Maison Leshoomo

Parties & Coalitions

Born

1962

Post

Parliament Buildings
Parliament Rd.
P.O Box 41842 – 00100
Nairobi, Kenya

Email

laikipiawest@parliament.go.ke

Telephone

0724958726

Maison Leshoomo

The fact that she received limited education doesn’t stop her from pursuing her dreams. As a victim of retrogressive culture, Leshoomo vows to help other girls to be educated to beat cultural norms that act as a hurdle. Maison’s political journey arose out of a gutsy choice she made to attend public meetings against her husband’s orders. The move opened the door for her to become a nominated councilor in 1992 a position she maintained for 10 years. She joined Maendeleo ya Wanawake in 1995 and rose to become the chairperson in Maralal District. In 2008, the Party of National Unity (PNU) nominated her to parliament. As a long serving member of the Samburu District Peace Committee, she has taken it upon herself to promote peace between the Samburu and the neighbouring communities.

All parliamentary appearances

Entries 41 to 50 of 314.

  • 22 Aug 2018 in National Assembly: Ilikuwa ninaomba nafasi. view
  • 22 Aug 2018 in National Assembly: Asante sana, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Mimi pia ninaunga mkono Hoja hii. Nchini Kenya tuna shida ya huo ugonjwa unaoitwa nasur kwa lugha ya mama. Ninaunga mkono ili tupate madaktari mashinani. Mambo haya ni mabaya zaidi kule mashinani kwa sababu ya ukosefu wa hospitali na madaktari wa kuhudumia akina mama ambao wako na shida hiyo. Hii ni shida kubwa kila mahali, haswa miongoni mwa jamii za wafugaji. Inakuwa aibu kubwa mpaka unaona wasichana hawaendi shuleni. Tunapochunguza tunapata wako na hiyo shida. view
  • 22 Aug 2018 in National Assembly: Vile vile, akina mama wanapojifungua hujipata kwenye hali hii. Unapata mama amekiti, na mkojo unatoka. Unapojaribu kuuliza, unapata hakuna daktari ambaye anaelewa ni kitu gani kinaendelea. Kwa hivyo, mimi pia naunga mkono ili jambo hili liweze kuangaziwa kwa kina kwa sababu ni jambo linalowaumiza akina mama. Limenyamaziwa kwa muda mrefu. view
  • 22 Aug 2018 in National Assembly: Akina mama wengi wanaona aibu kusema wako na shida hiyo. Watu wanaogopa. Tunaomba tuwe na madaktari mashinani. Tunawashukuru madaktari ambao Serikali imewaleta kutoka nje. Tunaona sasa wanaelekea mashinani kwenda kutibu magonjwa tofauti. Ninaomba The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 22 Aug 2018 in National Assembly: huo pia uwe ugonjwa mojawapo wanaenda kuangalia na kushughulikia, hasa huu ugonjwa unaitwa saratani. Madaktari wanarudi mashinani kwenda kutibu magonjwa. Naunga mkono na kusema madaktari hawa wanaotembea mashinani pia waende na wajaribu kuuliza kina mama ile shida wanapata kwa sababu shida hii iko hasa kwa kina mama wanaojifungua mara ya kwanza. view
  • 22 Aug 2018 in National Assembly: Ninaunga mkono Hoja hii na ninamshukuru dadangu kwa kuileta na tutazingatia kuwaelimisha kina mama wetu na wasichana ili mtu akiwa na shida hiyo afike hospitalini kwa haraka ili shida yake ipate kujulikana na kutatuliwa mara moja. Asante na ninaunga mkono. view
  • 22 Aug 2018 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Naunga hii… view
  • 22 Aug 2018 in National Assembly: Mhe. Naibu Spika wa Muda, kawaida huwa tunapitisha majina yakiwa pamoja, sio moja moja vile Mhe. Mbadi amesema. Kwa hivyo, naunga tupitishe wote pamoja. view
  • 22 Aug 2018 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Naunga mkono Ripoti hii kuhusu IPOA kwa sababu tunaelewa hili ni shirika la kuchunguza maafisa wa polisi wakati wananyanyasa wananchi. Tumepata shida nyingi katika Kaunti ya Samburu mahali ninatoka kwa sababu ya shida ya polisi na wananchi. Tulipopeleka kesi kwa IPOA, ninaamini waliifanya hiyo kesi na kuthibitisha ni nini kilikuwa kimefanyika. Hiyo IPOA iliweka kila kitu wazi. Ninaunga mkono uteuzi wa hawa watu kwa shirika hili kwa sababu tumeona ile kazi linafanya katika Kenya yetu. Hii IPOA haina bajeti ya kufanyia kazi. Naomba kamati husika na Serikali waipe hela kwa sababu mambo mengi ... view
  • 22 Aug 2018 in National Assembly: sababu hana raha kwa kazi yake. Kwa hivyo, hili shirika likibuniwa vizuri, litasaidia maafisa wake kufanya kasi na inafaa kuchunguza pande zote. Wanafaa kuangalia maafisa wa polisi na yale makosa ambao wamefanya. Kuna pande mbili. Wananchi walioteuliwa kuingia katika shirika hili wameorodhesha akina mama. Uteuzi huu umeangalia maeneo kadhaa. Lazima uteuzi huu umeangalia karatasi zao na masomo yao. Wamesoma na hii inaonyeshwa na makaratasi yao. Badala ya kumwangalia mama ambaye anatajwa kwamba alikuwa kwa Independent Electoral and Boundaries Commission (IEBC), naomba tusiangalie mtu mmoja na hatujui alichofanya. Pengine kamati husika iliangalia vizuri na ikapitisha kwa njia inayotakikana. Naomba tuwapitishe wote ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus