The fact that she received limited education doesn’t stop her from pursuing her dreams. As a victim of retrogressive culture, Leshoomo vows to help other girls to be educated to beat cultural norms that act as a hurdle. Maison’s political journey arose out of a gutsy choice she made to attend public meetings against her husband’s orders. The move opened the door for her to become a nominated councilor in 1992 a position she maintained for 10 years. She joined Maendeleo ya Wanawake in 1995 and rose to become the chairperson in Maralal District. In 2008, the Party of National Unity (PNU) nominated her to parliament. As a long serving member of the Samburu District Peace Committee, she has taken it upon herself to promote peace between the Samburu and the neighbouring communities.
1 Sep 2016 in National Assembly:
Mimi ningeomba watoe orodha ya zile kazi wamewapatia watu. Ikiwa Nanyuki, Laikipia na Isiolo wamefaidika, Samburu hatujui wameandika watu kazi gani. Hiyo ni kwa sababau kandarasi si kazi. Watu wanapewa kandarasi halafu wanaiita kazi ilhali hiyo ni kandarasi ya siku mbili au tatu. Kwa hivyo, hii sheria ikitengenezwa, iangaliwe zaidi ajali zinazowakumba watu wanaoishi pale. Sisi tunajua wameishi upande wa Samburu Mashariki kwa muda mrefu. Kwa hivyo,hiyo sheria iangaliwe vizuri na wananchi wale wanaishi huko, ijulikana kile wanafaidika nacho.
view
1 Sep 2016 in National Assembly:
Pia mahali pale wamepewa, ni muhimu waweke ua. Kwa sababau wasipofanya hivyo, inakuwa shida. Kila mtu anaingia. Watu wetu wameumia sana. Watu kadhaa wamekatwa mkono na wao hawajali. Kuna mzee mmoja wanasema haijulikani ni nini ilimkata, ilhali alikatwa na mashini yao. Kwa hivyo, tuna shida nyingi na ni muhimu iangaliwe wakati sheria hii inapitishwa. Hatutapinga njia ya sheria kupitishwa, lakini faida ya mwananchi aliye pale iangaliwe na ile njia wanatumia--- Wakipata watu watatu au wane, wanafikiri wanawakilisha hiyo jamii. Tungewaomba waongee na jamii kwa jumla. Kamati ya Ulinzi na Maswala ya Kimataifa ilitembea huko katika Bunge la Kumi. Ningeomba Mwenyekiti ...
view
1 Sep 2016 in National Assembly:
Naomba pia Mwenyekiti wa Kamati atembee huko ndipo aje alinganishe habari iliyopatikana wakati ule na sasa. Wakati mnaenda kukaa chini na hamuulizi wenye jamii hiyo na viongozi wao vile mambo yako pale, ni vigumu sana kuja tupitishe kitu kitakachodhuru watu The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
1 Sep 2016 in National Assembly:
wengine. Kwa hiyvo, yangu ni hayo. Sheria iangaliwe kwa njia ya kuwasaidia wananchi ambao wanaishi huko. Ahsante.
view
27 Jul 2016 in National Assembly:
Asante sana, Mhe Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nichangie Ombi hili la Mhe. Sara. Tatizo la mzozo kati ya wananchi na wanyama pori limeleta shida katika Kenya yote. Kule kwetu Samburu tunaishi na wanyama. Tunachunga mifugo yetu pamoja na wanyama wa pori. Inaonekana shida iliyoko ni wananchi wanauawa na wanyama pori kama vile ndovu na mamba. Hivi majuzi, mamba alivamia watoto. Inafaa Mwenyekiti wa Kamati ya Mazingira na Mali Asili atembee maeneo Bunge yaliyoathirika ili aelewe shida hii. Watu wanauawa na wanyama pori lakini hawalipwi fidia. Kila wakati, wanaambiwa wajaze makaratasi lakini hakuna malipo yoyote. Kuna masumbuko ...
view
26 Apr 2016 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Spika, kwa kunipatia nafasi hii pia niseme pole kwa familia ya Rais Mstaafu, Mwai Kibaki, na watoto wake. Kila Mkenya anajua kuwa niko hapa Bunge kwa sababu yake. Siku yake aliyowekewa na Mwenyezi Mungu imefika na tunasema pole. Pia, natoa pole kwa niaba ya Wasamburu wote. Alipofika Samburu, aliangalia na akajua kuwa kuna kiongozi na akanichagua kati ya Wasamburu. Hakuna mwanaume Msamburu aliyejua kuwa kuna kiongozi mwanamke Msamburu. Kwa hivyo, ile baraka alipea Wasamburu na kile ameonyesha Wasamburu ni kwamba mwanamke anaweza kuwa kiongozi. Hatutamsahau hata kama Mwenyezi Mungu amemchukua. Ni mama tutakayemkumbuka kwa yale ametufanyia. Nasema ...
view
21 Apr 2016 in National Assembly:
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Mswada huu unaohusu akina mama. Vile wenzangu wamezungumza ni kweli. Akina mama ndio wanaofanya kazi yote. Kila kazi katika pembe zote za Kenya zinahusu akina mama. Naunga mkono Mswada huu ambao umeletwa Bungeni. Uwezo wa kuwa kiongozi unatoka kwa Mungu. Hatujui ni kwa nini kina mama wanakatazwa kuwa viongozi. Katika Jimbo la Samburu, mama alikuwa amewekwa nyumbani kuchunga nyumba na kufanya kazi zote za nyumbani. Kenya nzima, kuna wazee ambao wanajijengea nyumba. Kwetu mama huwa anajijengea nyumba. Kama huna nyumba, bwana hataishi nawe. Lazima ujenge nyumba hiyo ...
view
21 Apr 2016 in National Assembly:
Nashukuru kwa sababu akina mama katika Jimbo la Samburu wamejitokeza kuwa viongozi. Nashukuru pia kuwa katika sheria zetu kuna kipengele cha uteuzi. Kipengele hicho kinawafungua akili akina mama. Nilikuwa diwani mteule, kisha nikawa Mbunge mteule, mwishowe nikapigania kiti cha ubunge. Kama ningetaka kiti cha gavana wa Samburu au Seneta wa Samburu ningekichukua. Kwa nini nasema hivyo? Hakuna mmoja wao alifikia zile kura nilipewa. Kama ningetaka kiti chochote ningekipata. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
21 Apr 2016 in National Assembly:
Akina mama wanatusiwa kwa wingi wanapopigania viti. Wengi wanashtuliwa na matusi hayo. Ningependa kuwaambia akina mama katika Kenya hii kuwa wasijali matusi hayo. Wapiganie haki ya watu wao. Lazima upiganie haki yako na wenzako. Usishtuliwe na matusi. Wakati huu katika Jimbo la Samburu, Seneta Naisula anapigania kiti cha ubunge cha Samburu West. Nina uhakika kuwa atapata kiti hicho kwa sababu yale matusi anayopata wakati huu si madogo. Matusi ambayo napata wakati huu yanainua gredi zangu zote kwa sababu ya kazi ninafanya.
view
21 Apr 2016 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika wa Muda, tunaunga mkono. Nashukuru Wabunge wetu wote na wanaume wale wako hapa kwa kuunga mkono huu Mswada kwa sababu kazi inahitaji kusaidiana. Hakuna mwanamume hapa hamwambii mkewe aangalie kama anapigwa. Anamwambia atembee amutafutie kura akijua anaweza.
view