Zainab Kalekye Chidzuga

Before joining politics, Zainab was the Coast Province treasurer for Maendeleo ya Wanawake Organisation (MYWO) for more than two decades. At one point, she also served as the chairperson, MYWO Kwale District. International women politicians like Margaret Thatcher, Hillary Clinton and Sirleaf Johnson inspired her to join politics. She is a widow and in seeking elective office, had to overcome many negative cultural beliefs regarding women in leadership.

All parliamentary appearances

Entries 121 to 130 of 180.

  • 3 Apr 2014 in National Assembly: Jambo la Nidhamu, Bw Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuelewa kwa nini mwenzetu anawataja Waislamu. Inaonekana kwamba Waislamu ndio ambao wameleta haya maafaa. Hili jambo si la Waislamu kwa sababu katika dini ya Kiislamu hakuna mahali ambapo kuna mambo ya kuuana. view
  • 3 Apr 2014 in National Assembly: Ndivyo alivyosema. Amezungumzia Waislamu ama Muslims. view
  • 3 Apr 2014 in National Assembly: Amezungumzia Waislamu, Bw. Naibu Spika wa Muda. view
  • 5 Mar 2014 in National Assembly: Jambo la nidhamu, Bw. Naibu Spika wa Muda. Tangu tulipoingia, wanaoongea ni wanaume peke yake. Tunaomba wanawake nao waongee tafadhali. view
  • 19 Feb 2014 in National Assembly: Asante sana, Naibu Spika. Ninasimama kuunga mkono mjadala huu, na kumpongeza mhe. Sakaja. Ni matakwa ya Wakenya na sisi viongozi kuona kwamba vijana wetu na akina mama wamepata uwezo wa kujiendeleza kimaisha. Lakini, nikiunga mkono Mswada huu, kuna vikwazo ambavyo ni lazima tuvitilie maanani. Kwanza ni kuhusu kusajili kampuni ambako kunahitajika pesa nyingi sana. Tukiangalia, vijana na akina mama hawajaanza kufanya kazi, hizo pesa watatoa wapi? Naibu Spika, tumejitolea sisi viongozi tuwafanyie usajilishaji wa kampuni vijana na akina mama, lakini bado kuna vikwazo vingine. Kwa mfano, kwenye shirika letu la ujenzi; National Construction Authority, ukiaangalia kuna vikwazo vingi. Kuna malipo ... view
  • 19 Nov 2013 in National Assembly: Ahsante sana, Bw. Naibu Mwenyekiti wa Muda. Ninasimama kuunga Hoja hii mkono vile ilivyoletwa na mhe. Shukra. Naunga mkono kwa sababu tumetoa nafasi zote ambazo ni nyingi zinazosimamiwa na Wabunge wa maeneo ya uwakilishi Bungeni; tano ama zaidi ya tano, zitakuwa mikononi mwenu. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 19 Nov 2013 in National Assembly: Kwa hivyo, kuomba hii nafasi moja si kioja! Hii nafasi inapaswa kuwa itachukuliwa na mwakilishi wa wanawake na itakuwa ya mwanaume ama mwanamke kijana. view
  • 12 Nov 2013 in National Assembly: Ahsante, Bi. Mwenyekiti wa Muda. Nimesimama kupinga pendekezo la Mwenyeketi la kukifanyia mabadiliko Kipengele hiki. Mwanamke anapoolewa, huenda ikawa hana ajira lakini inafaa ifahamike kwamba kufagia nyumbani kwake asubuhi na kumchemshia mumewe maji ya kuoga pia ni mchango kwenye ndoa. Mwanamke huyo pia huchangia mengi kwenye ndoa. Kwa hivyo, ana haki ya kupata ugavi sawia wa mali yatakayopatikana wakati wa ndoa. view
  • 12 Nov 2013 in National Assembly: Ahsante, Bi. Naibu Spika wa Muda. view
  • 18 Sep 2013 in National Assembly: Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono Hoja hii kwa kugeuza kile kipengele kinachosema ya kwamba wafikiriwe wakulima kulipwa ama kulipwa ridhaa. Hiyo ni lazima walipwe kwasababu chakula ni muhimu katika maisha ya mwanadamu na tukiangalia ule umasikini ambao tuko nao huko chini mashambani, mwingi umetokana na chakula chetu kuliwa na wanyama wa pori. Na kumfanya huyu mkulima ajiskie kwamba naye Serikali imemfikiria na ili na yeye pia aweze kuwalinda wale wanyama, ni lazima naye aone faida kutokana na kulipwa chakula chake kile ambacho amejitahidi kulima katika shamba lake. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus