Maison Leshoomo

Parties & Coalitions

Born

1962

Post

Parliament Buildings
Parliament Rd.
P.O Box 41842 – 00100
Nairobi, Kenya

Email

laikipiawest@parliament.go.ke

Telephone

0724958726

Maison Leshoomo

The fact that she received limited education doesn’t stop her from pursuing her dreams. As a victim of retrogressive culture, Leshoomo vows to help other girls to be educated to beat cultural norms that act as a hurdle. Maison’s political journey arose out of a gutsy choice she made to attend public meetings against her husband’s orders. The move opened the door for her to become a nominated councilor in 1992 a position she maintained for 10 years. She joined Maendeleo ya Wanawake in 1995 and rose to become the chairperson in Maralal District. In 2008, the Party of National Unity (PNU) nominated her to parliament. As a long serving member of the Samburu District Peace Committee, she has taken it upon herself to promote peace between the Samburu and the neighbouring communities.

All parliamentary appearances

Entries 61 to 70 of 314.

  • 28 Feb 2018 in National Assembly: Pia, tunaunga mkono mambo ya mahindi na Kahawa ambayo inategemea mvua. Tukiwa na maji mengi, hatutakuwa tukilia mvua haijanyesha kama kuna unyunyizaji wa maji kwa mimea yote. Naunga mkono Hoja hii. Tunataka kuhakikisha pesa zimetengwa kwa hiyo idara kwa sababu imebeba mambo mengi na inahitaji pesa ndio isonge. view
  • 28 Feb 2018 in National Assembly: Asante, Mhe. Naibu wa Spika. view
  • 6 Dec 2017 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Yangu pia nashukuru Mheshimiwa ambaye ameleta Hoja hii, kwa sababu kile tunapigania ni mambo ya misitu. Kwa ukweli… view
  • 6 Dec 2017 in National Assembly: Asante, Mhe. Spika wa Muda. Marekebisho ya pesa ni sawa. Inafaa pesa zitengwe za kuhusika na mambo ya misitu kwa sababu zinapitia vitengo vingi. Kama inawezekana, hizi pesa za misitu zingewekwa katika NG-CDF. Hiyo asilimia mbili katika NG- CDF ni kidogo sana kwa misitu. Misitu lazima tuzingatie. Hiyo misitu ndiyo inasaidia wafugaji kama sisi wenye ng’ombe na mbuzi. Hiyo misitu ikiisha, hata nyasi hatuwezi kupata. Kwa hivyo, NG-CDF ingeongezewa pesa zaidi ya hiyo asilimia mbili ili misitu isaidike. Pia, hatuelewi watu wa misitu wanachunga nini kwa sababu hao ndio wanamaliza misitu. Sio wananchi ambao wanamaliza misitu. Watu wa kuchunga misitu ... view
  • 29 Nov 2017 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii nichangie hii Hoja. Kabla sijachangia, nataka kutoa shukrani kwa Rais wetu kwa kuapishwa jana. Alifurahisha dunia yote kwa kuapishwa kwake. Hata sisi tumefurahi sana. Pia, natoa shukrani kwa Wakenya wote bila kujali vyama vya kisiasa. Wakenya wote walishuhudia kuapishwa kwa Rais wetu bila kujali kabila ama chama cha kisiasa. Wakenya wote walikuwa huko. Tunashukuru sana. Hiyo ni kujenga nchi yetu bila kufuata mambo ya siasa. view
  • 29 Nov 2017 in National Assembly: Pia, tunafurahi sana kwa sababu hatuna Kenya mbili, mbali ni hii moja. Kiti cha Rais ama Mbunge hakikaliwi na watu wawili. Ni mtu mmoja tu. Kwa hivyo, wote tunafurahi. Naambia wenzangu wote viongozi ya kwamba ni muhimu tushikane wote tuone kile kitu kitasaidia Wakenya. Ni kweli tumeona vile huyo mtoto amepigwa risasi. Kama mama na sisi kama viongozi tufikirie sana. Ukiangalia hayo mambo kwa runinga ni kama kuna watu wameanza kuvaa sare ya polisi. Ukiangalia hao polisi, unaweza kufikiria hawajapata mafunzo. Kwa hivyo, naomba Serikali iingilie kati hayo mambo ya sare za polisi kwa sababu watu wameanza kuzivaa. view
  • 29 Nov 2017 in National Assembly: Nikirudi kwa Hoja ya kutenga njia za gari za dharura, nakushuru kwa hii Hoja, kwa sababu tunafaa kuangalia kila barabara. Kwa ukweli, kuna culvert zingine ambazo zimetengenezwa kwa njia nzuri lakini kuna zile zinakaa kama milima. Hata ukiwa na mgonjwa, anaumia akirushwa kwa hizo culvert . Sisi ndio tunapitisha bajeti katika hili Bunge. Ningeomba pia tuangalie bajeti ya barabara, maji na hospitali ili tukipitisha wizara zipate pesa. Wakati mwingine pesa zinapitishwa na wizara hazipati hizo pesa. Ninatoka Samburu County ambayo ina shida kubwa sana. Mvua ikinyesha, barabara zote zinapasuka na watu hawawezi kwenda upande ule mwingine hata kwa hospitali na ... view
  • 29 Nov 2017 in National Assembly: Tukichangia mambo ya magari ya dharura, pia tuangalie mambo ya boda boda . Hapa Nairobi, nusu saa haipiti bila ya mtu wa boda boda kugongwa na gari kwa sababu hawana barabara za kupitia. Watu ambao wanasafiri kwa boda boda wanapita mbele ya magari. Inafaa tuangalie mahali boda boda zitapita kwa sababu watu wanaumia katikati ya magari. view
  • 29 Nov 2017 in National Assembly: Kwangu, tuna shida ya barabara. Ningependa kusema tuangalie sana katika wizara ambazo zina cartels ambazo zinapewa kazi ya kutengeneza barabara. Mtu anaweza kuchukua kampuni yake hapa, ipitishwe na apewe kazi ya kujenga barabara. Ningependekeza waanze kuzungumza na viongozi wa eneo Bunge wakati wanapeana hizo kandarasi ili wajue ni barabara gani zinatengenezwa na kwa namna gani. Unakuta kandarasi imepeanwa Nairobi na mtu anaenda Samburu na kiongozi hajui. Kwa hivyo, inafaa viongozi wahusishwe kwa yale mambo yanafanywa ndiyo tushirikiane pamoja tuone yamefanywa kwa njia inayotakikana. Unakuta vitu vingine vinaenda kombo kwa sababu viongozi hawaelezwi. view
  • 29 Nov 2017 in National Assembly: Naunga mkono Hoja hii. Lazima tuangalie vitu vingine ili tusaidike. Naomba ndugu zangu wa National Super Alliance (NASA) tuwe pamoja. Tumechaguliwa ili tushirikiane pamoja kama viongozi. Tunafaa kushirikiana na kufanye kazi ya wananchi. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus