Zainab Kalekye Chidzuga

Before joining politics, Zainab was the Coast Province treasurer for Maendeleo ya Wanawake Organisation (MYWO) for more than two decades. At one point, she also served as the chairperson, MYWO Kwale District. International women politicians like Margaret Thatcher, Hillary Clinton and Sirleaf Johnson inspired her to join politics. She is a widow and in seeking elective office, had to overcome many negative cultural beliefs regarding women in leadership.

All parliamentary appearances

Entries 111 to 120 of 180.

  • 15 Oct 2014 in National Assembly: Kama walivyosema wenzangu, inafaa tuwe na hazina itakayotengwa na Bunge hili ili vijana waweze kuwa na pesa zao. Pesa zilizotengewa vijana kupitia Uwezo Fund ni ndogo mno na hazitawafikia watu wote. Kukiwa na fedha maalumu zitakazoelekezwa upande wa matatu na pikipiki, hazitaweza kuchukuliwa na watu wengine isipokuwa washikadau kwenye sekta hizo. Watapewa mikopo nafuu itakayowawezesha kufaidika na kujisimamia. Wataweza kununua vipuri vyao ama kuwa na maduka ambayo yatakuwa yakiuza vipuri vyao badala ya kufanya safari ndefu. Kwa mfano, kule kwetu Kwale, kununua vipuri ni lazima mwenye pikipiki atoke aende Mombasa kutafuta vipuri vya pikipiki. Pia watakuwa wanaweza kujifundisha mambo ya ... view
  • 15 Oct 2014 in National Assembly: kuwa wa manufaa na kuinua uchumi wa nchi hii ama kwa kaunti zetu kwa jumla. Tutaweza kuondoa ule upungufu wa ajira miongoni mwa vijana wetu. Shukrani, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Naunga mkono Hoja hii. view
  • 15 Oct 2014 in National Assembly: Ahsante kwa kuniruhusu nichangie Hotuba ya Rais wetu, mhe Uhuru Kenyatta. Ningependa kumpongeza kwanza kwa sababu ametuonyesha mfano ambao tunastahili kufuata kama viongozi, kwamba sheria iko juu yetu sisi. Yeye alipojitoa mhanga kwenda Hague alikuwa anatuongoza kwa mfano bora. Ninampongeza kwa kitendo hicho. Rais alipomkabadhi msaidizi wake, mhe Ruto, mamlaka alikuwa anatuonyesha kwamba hana tamaa. Alituonyesha kwamba si lazima abaki kama Rais. Alituonyesha kwamba yuko tayari wakati wowote kutoa nafasi ili mtu mwingine ashike mamlaka. Hii ina maana kwamba hata baada ya wakati wake kuisha hatatuletea matatizo ya kulazimisha kubaki kwenye mamlaka; ataondoka kwenye kiti ili yule ambaye Wakenya watamchagua ... view
  • 15 Oct 2014 in National Assembly: tunatonesha vidonda. Badala ya vidonda kupoa kila kuchao tutakuwa tunavitonesha. La muhimu hapa ni kuwaita wale ambao waliathirika wazungumziwe na waweze kupatiwa kile kitawawezesha kuendelea na maisha ya kawaida kama ilivyokuwa wakati wa nyuma. Ninampongeza Rais. Akifuata mwenendo aliotuonyesha ni kweli Kenya itasonga mbele na tutadumisha amani yetu. Ahsanteni. view
  • 20 Aug 2014 in National Assembly: Ahsante sana Mhe. Naibu Spika. Kwanza, ningetaka kumkosoa Mwenyekiti wetu kwa kusema kwamba kamati ziko katika lokesheni; hakuna kamati ambazo ziko katika lokesheni, bali ni mtu mmoja ambaye anasimamia Wadi. Mwanakamati ni mmoja katika kila wadi. Kwa hivyo, hata hii kazi ni ngumu kwa hao wanakamati kwa sababu ni wachache. Pili, ni lazima tuweze kuelezwa ni vipi ambavyo wataweza kuwasaidia hao wanakamati kwa sababu wengine wanatoka sehemu ambazo ziko mbali sana na ile ofisi kuu ambayo inasimamia mambo ya hizi pesa. Inawabidi wao kutumia pesa zao za mfukoni kuzunguka. Hakuna gari la serikali ambalo linawasaidia hawa watu wanapokua wakizunguka nyanjani ... view
  • 6 Aug 2014 in National Assembly: Bwana Naibu Spika wa Muda nilikuwa nataka kuchangia lile suala la Lamu wala si hili. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 11 Jun 2014 in National Assembly: Shukrani sana. Nasimama kuunga mkono Mswada huu. Vile vile nampongeza Mbunge mwenzetu kwa kuleta hisia kama hizi ambazo zitaweza kukuza talanta ya wale wanaohusika na mambo ya kukanda mwili ili kuagua mifupa na mishipa ambayo ina shida. Kamati inayohusika na masuala ya afya yapaswa kujua kwamba kuna watu ambao wamezaliwa na kipawa cha ukandaji. Si kwamba wamekwenda shule kusomea hiyo taaluma lakini wanafanya kazi nzuri sana kule nyanjani. Kwa mfano, kuna wakunga ambao walichukuliwa na kuwekwa mahospitalini ili kusaidia akina mama waja wazito. Kuna watu vile vile ambao hawahusiki na mambo ya uzazi lakini wanahusika na mambo ya mifupa; wao ... view
  • 11 Jun 2014 in National Assembly: wachukuliwe na wapewe mafunzo zaidi ili waweze kusaidia jamii. Ni watu ambao wanaishi nasi katika jamii na wameweza kuokoa maisha licha ya kwamba hawajawahi kwenda shule. Lingine ni kwamba hili baraza linalonuiwa kuundwa, liwafikirie wale ambao hawakusomea hii taaluma shuleni ili nao wawakilishwe katika hilo baraza. Hii ni kwa sababu watu hawa wataleta maarifa wanayoyapata kule nyanjani. Wakenya wenzetu wanaosomea hii taaluma na kufanya kazi katika nchi za nje bado ni watu wetu. Tukifungua mlango ili waweze kurudi nyumbani na kufanya kazi humu nchini itakuwa ni bora kwetu. Tunapoteza pesa nyingi wakati hawa watu wanafanya kazi zao huko nchi za ... view
  • 11 Jun 2014 in National Assembly: Kwa hayo, ninamshukuru Mhe. Sang. Nina imani huu ndio mwanzo wetu sisi kama Bunge hili ili kuweza, kumwaangalia huyo mwanachi ambaye anaumia na hana uwezo wa pesa za kwenda kwa matibabu. Hii ni njia moja ambapo itaweza kuwasaidia watu wetu. Asanteni view
  • 3 Apr 2014 in National Assembly: Ahsante Mhe. Naibu Speaker. Langu ni pendekezo kwa Bodi ambayo inahusika na mikopo kwa wanafunzi. Hii ni kwa sababu tunaona, kwa mfano, katika sehemu ya Kwale, tunaweza kumaliza mihula kama miwili au mitatu na hakuna mtoto hata mmoja ambaye amepata mkopo huo. Hii ni keki ya Wakenya wote na inafaa igawanywe sawasawa ndiyo kila mahali watu wapate. Tungependa tujue ni mikakati ngani ambayo wameiweka ili kila sehemu ya nchi iweze kupata pesa hizo, ili watoto wetu waweze kusonga mbele na elimu. Hii ni kwa sababu vyuo vikuu vipo hata sehemu za nyanjani. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus