemlemea. Hadi sasa shule hazina bodi. Tukiliangazia suala hilo, mutakubaliana nami kwamba huyu bwana amelemewa na majukumu yake. Sina shaka kwamba ndugu yangu Kaimenyi ni msomi. Ana sifa za usomi, lakini tusipotoke kwamba mtu anaweza kutekeleza majukumu kwa sababu ya usomi. La! Majukumu mengine The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
8 Jul 2015 in National Assembly:
yanamshinda licha ya kwamba ni majukumu ya elimu. Tukiangalia jinsi nchi hii inavyoendelea, na tukimwacha ndugu yetu Kaimenyi aendelee---
view
8 Jul 2015 in National Assembly:
Bw. Spika, mheshimiwa anasema hanielewi. Nitamufafanulia jioni tukikutana baada ya futari yake. Kwa sasa, ninaomba aniache niyaseme. Aelewe asielewe, hiyo ni shida yake. Mhe. Spika, ninawomba Wabunge watafakari iwapo wanataka Prof. Kaimenyi aendelee na kazi ama aondoke. Hoja hii inasema tuangalie kama tunaweza kumptatia nafasi nyingine ama la, lakini tumeambiwa kwamba Bunge hili litateua kamati maalum kuangalia jinsi anavyofanya kazi; na kwamba kwa sasa tuendelee mbele ili tuipatie kamati hiyo nafasi ya kuifanya shughuli hiyo. Maoni yangu ni kwamba sidhani kama Prof. Kaimenyi anaweza kuyatekeleza majukumu kwenye kitengo cha elimu. Matatizo aliyonayo ni mengi. Kama angeliweza kuketi chini na kuzungumza ...
view
8 Jul 2015 in National Assembly:
Mhe. Spika, nilitaka kueleza Kaimenyi ni mtu wa aina gani.
view
8 Jul 2015 in National Assembly:
Mhe. Spika, nimeyaelewa mambo ambayo ndugu yangu amesema. Mhe. Chepkong’a ni mtu ambaye ninamheshimu sana, lakini hapa hatuzungumzi kuhusu ng’ombe wa Wakalenjin; tunazungumza kuhusu ng’ombe wa Njuri Ncheke kule Meru.
view
8 Jul 2015 in National Assembly:
Mhe. Spika, naomba tu nimalize kwa kusema kuwa tukubaliane kuwa Kipengele cha 10 cha Katiba kinasema yeyote anaweza kufasiri Katiba. Nimeisoma. Mtu yeyote anaweza kufasiri Katiba. Vile tumeifasiri, tunaomba Bunge lionyeshe huu uwe ni mfano kwa wenzetu ambao wamepewa nafasi za kuhudumia nchi hii. Kama hawaendi kulingana na matakwa ya wananchi, basi Bunge litoe nafasi ya kumuita Kaimenyi aje aangaliwe. Natumai mnaelewa na yale ninasema. Nasema Bunge litoe nafasi Kaimenyi aitwe aje aeleze upande wake maana lazima apewe nafasi. Ndio tunasema kuwa hiyo kamati ikiundwa impe nafasi ajieleze. Kama atapatikana na makosa, ataadhibiwa. Kwa sasa, naomba tukubaliane, tuipitishe hii Hoja ...
view
8 Jul 2015 in National Assembly:
Kwa hayo mengi mhe. Spika, naomba kuunga mkono Hoja hii. Asante.
view
1 Jul 2015 in National Assembly:
Which county?
view