Zainab Kalekye Chidzuga

Before joining politics, Zainab was the Coast Province treasurer for Maendeleo ya Wanawake Organisation (MYWO) for more than two decades. At one point, she also served as the chairperson, MYWO Kwale District. International women politicians like Margaret Thatcher, Hillary Clinton and Sirleaf Johnson inspired her to join politics. She is a widow and in seeking elective office, had to overcome many negative cultural beliefs regarding women in leadership.

All parliamentary appearances

Entries 131 to 140 of 180.

  • 18 Sep 2013 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, pia katika kuongezea, mimi nikiwa mwanachama wa kamati ambayo inasimamia mambo haya ya wanyama pori pamoja na mazingira ni The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 18 Sep 2013 in National Assembly: kwamba tunakuja na Mswada ambao utaweza kuleta haya mambo kwa pamoja ili tuweze kuyajadiili kisawasawa katika Bunge na pia tuweze kupata maoni tofauti tofauti kwa wananchi. Ni lazima wananchi wetu waweze kufikiria kwasababu bila chakula tutakuwa kila siku sisi ni waombaji na hatutaki kuona Kenya yetu ikiwa siku zote inatafuta chakula kutoka nje. Sehemu nyingi katika nchi hii ni sehemu za kilimo lakini zimefanywa ziwe masikini ama wawe na njaa kwasababu ya mnyama wa pori ambaye anaendelea kula chakula chetu. view
  • 18 Sep 2013 in National Assembly: Kwa hivyo, tunaomba ijapokuwa Hoja hii imezungumzia tuu sehemu moja ya Mount Kenya, hili neno sio la Mt. Kenya peke yake bali ni neno ambalo litahusisha Kenya nzima popote pale palipo na mnyama wa pori ili mkulima aweze kulipa chakula chake. view
  • 18 Sep 2013 in National Assembly: Asante na naunga mkono mjadala huu kwa kupitia hicho kipengele kubadilishwa. Asante. view
  • 18 Sep 2013 in National Assembly: By mistake. view
  • 31 Jul 2013 in National Assembly: Mhe. Naibu Spika wa Muda, nachukua hii nafasi kumpongeza Mhe. Njenga kwa kuleta Hoja hii. Hoja hii imekuja kwa wakati unaofaa hasa tukiangalia kule mashinani kati ya vijana wetu. Kusema kweli, vijana wanastahili kutengewa pesa za kutosha katika Bajeti ya Kenya, kinyume na vile ilivyo leo kwa sababu kwanza, wao ni wengi na pili, mahitaji yao yamekuwa zaidi haswa kwa wale ambao wametoka mashule kabla ya kumaliza elimu kwa sababu ya ukosefu wa pesa. Wameshindwa kuendeleza masomo yao. Kwa hivyo, nafikiri hizo pesa zikitengwa, zitasiadia. Nawaomba Waheshimiwa wenzangu kuwa kila wanapozungumza, wale ambao wanashikilia constituencies, hujitaja wao peke yao na ... view
  • 9 Jul 2013 in National Assembly: Ahsante sana mhe. Naibu Spika. Naunga mkono Hoja hii kwa sababu kule kwetu Pwani tuko na msemo unaosema kwamba: “Mpanda ngazi hushuka”. Unapokuwa pale juu haufahamu kuwa siku moja utashuka. Kwa hivyo, ukiwa pale juu, waangalia walio chini na uwatendee haki. Tunaposema kwamba tunataka kupigana na ufisadi katika nchi hii, ufisadi huu tuuangalie kwa pande zote. Isiwe mfisadi aliye na cheo cha chini ndiye anayechukulia hatua lakini walio na vyeo vya juu wanawachwa. view
  • 9 Jul 2013 in National Assembly: Ikiwa kweli Serikali ya Jubilee imeamua kupambana na ufisadi, tunataka tuanze kuyaona hayo mapambano kuanzia waliokuwa na mamlaka. Waregeshe mali ya Wakenya. Wale waliokuwa na mamlaka watuonyeshe mfano mzuri kabla hawajapelekwa kortini kwa kujitokeza. Naomba kile kiboko ambacho Jubilee inatumia, ikitumie ili waliochukua pesa zetu na kuzipeleka katika nchi za nje, waadhibiwe. Goldenberg inafaa kufufuliwa upya ili haki itendeke kwa Wakenya. Tukifanya hivyo, hakuna mwingine atakayedhubutu kufanya ufisadi kwa sababu atakuwa anajua mkono wa sheria unafanya kazi. view
  • 9 Jul 2013 in National Assembly: Kenya imekuwa na uzoefu wa watu kuzungumzia ufisadi lakini hakuna hatua inayochukuliwa. Tume nyingi sana zimeundwa kwa kisingizio kwamba zitachunguza ufisadi na kuleta ripoti. Mwishowe, zile ripoti zinawekwa kwa makabati na Mkenya anaendelea kuwa maskini. Ndio mpaka leo tunashindwa kuwalipa walimu wetu. Pesa ziko lakini hatutaki kutenda haki. Naunga mkono Hoja hii ili tuisafishe nchi yetu, tuaminike hata katika ulimwengu wote kwamba Kenya iko tayari kuisafisha nyumba yake na tuweze kutimiza haki kwa watu wetu. view
  • 9 Jul 2013 in National Assembly: Naunga mkono. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus