Zainab Kalekye Chidzuga

Before joining politics, Zainab was the Coast Province treasurer for Maendeleo ya Wanawake Organisation (MYWO) for more than two decades. At one point, she also served as the chairperson, MYWO Kwale District. International women politicians like Margaret Thatcher, Hillary Clinton and Sirleaf Johnson inspired her to join politics. She is a widow and in seeking elective office, had to overcome many negative cultural beliefs regarding women in leadership.

All parliamentary appearances

Entries 151 to 160 of 180.

  • 12 Jun 2013 in National Assembly: kutekelezwa kulingana na Katiba ili kuwe na usawa. Kila mahali tunahitaji watu wa kutuhudumia. Sio kwamba upande mmoja waajiriwe na upande mwingine, wasiajiriwe. view
  • 12 Jun 2013 in National Assembly: Bi. Naibu Spika wa Muda, hao watu wanapoajiriwa, baada ya miezi sita, wanasema wanataka kurudi kwao. Wakiruhusiwa, ile sehemu inabakia bila watu wa kuhudumu. view
  • 12 Jun 2013 in National Assembly: Naunga mkono Hoja hii, lakini tuwe na usawa katika uajiri na uajiri ufanywe kule mashinani. Pia wale wanaosimamia wanasema kwamba lazima mhojiwa awe amehitimu na awe na ujuzi wa kazi hiyo wa miaka mitatu ama mitano. Ikiwa mtu hakuajiriwa hata siku moja, atatoa wapi ujuzi wa miaka hiyo mitatu au mitano? Maadamu hao watu walienda chuoni na wakasoma, ni vizuri waajiriwe ndio waweze kupata ujuzi. Waajiriwe katika mashinani, sio kuitwa Nairobi kuhojiwa. Wabunge hawana pesa na wanaambiwa wawakatie tikiti ya kusafiri kuja Nairobi ili waweze kuhojiwa na kuajiriwa. Tunaomba jambo hili litiliwe maanani. view
  • 12 Jun 2013 in National Assembly: Naunga mkono Hoja hii. Ahsante sana. view
  • 12 Jun 2013 in National Assembly: Ahsante sana Bi. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono Hoja hii kwa sababu ni moja kati ya zile nguzo ambazo zinasimamia taifa hili katika upande wa afya. view
  • 12 Jun 2013 in National Assembly: Kusema ukweli, tuna upungufu mkubwa sana katika nchi hii. Nikiongea hususan katika upande wa Pwani, kuna masikitiko makubwa sana wakati akina mama wanatembea zaidi ya kilomita ishirini kutafuta matibabu. Hata wakifika huko wanapata kwamba huduma ni duni kwa sababu hatuna wauguzi wa kutosha, maabara hayana wasimamizi wa kutosha na hata hakuna vifaa vya kutosha. Bi. Naibu Spika wa Muda, pia ningependa ieleweke vizuri sana kwamba ijapokuwa tunapigania hao watu waajiriwe ili tupata hiyo huduma, kuna upendeleo katika uajiri. Tarehe nne mwezi wa nne hadi tarehe kumi na sita, watu walikuwa wakisajiriwa ili waweze kupata ajira katika sekta ya afya. view
  • 12 Jun 2013 in National Assembly: Bi. Naibu Spika wa Muda, ni ajabu kwamba tuna majimbo lakini watu wanaitwa Nairobi kuja kuhojiwa. Kwa nini hiyo huduma haiwezi kufanyika katika makao makuu view
  • 4 Jun 2013 in National Assembly: Ahsante sana, Bi. Naibu Spika wa Muda. Hoja hii imekuja wakati unaofaa lakini ni lazima kwanza tuangalie chanzo cha matatizo haya. Alipokuwa Waziri wa Kilimo Makamu wa Rais William Ruto, wakulima katika eneo la Pwani walivuna chakula kingi mpaka wakakosa mahali pa kukihifadhi na kikaoza. Kuna shida katika Wizara ya Kilimo. Tunaomba Waziri wa Kilimo wa sasa aige mfano wa Mheshimiwa Ruto. Tunaomba asikae ndani ya ofisi bali aende mashambani akajionee na awasikize wananchi. Halmashauri ya nafaka nchini imejitwika majukumu yakuleta mbolea, ambayo si majukumu yake. Kama halmashauri hiyo imeshindwa kutuletea mbegu, italeta mbolea? Tumeipitisha Katiba ambayo imeanzisha serikali za ... view
  • 4 Jun 2013 in National Assembly: Mamlaka ya kununua mbegu yatakapopewa kaunti na taasisi iliyopendekezwa kuundwa, bodi ndogo katika kaunti zitapatiwa hayo mamlaka na tutaweza kupata mbegu na mbolea kwa wakati unaofaa. Wakati huo itakuwa rahasi kuwatambua wale ambao watakuwa wanazembea katika kazi zao, kinyume na hali ilivyo sasa, ambapo uzembe uko katika Serikali Kuu. Wakenya wanalia kwa sababu mbegu na mbolea haziwafikii kwa wakati unaofaa. Ninakumbuka kwamba katika miaka ya 90, kule kwetu Pwani kuliletwa mbegu iliyoitwa “Coast Composite”. Mbegu hiyo ilizaa ajabu lakini kulipoonekana kwamba Wapwani walianza kupata chakula, mbegu hiyo iliangamizwa. Sasa tunaletewa mbegu ndani ya mifuko. Tunaambiwa ndiyo mbegu inayofaa lakini tukipanda ... view
  • 4 Jun 2013 in National Assembly: Ahsante sana, Bi. Naibu Spika wa Muda. Hoja hii imekuja wakati unaofaa lakini ni lazima kwanza tuangalie chanzo cha matatizo haya. Alipokuwa Waziri wa Kilimo Makamu wa Rais William Ruto, wakulima katika eneo la Pwani walivuna chakula kingi mpaka wakakosa mahali pa kukihifadhi na kikaoza. Kuna shida katika Wizara ya Kilimo. Tunaomba Waziri wa Kilimo wa sasa aige mfano wa Mheshimiwa Ruto. Tunaomba asikae ndani ya ofisi bali aende mashambani akajionee na awasikize wananchi. Halmashauri ya nafaka nchini imejitweka majukumu yakuleta mbolea, ambayo si majukumu yake. Kama halmashauri hiyo imeshindwa kutuletea mbegu, italeta mbolea? Tumeipitisha Katiba ambayo imeanzisha serikali za ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus