The fact that she received limited education doesn’t stop her from pursuing her dreams. As a victim of retrogressive culture, Leshoomo vows to help other girls to be educated to beat cultural norms that act as a hurdle. Maison’s political journey arose out of a gutsy choice she made to attend public meetings against her husband’s orders. The move opened the door for her to become a nominated councilor in 1992 a position she maintained for 10 years. She joined Maendeleo ya Wanawake in 1995 and rose to become the chairperson in Maralal District. In 2008, the Party of National Unity (PNU) nominated her to parliament. As a long serving member of the Samburu District Peace Committee, she has taken it upon herself to promote peace between the Samburu and the neighbouring communities.
29 Nov 2017 in National Assembly:
Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii.
view
7 Nov 2017 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kutoa shukrani kwa Mhe. Peris kwa kuleta Hoja hii. Mambo ya ng’ombe yamezungumziwa sana. Kama watu wangesikia, mambo haya hayangefika hapa. Kila mtu ameumwa na hayo mambo.
view
7 Nov 2017 in National Assembly:
Hii si mara ya kwanza kwa ng’ombe kupigwa risasi. Ukiona vile tumenyamaza sisi wengine, ni kwa sababu ya mshangao. Wale wamepiga ng’ombe risasi wajue wamebeba laana kubwa sana. Wakati ng’ombe anapigwa risasi na analia, ujue ataenda na mtu tu. Haendi peke yake.
view
7 Nov 2017 in National Assembly:
Kwa hivyo, tunaona hakuna haja ya kupiga kelele. Ningependa kuwaambia ndugu zangu ambao ni viongozi wa Laikipia kuwa ni lazima tukae chini na tujue haya mambo ya Laikipia yalianza namna gani. Hii si mara ya kwanza taabu imetokea Laikipia. Imetokea mara mingi na tukajaribu kuleta peace caravan na itapoa. Mambo ya kupiga ng’ombe risasi ilianza miaka mitatu iliyopita. Ukame huwa kila wakati na kila wakati tunaenda Laikipia kutafuta nyasi. Hatuendi kuchukua shamba ya wenyewe kwa nguvu, kuvunja ama kubeba vitu. Watu wanaenda kununua nyasi kwa wale ambao wako kwa mashamba. Mambo ya kuleta askari kupiga ng’ombe risasi ilianza miaka mitatu ...
view
7 Nov 2017 in National Assembly:
Kile hatuwezi kukubali pia ni kile IGP, Mr. Boinett, amesema kuwa watu wanaenda kushika ng’ombe na ndio wanapigwa risasi. Hatujawahi kumpata mtu ambaye ameenda kushika ng’ombe na akafa naye. Kuna shida ya ng’ombe mahali kwingi. Pia, maafisa wa Serikali ambao wako kule wako na shida nyingi. Kama wanasusia Serikali, wasisusie Serikali kwa kutumia Wasamburu. Wasusie Serikali kwa njia nyingine kwa sababu kuna mambo mengi pale. Kwa hivyo, dada zangu viongozi, kuna mambo mengi pale. Tushaajua na tushaakaa mara tatu na lazima turudi tukae chini tujue ni nini kinaendelea. Naomba viongozi wa Laikipia tusitie hili jambo moto sana isionekane kama kwamba ...
view
7 Nov 2017 in National Assembly:
Naomba sisi viongozi tujaribu kufuatilia kujua ni nini kilifanyika huko Laikipia. Wale ambao ng’ombe wao waliuliwa wako na shida nyingi sana. Kwa mfano, watoto wao hawawezi kwenda shule. Katiba yetu inawachunga wananchi na mali yao. Lakini sasa mali imeharibiwa na Wasamburu hawana shamba ya kwenda kuchuna majani. Ng’ombe wao ndio majani chai, sukari, mahindi na miraa. Kwa hivyo, ni lazima tujue ya kuwa ng’ombe ndio tegemeo la wafugaji. Ni ngómbe wametulea sisi mpaka tukawa hivi na bado wanatulea. Tutafute njia ya kisheria ya kutatua jambo hili. Naunga mkono kuundwa kwa kamati ya Bunge ya kuchunguza mambo yanayoendelea. Naomba Mbunge wa ...
view
15 Feb 2017 in National Assembly:
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika kwa kunipa nafasi hii kuzungumzia sheria hii kuhusu wanyama wetu. Kwa sababu wenzangu wameongea zaidi kuhusu mambo ya wafugaji wa mbuzi na ng’ombe, kwa kweli, hizo ndizo shida zinazowakumba wachungaji. Ni muhimu sana kuwe na sheria hii ili tupate bodi ya kuangalia mambo hayo. Mara kwa mara, wafugaji wanapata shida kwa sababu hawana namna nyingine. Wanategemea wanyama wao pekee. Hakuna sheria katika Kenya yetu ya kulinda wanyama wao. Ndio unaona shida zote za ukame, maji na zingine zinawakaba wanaochunga wanyama wetu. Ni ukweli tukipata hiyo bodi, tutakuwa na sheria ya kuchunga wanyama wetu. The electronic ...
view
15 Feb 2017 in National Assembly:
Sheria imewekwa kwa kila kitu kinachotengenezwa katika Kenya yetu. Kuna bodi ya sukari, bodi ya kahawa, bodi ya majani na bodi ya kila kitu. Tunaomba tuipitishe hii sheria kwa sababu itasaidia wafugaji wote katika Kenya nzima. Tumetembea na tukaona vile wafugaji wanachunga wanyama wao na vile sheria imewekwa. Tukipitisha hii sheria, itawasaidia wafugaji na wanyama wao. Sheria hii itatusaidia hasa katika wakati wa ukame kama huu. Mwenzangu amesema hajui mahali Kshs450 milioni zimeenda na hiyo pesa inaendelea kununua wanyama katika kila pembe ya Kenya ambayo imeathiriwa na ukame. Ningeomba pesa ipitishwe ili isaidie pande za wanyama yetu. Wafugaji wanaumia sana ...
view
15 Feb 2017 in National Assembly:
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika kwa kunipa nafasi hii. Naunga mkono.
view