Before joining politics, Zainab was the Coast Province treasurer for Maendeleo ya Wanawake Organisation (MYWO) for more than two decades. At one point, she also served as the chairperson, MYWO Kwale District. International women politicians like Margaret Thatcher, Hillary Clinton and Sirleaf Johnson inspired her to join politics. She is a widow and in seeking elective office, had to overcome many negative cultural beliefs regarding women in leadership.
10 Feb 2015 in National Assembly:
Thank you very much, hon. Speaker. Kwa niaba ya wananchi wa Kwale, ningependa kuchukua fursa hii nitoe rambirambi zangu na zao kwa familia ya marehemu Muchai, familia ya walinzi wake pamoja na familia ya dereva wake. Tukiwa tunaomboleza kifo cha mwenzetu, wakati umefika sisi kama Wakenya - nikisema sisi kama Wabunge tutakuwa tumejitenga, tungependa tujue. Tulimwona Rais wa nchi yetu akianzisha ule mradi wa kamera ambazo zinamulika mienendo yote katika eneo la Nairobi. Kamera hizi kweli zafanya kazi, ama wale ambao wanapaswa kuwa wanazisimamia walikuwa wamelala? Hii ni kwa sababu mahali ambapo aliuliwa mwenzetu ni katikati ya mji na katikati ...
view
10 Dec 2014 in National Assembly:
Asante sana, Madam. Spika. Nasimama kuunga mkono huu Mswada. Kwanza ninampongeza Mhe. mwenzetu kwa kutuletea huu mjadala ulio wa maana sana katika taifa hili letu, maana ni wa kuokoa maisha. Tukiwa tunachangia huu mjadala, ni lazima tuangalia na pia tujiulize hata hizi ajali zikitokea, kuna shida gani? Haswa ningezungumzia kuhusu ujenzi wetu wa barabara. Ukiangalia barabara zetu, hazina sehemu zimetengwa hususan kwa watu wanaotumia pikipiki. Ningeomba Wizara inayohusika, tunavyoendelea na ujenzi mpya wa barabara zetu au ukarabati, waweze kutilia maanani ili tuweze kuwa na sehemu ambazo waendeshaji boda boda wataweza kuzitumia. Naibu Spika wa Muda, kuna matuta mengi yaliyo katika ...
view
10 Dec 2014 in National Assembly:
hali hiyo, unakuta ajali zinatokea maana, mtu atakuja kwa kasi bila kujua kwamba, pale kuna tuta na mwishowe gari lake linatatisika ama kuvunjika. Katika huu ujenzi wa barabara, katika sehemu zetu za mashambani, utashangaa ya kwamba, upana wa barabara ni ule ule tangu wakati wa ukoloni ambapo, pengine ni gari moja tu lililokuwa linapita katika barabara hiyo. Barabara hiyo ni nyembamba sana. Wakati wa mvua, inakuwa mbaya zaidi maana, barabara yenyewe vile ilivyolimwa, ina mavumbi hapo katikati. Gari linapaswa kupita katikati ya ile barabara. Likitokea gari lingine ama pikipiki, kupishana ni vigumu. Mwisho unaingia ndani ya mtaro ama mgongane. Tunaomba ...
view
10 Dec 2014 in National Assembly:
Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, nilikuwa nikizungumzia waendeshaji boda boda. Ni jukumu letu kuhakikisha kwamba sheria za barabarani zinaheshimiwa. Mara nyinyi sisi wananchi tunatazama tu boda boda mmoja akibeba zaidi ya watu watatu, wanne ama watano. Ni kweli tunataka vijana wetu wapate pesa lakini polisi wa trafiki nao wanaangalia nini? Ajali inapotokea na watu kufariki, unakuta badala ya kufa mmoja, ingawa hatuombei wafe, watakufa sita na hiyo inatokana na uzembe uliyoko katika upande wetu wa trafiki.
view
10 Dec 2014 in National Assembly:
Kumalizia ninaomba kuunga mkono huu Mswada na yale yote tuliyoyazungumza hapa ama tuliyojadili yaweze kutiliwa maanani. Kwa wale ambao wanahusika pia waweze kuyasikia na kuyatilia maanani tuone vile ambavyo tunaweza kuokoa maisha ama pia kuokoa vijana wetu katika ajali zile ambazo zinaendelea katika barabara zetu. Naunga mkono huu mjadala. Thank you very much.
view
28 Oct 2014 in National Assembly:
Bi. Mwenyekiti, pia mimi ninasimama kuunga mkono. Liseni ya utafiti ni mojawapo ya njia ambazo zitaleta mapato. Ijapokuwa tutakuwa tukitegemea madini, pia tutapata mapato kutokana na kuuza leseni ambazo zitasimamia kazi kutoka mwanzo. Ninaunga mkono.
view
15 Oct 2014 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika, nachukua nafasi hii kwanza kukushukuru kwa kunipa nafasi hii niweze kuchangia mjadala huu. Mjadala huu, kusema ukweli, ni mjadala ambao unagusa roho ya uchumi kule nyanjani.
view
15 Oct 2014 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika wa Muda, vijana wa boda boda ni fungu ambalo tunaweza kusema linasaidia katika ajira mashinani lakini ni sehemu ya uchumi ambayo haijatiliwa maanani kuboreshwa. Ninampongeza Mheshimiwa kwa kuuleta huu mjadala na ningeomba badala ya Hoja hii, alete Mswada wa sheria ili tuweke sheria mwaafaka ambazo zitaweza kusimamia sekta hii. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
15 Oct 2014 in National Assembly:
Kama walivyozungumza wenzangu, vijana wa boda boda wana mengi ambayo wanastahili kufanyiwa. Utapata Waheshimiwa mara nyingi ndio ambao wamesimamia yale matatizo ambayo yanawakumba hao vijana; kwamba mtu akiumia na ile pikipiki, Mheshimiwa ndiye anampeleka hospitali. Kama ni leseni, ni Mheshimiwa anashughulikia. Lakini kuna njia ambazo Serikali kupitia kwa hili Bunge inaweza kuboresha biashara hii iwe ya manufaa zaidi. Kwanza, utakuta kwa mfano kama kule kwetu Kaunti ya Kwale, hao vijana kupata leseni ni lazima waende Mombasa. Ingekuwa bora ikiwa kupitia kwa wizara inayohusika na usafiri, kungekuwa na shule maalum ya kuwapatia watoto hao mafunzo. Wakimaliza mafunzo yao, wapewe vifaa viwili ...
view
15 Oct 2014 in National Assembly:
Tukiangazia usalama, pikipiki zinafaa kuwekewa kifaa aina ya “Track It”, kama magari kwa sababu baadhi ya pikipiki zinatumiwa na wahalifu. Juma lililopita kule kwetu Kwale, kuna mzee aliyeuawa na majambazi waliokuwa kwenye pikipiki. Hiyo siyo mara ya kwanza kisa kama hicho kutokea. Visa kama hivyo vimekuwa vikitokea mara kwa mara katika sehemu hiyo. Kukiwa na kifaa cha “Track It” kwenye pikipiki, itakuwa rahisi kujua pikipiki hiyo iko wapi, ni ya nani na ilikuwa na nani wakati uhalifu ulipotekelezwa. Mwendo wa pikipiki hiyo utafuatiliwa kupitia mahali maalum pa kuangalia pikipiki zinatembea katika sehemu gani.
view