Maison Leshoomo

Parties & Coalitions

Born

1962

Post

Parliament Buildings
Parliament Rd.
P.O Box 41842 – 00100
Nairobi, Kenya

Email

laikipiawest@parliament.go.ke

Telephone

0724958726

Maison Leshoomo

The fact that she received limited education doesn’t stop her from pursuing her dreams. As a victim of retrogressive culture, Leshoomo vows to help other girls to be educated to beat cultural norms that act as a hurdle. Maison’s political journey arose out of a gutsy choice she made to attend public meetings against her husband’s orders. The move opened the door for her to become a nominated councilor in 1992 a position she maintained for 10 years. She joined Maendeleo ya Wanawake in 1995 and rose to become the chairperson in Maralal District. In 2008, the Party of National Unity (PNU) nominated her to parliament. As a long serving member of the Samburu District Peace Committee, she has taken it upon herself to promote peace between the Samburu and the neighbouring communities.

All parliamentary appearances

Entries 51 to 60 of 314.

  • 15 Aug 2018 in National Assembly: Ilikuwa ninaomba nafasi. view
  • 15 Aug 2018 in National Assembly: Asante sana, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Mimi pia ninaunga mkono Hoja hii. Nchini Kenya tuna shida ya huo ugonjwa unaoitwa nasur kwa lugha ya mama. Ninaunga mkono ili tupate madaktari mashinani. Mambo haya ni mabaya zaidi kule mashinani kwa sababu ya ukosefu wa hospitali na madaktari wa kuhudumia akina mama ambao wako na shida hiyo. Hii ni shida kubwa kila mahali, haswa miongoni mwa jamii za wafugaji. Inakuwa aibu kubwa mpaka unaona wasichana hawaendi shuleni. Tunapochunguza tunapata wako na hiyo shida. view
  • 15 Aug 2018 in National Assembly: Vile vile, akina mama wanapojifungua hujipata kwenye hali hii. Unapata mama amekiti, na mkojo unatoka. Unapojaribu kuuliza, unapata hakuna daktari ambaye anaelewa ni kitu gani kinaendelea. Kwa hivyo, mimi pia naunga mkono ili jambo hili liweze kuangaziwa kwa kina kwa sababu ni jambo linalowaumiza akina mama. Limenyamaziwa kwa muda mrefu. view
  • 15 Aug 2018 in National Assembly: Akina mama wengi wanaona aibu kusema wako na shida hiyo. Watu wanaogopa. Tunaomba tuwe na madaktari mashinani. Tunawashukuru madaktari ambao Serikali imewaleta kutoka nje. Tunaona sasa wanaelekea mashinani kwenda kutibu magonjwa tofauti. Ninaomba The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 15 Aug 2018 in National Assembly: huo pia uwe ugonjwa mojawapo wanaenda kuangalia na kushughulikia, hasa huu ugonjwa unaitwa saratani. Madaktari wanarudi mashinani kwenda kutibu magonjwa. Naunga mkono na kusema madaktari hawa wanaotembea mashinani pia waende na wajaribu kuuliza kina mama ile shida wanapata kwa sababu shida hii iko hasa kwa kina mama wanaojifungua mara ya kwanza. view
  • 15 Aug 2018 in National Assembly: Ninaunga mkono Hoja hii na ninamshukuru dadangu kwa kuileta na tutazingatia kuwaelimisha kina mama wetu na wasichana ili mtu akiwa na shida hiyo afike hospitalini kwa haraka ili shida yake ipate kujulikana na kutatuliwa mara moja. Asante na ninaunga mkono. view
  • 13 Jun 2018 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda. Ninaunga mkono kitengo cha huduma ya vijana. Pesa hizi ni nyingi na zinasaidia watoto wetu. Tungepewa pesa hizi kama wawakilishi wa wanawake kwa sababu sisi pia ni sehemu ya Bajeti ya Serikali kuliko zile pesa zingine kidogo tungeongezewa. Wale vijana ambao wanaandikwa katika huduma ya vijana hawapati kazi baada ya kutoka huko. Hii pesa itasaidia vijana wakitoka NYS kuajiriwa kama polisi ili wafanye kazi kuliko kwenda mafundisho kisha wanabaki barabarani bila kazi. view
  • 28 Feb 2018 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu wa Spika. Mimi pia naunga mkono haya mambo ya kilimo. Tunaelewa vizuri sana kwamba Kilimo ndicho muhimu zaidi kwa wananchi wa Kenya. Ikiwa hatutatenga pesa za kutosha kwa idara ya kilimo, itakuwa ngumu kwa Wakenya kuendelea kupata mavuno yao. view
  • 28 Feb 2018 in National Assembly: Kuhusu Kamati ya Kilimo na Mifugo; kila wakati tukijaribu kutenga pesa kwa kilimo; mara kwa mara, unakuta pesa zinaenda pahali pengine. Naunga mkono Hoja hii nakusema ni muhimu tutenge pesa nyingi kwa sekta ya kilimo. Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi iko na idara nyingi. Wafugaji wanaumia sana. Pesa ikitengwa kwa mambo ya mifugo, sisi ndio tunaumia. Ukame na njaa zinamaliza wanyama. Maji inategemewa kwa mambo ya wanyama. Kwa hivyo, tunaumia kabisa kama wafugaji. Kama sasa, kila mtu anaona katika Kenya vile mifugo wanakufa kwa sababu ya ukosefu wa maji na nyasi. view
  • 28 Feb 2018 in National Assembly: Kuna hadithi moja ambayo hatuwezi kukubali. Kuna wakati tunatenga pesa nyingi sana ya nyasi na ya kununua chakula cha ng’ombe lakini hatuelewi zina kwenda wapi. Kwa hivyo, tunataka tutenge pesa nyingi ili zisaidie mifugo. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus