The fact that she received limited education doesn’t stop her from pursuing her dreams. As a victim of retrogressive culture, Leshoomo vows to help other girls to be educated to beat cultural norms that act as a hurdle. Maison’s political journey arose out of a gutsy choice she made to attend public meetings against her husband’s orders. The move opened the door for her to become a nominated councilor in 1992 a position she maintained for 10 years. She joined Maendeleo ya Wanawake in 1995 and rose to become the chairperson in Maralal District. In 2008, the Party of National Unity (PNU) nominated her to parliament. As a long serving member of the Samburu District Peace Committee, she has taken it upon herself to promote peace between the Samburu and the neighbouring communities.
1 Feb 2017 in National Assembly:
Asante sana Mhe. Naibu Spika kwa kunipa hii nafasi nichangie Hoja hii inayohusu vitambulisho na kadi za kura. Sisi kama viongozi inatubidi kuhakikisha kuwa Wakenya wote wamepata vitambulisho na kadi za kura. Lakini jinsi mambo yanavyoendelea katika nchi yetu si sawa. Mimi ninatoka jamii ya wafugaji. Watu wetu wote ambao wanavyo The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
1 Feb 2017 in National Assembly:
vitambulisho na wale ambao hawana, wametapakaa kila mahali kwa sababu ya kupeleka ng’ombe malishoni. Ombi langu ni kuwa muda huu uliotengewa hii shughuli ya uandikishaji kura ni mdogo. Wakenya wangeongezwa muda zaidi ili wapate vitambulisho na kadi za kura. Kuna shida nyingi katika kaunti za wafugaji. Wafugaji hawana vitambulisho ijapokuwa wametuma maombi ya kutaka kupata vitambulisho. Basi, wale wanaohusika sharti wapeane vitambulisho kwa wananchi. Hii ni kwa sababu hata watoto ambao wamemaliza Kidato cha Nne hawajapata vitambulisho ilihali wamekwisha kujisajili. Cheti cha kusubiri kitambulisho hakiwezi kutumika katika kusajili kadi ya kura. Ni muhimu hivyo vitambulisho vitoke na tuwahamasishe wananchi wajisajili ...
view
19 Oct 2016 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie Hoja hii. Nashukuru Mhe. Nooru na hata mimi ni mmoja wa wanakamati wake. Kwa kweli kuna mambo ambayo tunashindwa kuelewa kwa sababu tunayazungumzia kila mwaka. Haya mambo yanahusu njaa, maji na wafugaji. Ningependa kusema kwamba ile shida tuko nayo kubwa sana kwenye kaunti zetu ni kuhusu wafugaji. Mambo ya njaa na kukosa maji yamezidi na hata shida kubwa ni kwamba wanyama wa pori wanang’ang’ania hayo maji kidogo na wananchi.
view
19 Oct 2016 in National Assembly:
Katika Kaunti yangu ya Samburu tumepoteza watu kadhaa kwa sababu ya ndovu ambao wanang’ang’ania maji na tumeshindwa kutatua hilo jambo. Hii ni kwa sababu kaunti zimepewa pesa na ukiangalia sehemu zingine haziangalii shida za watu wao. Katika Samburu Kaunti, miaka nenda miaka rudi, shida ni njaa na maji. Saa hii watoto wamefunga shule mapema kwa sababu ya maji. Kama leo nimejitolea kuwachotea wafugaji maji, ningependa kuuliza: Shida iko wapi kwa sababu kaunti ziko na pesa? Pia tunaomba Serikali yetu kuu iweze kuangalia hizo pesa ambazo zinatumwa kwa kaunti zinatumika kwa njia gani.
view
1 Sep 2016 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Tukiwa hapa na tunapofinya mashini hizi, ni vizuri uangalie kila upande kwa sababu ni vibaya kwa Mwakilishi wa Kaunti ama wa Eneo la Bunge kusikiliza mambo yake yakizungumzwa na wengine na yeye ako hapa. Kwa hivyo, nashukuru kwa hii nafasi uliyonipanitia kuzungumzia kuhusu Hoja hii ya Waingereza. Kila eneo liko na mipango yake na shida zake kuhusu Hoja hii. Mimi nitazungumzia Kaunti ya Samburu.
view
1 Sep 2016 in National Assembly:
Ahsante. Kaunti ya Samburu imekuwa na shida nyingi kuhusu Waingereza. Tumeona nyingi zimetatuliwa lakini wakati sheria inatengenezwa, ni muhimu tusikilizwe.
view
1 Sep 2016 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika wa Muda, ungenisaidia kwa sababu naona kama mashauriano yamekuwa mengi.
view
1 Sep 2016 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Wakati sheria ya Kenya kushirikiana na nchi nyingine inatengenezwa, ni muhimu kwa shida zinazoletwa na nchi nyingine kuangaliwa. Ni muhimu pia tuangalie sheria ambazo zitawachunga wananchi wa Kenya. Kaunti ya Samburu, na hasa Samburu Mashariki, imekuwa na shida nyingi. Waingereza wameishi huko kwa muda. Kadri wanavyoishi huko, ndivyo tunavyozidi kupoteza maisha ya binadamu. Watu wengi wamepoteza maisha yao kwa sababu ya jinsi Waingereza hao The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
1 Sep 2016 in National Assembly:
wanavyotumia silaha zao. Wanapoenda kwa mafunzo, wanawacha silaha zao nje. Wanatupa mabomu, risasi na kila aina ya silaha. Mnajua maeneo yetu ni ya wafugaji. Ng’ombe zinatembea zikitafuta nyasi na watoto wanazichunga. Watu wengi wamepoteza maisha yao. Hilo ni jambo moja linalopaswa kuangaliwa. Jambo la pili ni hili: Tangu wakuje huko, hatujapata faida kutoka kwao kama vile msaada wa maji kwa mashule. Bado tuna shida ya maji na barabara. Hata wakitengeneza barabara, wanapitisha tinga tinga mara moja na baadaye inaonekana ni kama haikutengenezwa. Wanadanganya wananchi kwamba wataleta maji, watatengeneza barabara na kuleta hospitali, lakini bado hatujaona wakifanya kitu.
view
1 Sep 2016 in National Assembly:
Ikiwa hii sheria itatiwa sahihi, waende watutengenezee kitu kile kitadumu wala si kuwadanganya wananchi. Wakituwekea hospitali, barabara au kisima cha maji, itasaidia kila mtu kwa sababu wanadanganya wananchi. Wakati wanalipa malipo ya wale watu wameaga, hawaangalii wale wanyama ambao wameumizwa na hayo mabomu. Wakati ng’ombe na mbuzi wanakufa kwa sababu ya hayo bomu, hawachukulii maanani. Kwa hiyvo, ningependa sheria hii iangalia vile vitu vinasaidia wananchi. Mahali pale wanafanyia mazoezi, kuna mahali ambapo walikuwa wamepewa na sasa wamesongeza mipaka had kwa mashamba ya jamii. Wakati wanaulizwa ni kwa nini wamesonga, hata hawajali mtu. Kwa sababu Mwenyekitu yuko hapa, ningependa waangalie wananchi. ...
view