Before joining politics, Zainab was the Coast Province treasurer for Maendeleo ya Wanawake Organisation (MYWO) for more than two decades. At one point, she also served as the chairperson, MYWO Kwale District. International women politicians like Margaret Thatcher, Hillary Clinton and Sirleaf Johnson inspired her to join politics. She is a widow and in seeking elective office, had to overcome many negative cultural beliefs regarding women in leadership.
25 Mar 2015 in National Assembly:
Shukrani sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kwanza naomba kumpongeza Mheshimiwa Joyce, kwa sababu ya hii Hoja aliyoileta. Kusema ukweli, shida tuliyonayo Kenya ni kuwa sheria tukonazo nyingi lakini utekelezaji ndio shida. Ikiwa tuliweza kukipitisha Kiswahili kiwe lugha ya Taifa tangu enzi za Raisi aliyestaafu Mheshimiwa Moi na mpaka leo hakijatiliwa maanani, tungependa tujiulize: Shida iko wapi? Pia tuangalie jinsi ambavyo tunaweza kuirekebisha shida hiyo ili Kiswahili kiweze kutumika hata kwenye chupa za dawa. Maelezo yawe yameandikwa kwa Kiswahili ndio yule mama kijijini asiweze kumpatia mtoto wake dawa kipimo cha zaidi. Ninaunga mkono Hoja hii kwa sababu mengi tunayoyazungumza hapa ...
view
25 Feb 2015 in National Assembly:
Shukrani sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia Hoja hii ambayo imeletwa na Mheshimiwa mwenzetu. Ninampongeza mheshimiwa kwa kuwa hii ni Hoja muhimu kwa maisha ya Mkenya. Ningependa kumpongeza kwa kuwa ametambua kwamba ni wachache wametambulika katika kufidiwa na wakoloni. Kwa kweli, upiganiaji wa Uhuru haukuwa katika sehemu moja ya Kenya hii; ulikuwa katika kila pembe za nchi hii. Kwa sababu ya hali ya umaskini uliowakabidhi watu wetu katika maeneo mengine, mpaka sasa, hawajaweza kwenda kortini ili kutetea haki zao. Ni wajibu wa Serikali kusimama kidete kuwatetea Wakenya. Ninamshukuru mheshimiwa kwa kuwa ameweza kuyataja ...
view
25 Feb 2015 in National Assembly:
. Kuna Mzee Munyambu Mbaa Kivanguli, kutoka Ukambani, ambako ndiko kwenye usuli wangu kwa upande wa babangu. Kuna Mzee Mwamgogo, Mzee Jerumani na Mama Mekatilili, ambaye alitoka sehemu za Ugiriama. Hao ni miongoni mwa wale ambao waliweza kututetea. Wako wengine wengi ambao hatuwajui. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
25 Feb 2015 in National Assembly:
Ni wajibu wetu sisi kama Waheshimiwa kwenda mashinani na kuleta rekodi kamili kwa maana kila mmoja wetu anamjua ni nani aliyeweza kusimama kidete katika sehemu yake ya uwakilishi na kutetea haki za Wakenya. Baadaye, tunapaswa kuwa na kamati maalumu ambayo itaisukuma Serikali yetu ili iweze kuwatetea watu wetu ili waweze kupata haki yao. Hata kama watu hao wameshakufa, wameacha watoto na wajukuu. Hatutakwenda tukamfukue mtu ndiyo aje aseme kwamba aliteswa, lakini tunawajua wale ambao waliteseka. Kwa hivyo, ni wajibu wetu, kama Waheshimiwa, kuchukua rekodi na kusimama imara kuwatetea hao ndugu zetu. Kutambuliwa tu kama mashujaa, haijatosha. Baadhi yao hawatambuliwi kamwe ...
view
25 Feb 2015 in National Assembly:
Shukurani, Mhe. Spika. Nasimama kuunga mkono Ripoti ambayo imeletwa na Kamati hii ambayo inasimamia mambo ya jinsia. Ninawapongeza kwa kuwa Ripoti hii imetuonyesha waziwazi kuwa ni kweli kuna akina mama ambao wamepatiwa nafasi. Hata hivyo, kuna watu ambao hawako tayari kuwaona akina mama wakiongoza. Kwa sababu hiyo, kwa niaba ya akina mama wenzangu Kenya nzima, tunashukuru kwamba Kamati hii imemtoa mama huyu katika dhuluma ambayo alikuwa amepangiwa na wale wachache ambao hawataki kuona akina mama wakisonga mbele katika uongozi. Nawapongeza na naunga mkono Ripoti hii.
view
25 Feb 2015 in National Assembly:
Shukrani mhe. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono kwamba CDF ibaki. Ningetaka nikichangia hii Hoja nianze kwa kuwauliza waheshimiwa Wabunge wenzangu maswali. Swali la kwanza, je wanaotengeneza sheria ni akina nani? Wanaotengeneza sheria za Kenya ni sisi hapa na sisi ndio tulitengeneza sheria ya CDF, na hivyo basi CDF lazima ibaki. Kwa hali na mali, CDF ibaki. Hii ni kwa sababu magavana hivi sasa wanazunguka; unasikia wameenda kufungua miradi. Wangefungua nini kama ingekuwa si CDF? CDF imetuwekea mashule. CDF imetuwekea zahanati. CDF imetuwekea wadi za akina mama ambazo magavana wanaenda kufungua. Ingekuwa si CDF, wangefungua nini?Hii ni kwa sababu ...
view
25 Feb 2015 in National Assembly:
Pesa zao za bursary pia hatuelewi ziko wapi pesa za bursary ambazo zinatoka CDF wazazi wanazifurahia. Ninaomba CDF ibaki na tuiongeze zaidi na zaidi.
view
25 Feb 2015 in National Assembly:
Tusiongeze tu CDF bali pia na mfuko ambao tunauita “Social Fund” ambao utasimamiwa na wawakilishi wa wanawake. Zile pesa za magavana zikatwe na ziongezwe kwa hii Social Fund; tufanye kazi pamoja tuinue Kenya yetu.
view
25 Feb 2015 in National Assembly:
Kuna watu tunaweza kuwaita mabepari ambao bado wanataka kutuwekea ukoloni Kenya, na ni hao wanaoitwa World Bank. Wameona kwamba hatutaenda tena kukopa pesa kwa sababu CDF na Social Fund zinashikilia ile nafasi ambayo wao walikuwa wakishikilia. Hatutaki tena madeni. Sisi wenyewe tunaweza kujisimamia na tunajisimamia kupitia Social Fund na CDF. Wabunge wenzangu, katika bajeti ya mwaka huu, ikiwa hakuna CDF na Social Fund, there will be no Budget . There is will be no Budget for this country . Kwanza tupitishe yetu halafu tuangalie hayo mengine.
view
25 Feb 2015 in National Assembly:
Kwa hayo mengi, thank you very much .
view