1 Apr 2015 in National Assembly:
Asante sana, mhe. Naibu Spika wa Muda. Naomba nami nitoe mchango wangu kwa Hotuba ya Rais kuhusu hali halisi ya nchi yetu. Nitazungumzia masuala kadha wa kadha. La kwanza ni uwajibikaji wa wananchi kuhusu usalama. Nakubaliana na Rais kuwa usalama ni jukumu la kila mmoja wetu na lazima tufanye bidii ili tuhakikishe kuwa unaimarishwa. Hata hivyo, naomba pia nitoe maoni yangu kuhusu ugatuzi na jinsi ufisadi unavyoendelea huko mashinani. Tunaulizana ni lipi linaendelea. Rais ametuletea orodha hii hapa Bungeni. Wale Wakristo ambao wako hapa wananisikiza wanajua kwamba wayahudi walipotaka kumsulubisha Yesu walimpeleka kwa Pilato. Pilato aliona mambo ni magumu akanawa ...
view
1 Apr 2015 in National Assembly:
barabara. La sivyo, huyu ambaye amepewa hiyo kandarasi hangeshindwa kutekeleza wajibu wake wa kumaliza barabara hiyo. Maafisa wa ardhi nao wanachangia sana katika ufisadi. Nikiangalia sehemu kama ya Msambweni pale Voi, mtu alipewa nafasi ya kujenga kiwanda cha Bata. Kilipomshinda akauza na hivi sasa mwenyewe anataka kuwafukuza wananchi ilhali alishindwa kujenga kiwanda cha Bata. Naomba huu ufisadi ambao umekita mizizi nchini uangaziwe ili sote tupate kuokoka na kutoka kwa ufisadi. Labda lingekuwa jambo la busara wale ambao wamefanya ufisadi---
view
1 Apr 2015 in National Assembly:
barabara. La sivyo, huyu ambaye amepewa hiyo kandarasi hangeshindwa kutekeleza wajibu wake wa kumaliza barabara hiyo. Maafisa wa ardhi nao wanachangia sana katika ufisadi. Nikiangalia sehemu kama ya Msambweni pale Voi, mtu alipewa nafasi ya kujenga kiwanda cha Bata. Kilipomshinda akauza na hivi sasa mwenyewe anataka kuwafukuza wananchi ilhali alishindwa kujenga kiwanda cha Bata. Naomba huu ufisadi ambao umekita mizizi nchini uangaziwe ili sote tupate kuokoka na kutoka kwa ufisadi. Labda lingekuwa jambo la busara wale ambao wamefanya ufisadi---
view
25 Mar 2015 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika wa Muda, nashukuru kwa nafasi hii ambayo umenipatia nimpongeze mhe. (Bi.) Joyce Lay kwa Hoja hii ambayo ameileta Bungeni asubuhi ya leo. Naomba pia nitumie nafasi hii kumshukuru.
view
25 Mar 2015 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika wa Muda, nikimkumbuka Rais wa Tanzania, mhe. Julius Kabarage Nyerere, ambaye alikitafsiri kitabu chake cha Uhuru WaWatumwa, natumaini kwamba tunaelekea kupata uhuru wetu. Sheria za nchi yetu zimeandikwa kwa lugha ya Kiingereza. Hoja hii inaomba wanaohusika watafsiri sheria zetu zote, pamoja na Katiba, kwa lugha ya Kiswahili; ambayo ndiyo lugha inayoeleweka na wengi. Tukiangalia ule udhalimu waliofanyiwa Wakenya, utaona kwamba mara nyingi waadhiriwa wanashindwa kueleza kwa lugha ya Kiingereza kwa sababu lugha ambayo wanaifahamu ni Kiswahili. Mara nyingi, washukiwa wanapopelekwa mahakamani, wakalimani ambao wameajiriwa kutafsiri lugha ya Kiingereza mara nyingi huwapotosha washtakiwa. The electronic version of the ...
view
25 Mar 2015 in National Assembly:
Mhe. Spika, tulipoipitisha Katiba mwaka wa 2010, tukaingia katika sera ya ugatuzi, moja ya vipengele ambavyo vinahusika ni makadirio ya fedha za kaunti. Makadirio hayo huandikwa kwa lugha ya Kiingereza, na watu hawaelewi. Utakuta fedha ambazo zinaombwa na kaunti zimeandikwa kwa Kiingereza na wananchi wanashindwa watajikwamua namna gani kutoka kwa hali hiyo ili wapate kuyaelewa makadirio hayo. Wakitaka kuyapitisha, mara nyingi wanayapitisha kwa sababu ya maelezo wanayopata kutoka kwa wahusika, ambao huwadanganya wananchi kua wamefanya marekebisho kwa sababu ya shida ya lugha. Mazungumzo yetu ya kawaida hufanywa kwa Kiswahili. Ninapochangia Hoja na Miswada hapa Bungeni, mara nyingi mimi hutumia lugha ...
view
25 Mar 2015 in National Assembly:
Thank you, hon. Temporary Deputy Chairman. Let us agree on something. The Auditor- General is an external auditor; he is not expected to be stationed in a particular county, or station. For that matter, what he requires is adequate staff to go round once the audit begins and complete the audit within a time frame that is stated in law. He needs not have his presence in every county. This will be an expensive affair, and for that matter I tend to think that this will become a money Bill. That is what I am trying to avoid. With due ...
view
18 Mar 2015 in National Assembly:
Ahsante Naibu Spika wa Muda, kwa fursa hii ambayo umenipa nami niweze kutoa maoni yangu kuhusu Hoja hii. Kwanza, naunga mkono Hoja hii kwa dhati. Ni jambo la kushangaza kuwa wenzangu wanasema ni vibaya kuorodhesha shule ama wanafunzi ambao wamehitimu vyema katika mitihani ya taifa. Tunaorodhesha shule ambazo zimefanya vyema ili umma upate kujua ni wapi matokeo yamekuwa mazuri. Watu watajiuliza ni kwa nini matokeo yamekuwa mazuri. Huenda ikawa ni kwa sababu ya vifaa vizuri vya shule, walimu, mazingara nakadhalika. Tusipoorodhesha shule na wanafunzi, ni lini umma utajua sehemu fulani inafanya vyema kuliko sehemu nyingine? Tusipofanya hivyo fedha za serikali ...
view
18 Mar 2015 in National Assembly:
wanafunzi wanashindana katika mazingara ambayo ni sawia. Shule za hapa jijini Nairobi zina vifaa. Kwa hivyo walimu wanakimbilia huku. Wale waliobaki mashinani wana shida zao. Shule huko hazina vifaa. Kama Serikali itahakikisha imesambaza vifaa na walimu wazuri wanabaki mashinani, basi wanafunzi watakuwa wakishindana katika mazingara sawasawa. Kwa hivyo, naunga mkono Hoja hii. Nawasihi Wabunge wenzangu wafikirie ni nini wanachotaka kufanyia wanafunzi wetu wanaposema shule zisiorodheshwe. Juzi hatukupata hiyo orodha. Nini kimetokea? Orodha ziko. Hata katika kaunti yangu najua zile shule ambazo zimefanya vyema na zile ambazo hazikufanya vema. Nimejua upungufu uko wapi. Tunajua ni wapi tunatelezea. Hii ni kwa sababu ...
view
12 Feb 2015 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika, naomba nichukue nafasi hii nichangie Mswada huu, ambao umeletwa Bungeni kuhusu Mkaguzi Mkuu. Niko na mambo matano au sita ambayo ningeomba niyaangazie ili tupate mwelekeo unaofaa kuhusu Mswada huu, ambao umeletwa Bungeni. Kitu cha kwanza ni uhuru wa Mkaguzi Mkuu. Mkaguzi Mkuu ambaye anahusika na ukaguzi wa vitabu vyote, au hesabu zote za Serikali pamoja na mashirika ya Serikali, anahitaji kuwa na uhuru wa kuajiri wafanyikazi wake. Tukiangalia kipengele kimoja Tume ya Uajiri wa Umma, kwa kimombo “Public Service Commission” ndio inatakiwa kuajiri wafanyi kazi wa Mkaguzi Mkuu.
view