24 Jun 2015 in National Assembly:
. Lile ambalo naona bado lina kero ni fedha ambazo zimewekwa katika kitengo cha elimu. Hapo awali, tulikuwa tumeweka Ksh11,000 kwa kila mwanafunzi kwa mwaka. Sasa zimeongezwa zimefika Ksh13,000 kwa mwaka kwa kila mwanafunzi. Lakini tukiangalia Ksh13,000 kwa kila mwanafunzi, haziwezi kufadhili mwanafunzi kusoma kwa mwaka mzima. Ndio maana katikati, unaona kila wakati wanafunzi wanaambiwa warudi nyumbani. Tunatarajia wakati utafika ambapo tutasema kuwa kama elimu ya sekondari inafadhiliwa kikamilifu na Serikali, basi iwe kweli inafadhiliwa kikamilifu na Serikali. Fedha zitengwe za kutosha. Wanafunzi wakilipiwa karo, basi wajue wanaenda muhula wa kwanza mpaka wamalize muhula wa mwisho bila kuambiwa na walimu ...
view
24 Jun 2015 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika, naomba niweke tamati nikiunga mkono ugavi wa fedha hizi. Ni matumaini yangu kwamba Mswada huu utapitishwa, na kwamba miradi inayoendelea itatekelezwa vyema na wala haitatekelezwa kiholela kama ilivyofanyika mwaka jana. Kandarasi ya kujenga barabara ya kutoka Voi kwenda Mwatate hadi Wundanyi ilitolewa lakini baadaye, Serikali ikakataa kuufadhili mradi huo na mwenye kandarasi akaondoka. Rais alipoenda Taita- Taveta hivi juzi, alisema mwenye kandarasi atarudi mwezi wa kwanza na, ghafla bin vuu, akarudi. Naomba kwamba kwenye miradi inayofadhiliwa na Serikali, kusiwe na ukora. Haki ifanywe na fedha zitumike vyema ili miradi yote ikamilike.
view
24 Jun 2015 in National Assembly:
Kwa hayo mengi, naomba kuunga mkono Mswada huu.
view
17 Jun 2015 in National Assembly:
Ahsante, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Naomba nami nichangie Hoja hii kuhusu gharama za ndoa na vile ndoa zimekuwa haziwezi kufanyika hivi sasa kwa sababu ya matatizo ambayo yameletwa hasa na Serikali. Tulipopitisha Mswada wa Ndoa wakati mwingine, hatukutarajia kuwa baadaye Serikali itageuka iseme kuwa itaweka sheria ya kusema kuwa yule ambaye anataka kufunga ndoa lazima asafiri hadi makao makuu ambayo yamepangwa na Serikali. Nikitoa mfano, watu wangu wa Taita watoke Taita waende Mombasa ama waje Nairobi ndio waweze kupata cheti cha ndoa.
view
17 Jun 2015 in National Assembly:
Utakubaliana nami kuwa cheti cha ndoa ni muhimu na kila mtu anakihitaji ili kuthibitisha kuwa amefunga ndoa na mtu na kuwa wale watoto ambao Mungu amewajalia mkapata wametokana na ile ndoa mliofunga. Tatu, mmoja wenu akiwa hayupo na ameaga ndunia, mali mtaigawanya namna gani ama ni nani ataachiwa mali? Mkiwa mnamiliki mali, nani ataweza kumiliki hiyo mali? Lakini hivi sasa, imekuwa ni kero kubwa kwa mtu yeyote anayetaka kuoa mwenzake ama kuolewa na mwenzake. Inambidi, licha ya kutoa mahari, agharamie usafiri kwenda kutafuta cheti na asajiliwe. Badaye, ndio arudi tena kanisani kuja kufunga ndoa. Swali tunalouliza ni: Kwa nini tumeweka ...
view
17 Jun 2015 in National Assembly:
ni “ Come, let us stay” Hiyo sio nia yetu. Nia ilikuwa kutafuta taratibu ambazo zinaweza kukubaliwa ili watu wakiamua wakae pamoja, waweze kuenda pahali ambapo wanahitaji wapatiwe cheti na mtu ambaye amethibitishwa kuwa amehitimu kufunganisha ndoa. Hivi sasa, tumeshindwa kuheshimu kanuni za ndoa kwa sababu tumeifanya iwe ghali mno. Watu wameamua tu wataondoka manyumbani mwao waje wakae kwa sababu wanaogopa zile gharama.
view
17 Jun 2015 in National Assembly:
Ombi letu ni hili: Katika kila kaunti, kuwe na ofisi ambayo imesajiliwa na ina msajili ambaye anaweza kuandikisha, kufunga ndoa na kupeana cheti. Nakubaliana na mawazo ambayo yalitolewa hapo awali kuwa mara nyingine, kulikuwa na watu bandia ambao walijitokeza wakaanza kufunga watu ndoa na kuwapatia vyeti. Lakini hilo halimaanishi watu wote waadhibiwe kwa ujumla. Tunaomba irudishwe pale ilipokuwa na makanisa yakubaliwe kutoa vyeti vya ndoa pale pale ambapo watu wanaamua waoane ama wafunge ndoa.
view
17 Jun 2015 in National Assembly:
Ndugu zetu waislamu wana bahati. Hawakuhusishwa na sheria hii kwa sababu makadhi kokote walipo wanaweza kufungisha ndoa zao. Lakini sisi wakristo tuna shida kubwa sana kwa vile watu lazima wasafiri ndio waende kupata vyeti. Halafu ile ilani ambayo inahitajika ni kubwa. Unatakiwa kutoa ilani siku 21. Katika wakati huo, hauwezi kupanga kitu chochote kwa sababu haujui ikiwa ilani italeta kero na mtu mwingine ataenda asimamishe hiyo ndoa. Kwa hivyo, tunaomba kuwa gharama za ndoa zirudi chini. Tuhakikishe kuwa ofisi zimetengwa katika kila sehemu ya kaunti. Watu waweze kufungishwa ndoa na wale ambao watasajiliwa kuweza kupeana vyeti wawe ni watu wa ...
view
17 Jun 2015 in National Assembly:
Kwa haya machache, naomba kuunga mkono Hoja hii. Asante, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda.
view
16 Jun 2015 in National Assembly:
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili nami nitoe mchango wangu kwa Ripoti hii ya Kamati ya Uwekezaji. Kiwanda hiki ambacho kuanzia mwaka wa 2007 - katika mahojiano na makubaliano ya Baraza la Mawaziri - ilikubalika wazi wazi kuwa kinahitaji kuboreshwa ili Serikali ya Kenya iwe na zile hisa zake theluthi hamsini na mwekezaji mpya aje achukue nafasi ya BP, Shell na Chevron, ambao ndio walikuwa wanashikilia hisa hizo nyingine. Jambo la kushangaza ni kuwa ombi lilipotumwa kwa mashirika mbalimbali ya ulimwengu, kati ya mashirika yaliyoomba kuingia na kumiliki hizo hisa, ilikuwa kampuni ya Essar ...
view