Zainab Kalekye Chidzuga

Before joining politics, Zainab was the Coast Province treasurer for Maendeleo ya Wanawake Organisation (MYWO) for more than two decades. At one point, she also served as the chairperson, MYWO Kwale District. International women politicians like Margaret Thatcher, Hillary Clinton and Sirleaf Johnson inspired her to join politics. She is a widow and in seeking elective office, had to overcome many negative cultural beliefs regarding women in leadership.

All parliamentary appearances

Entries 141 to 150 of 180.

  • 2 Jul 2013 in National Assembly: Ahsante sana, mhe. Naibu Spika wa Muda. Nina matatizo kidogo; ni kama nimepoteza kadi yangu na haijulikani iko wapi. Nasimama kuunga mkono Hoja hii kwa sababu ina maana kwa Wakenya. Lakini mbona tunangoja mpaka wakati matatizo yanatokea ndio watu waende mbio? Mambo ya mafuriko yamekuwa ni kama kitega uchumi kwa wengine. Wakati mafuriko yanatokea, utaona bajeti kubwa kubwa zinazinduliwa kutoka mahali ambapo hapaeleweki na hizo pesa zitatumika na watu hawaelewi zinatumika vipi. Hizo pesa zinazotumika wakati wa mafuriko hazingetumika kama tungekuwa na mipangilio ya maana. Hayo mafuriko hayangeweza kutusumbua tena katika Kenya hii. Mhe. Naibu Spika wa Muda, kuna sehemu ... view
  • 19 Jun 2013 in National Assembly: Ahsante sana Mhe Naibu Spika wa Muda. Naunga mkono Hoja hii kuhusu mtoto wa kike. Sisi tunaoishi katika sehemu kame sio kwamba tuliomba kuishi kule bali ni maumbile ya Mwenyezi Mungu. Serikali zilizopita zilitutenga ndio maana tumeamua kuwa na Hoja kama hii. Namuunga mkono Mhe. Dukicha kwa kuleta Hoja hii. Kwa kweli hakuna shule katika sehemu kame. Hata kama mtazungumzia CDF, tunafahamu kwamba imekuja juzi tu. Miaka ya nyuma shule hazikujengwa. Kuna sehemu za wafugaji wanaotafutia wanyama wao lishe. Wao hata hawana nafasi ya kusoma. Ndiposa tunaonelea kuwe na shule ambako watoto watalala na kusoma. Mimi nazungumzia watoto wote wa ... view
  • 12 Jun 2013 in National Assembly: Ahsante sana Mheshimiwa Spika. Nasimama kuunga mkono Hoja hii inayohusu vijana. Hii ni kwa sababu tukiweza kutimiza yale yaliyo katika hii Hoja tutakuwa tumewasaidia vijana wetu kwa vile wametufanyia kazi nzuri. Wakati wa kura za 2007 tuliambiwa kwamba vijana walifanya fujo. Tulirudi mashinani tukaongea nao. Wakati huu tulipiga kura na hapakutokea fujo yoyote. Hii itakuwa ni zawadi kubwa sana kwa watoto wetu. Hii Hoja itawarekebisha vijana kinyume na wanavyofikiria wengi. Wabunge wenzangu, huko Kwale vijana wangu walisema kwamba Wabunge wapewe pesa. Hii ni kwa sababu kila uchao vijana wako mlangoni. Asubuhi ukiamka unapata SMS zaidi ya 1000 kwenye simu, “Twataka ... view

  • 12 Jun 2013 in National Assembly: Naunga mkono Hoja hii kwa sababu itatatuwa tatizo kubwa tulilonalo humu nchini. Tumezungumza hapa kwamba vijana wengi wameingilia mambo ya mihadarati. Wakipewa pesa hizi wao wenyewe wana lugha zao. Wataongea wenyewe kwa wenyewe na watatua shida hii ya matumizi ya mihadarati. Naomba tutilie maanani wazo kuwa kijana akipewa chombo cha kujiendeleza kimaisha hatarudi tena mtaani kuvuta unga ama kupiga watu kabari. Atarudi shambani ama kwenye kufanya biashara. Baadaye tutakuwa na viongozi walio na nidhamu. Naunga mkono. view

  • 12 Jun 2013 in National Assembly: Ahsante sana Bi. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono Hoja hii kwa sababu ni moja kati ya zile nguzo ambazo zinasimamia taifa hili katika upande wa afya. view
  • 12 Jun 2013 in National Assembly: Kusema ukweli, tuna upungufu mkubwa sana katika nchi hii. Nikiongea hususan katika upande wa Pwani, kuna masikitiko makubwa sana wakati akina mama wanatembea zaidi ya kilomita ishirini kutafuta matibabu. Hata wakifika huko wanapata kwamba huduma ni duni kwa sababu hatuna wauguzi wa kutosha, maabara hayana wasimamizi wa kutosha na hata hakuna vifaa vya kutosha. Bi. Naibu Spika wa Muda, pia ningependa ieleweke vizuri sana kwamba ijapokuwa tunapigania hao watu waajiriwe ili tupata hiyo huduma, kuna upendeleo katika uajiri. Tarehe nne mwezi wa nne hadi tarehe kumi na sita, watu walikuwa wakisajiriwa ili waweze kupata ajira katika sekta ya afya. view
  • 12 Jun 2013 in National Assembly: Bi. Naibu Spika wa Muda, ni ajabu kwamba tuna majimbo lakini watu wanaitwa Nairobi kuja kuhojiwa. Kwa nini hiyo huduma haiwezi kufanyika katika makao makuu ya kaunti? Naomba hili jambo liangaliwe sana. Kwa mfano, katika eneo la Kwale, msichana mmoja tu aliitwa kwenda kuhojiwa, lakini hakuweza kuchukuliwa. Je, kuna usawa katika uajiri? Tunaomba kwamba katika upande wa uajiri, pia uangaliwe na uweze The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus