The fact that she received limited education doesn’t stop her from pursuing her dreams. As a victim of retrogressive culture, Leshoomo vows to help other girls to be educated to beat cultural norms that act as a hurdle. Maison’s political journey arose out of a gutsy choice she made to attend public meetings against her husband’s orders. The move opened the door for her to become a nominated councilor in 1992 a position she maintained for 10 years. She joined Maendeleo ya Wanawake in 1995 and rose to become the chairperson in Maralal District. In 2008, the Party of National Unity (PNU) nominated her to parliament. As a long serving member of the Samburu District Peace Committee, she has taken it upon herself to promote peace between the Samburu and the neighbouring communities.
21 Apr 2016 in National Assembly:
Nina hakika kina mama tutapigania viti. Kama kwetu Kaunti ya Samburu hatukupata kiti cha kuchaguliwa cha waakilishi wa kaunti lakini kwa sababu ya kuteuliwa, tulipata kina mama kumi. Kwa hivyo, naunga mkono uteuzi ili usaidie wengine.
view
21 Apr 2016 in National Assembly:
Naunga mkono. Asante.
view
14 Apr 2016 in National Assembly:
On a point of order, Hon. Temporary Deputy Speaker.
view
14 Apr 2016 in National Assembly:
Naibu Spika wa Muda, unatumia mbinu gani kutupatia nafasi? Hii ni kwa sababu unaona mtu amekuja nyuma na anapata nafasi ya kuongea na wewe umekaa hapa kwa muda huo wote. Ni vizuri tuelewe unafuata mtindo gani.
view
14 Apr 2016 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Sisi tunaunga mkono Hotuba ya Rais na tunamshukuru sana kwa kuwa ameeleza Wakenya kuhusu ile kazi amefanya kwa hii miaka mitatu. Ile tu ningependa kuchangia pia ni kumshukuru kwa mambo ya barabara. Kama kaunti yangu ya Samburu, tunashukuru kwa sababu kutoka Rumuruti hadi Maralal tumeona barabara imeanza kutengenezwa. Katika miaka 50 tumekuwa tukililia hiyo barabara na sasa hivi inaendelea. Tunahimiza Serikali iweke nguvu kazi iende haraka kwa sababu kazi inaenda polepole . Tunamshukuru pia Rais kwa mambo ya hospitali na mashini za kaunti kwa sababu tunajua magonjwa mengi yanaenea katika kaunti bila hayo ...
view
14 Apr 2016 in National Assembly:
nchini. Tunashukuru kuwa masuala ya kutokuwa na usalama yamerudi chini na kuangaliwa. Sisi pia tunachangia katika Serikali yetu ya Jubilee. Rais anafuatilia sheria za Katiba ambayo wananchi walipitisha. Kile tunachukia ni vile wenzetu katika CORD walifanya wakati Rais wetu anafuatilia sheria za Katiba ya Kenya na kuja hapa kueleza wananchi kile kinatendeka nchini. Wenzetu walianza kupigia Rais firimbi. Tulichukulia mambo hayo kama mambo ya utoto. Viongozi hawatakiwi kufanya hivyo. Naomba wenzetu wafahamu kuwa sisi ni viongozi katika Bunge hii. Wananchi wametuchagua kuja hapa. Ikiwa wanaona kuwa kuna mambo Serikali ya Jubilee haifanyi, wangekaa chini na kusema nini hakifanyiki. Sio kuja ...
view
14 Apr 2016 in National Assembly:
Asante sana, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Hakuna haja ya kujibu swali hilo kwa sababu hivyo ndivyo Wakenya wote walichukulia tabia yao. Hakuna haja ya kujibishana. Tunamshukuru Rais kwa Hotuba yake. Tutampa mkono kwa njia yoyote ile inayotakikana.
view
23 Mar 2016 in National Assembly:
Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi kuunga mkono Hoja hii. Wenzangu wamezungumzia ugonjwa huu na kwa kweli, umeathiri watu wengi. Tunaomba Serikali iangalie njia zinazoweza kutumika kuzuia ugonjwa huo. Watu wengi nchini Kenya hawaelewi chanzo cha ugonjwa huo. Watu wengi wamekufa. Wakati watu wanaenda kutafuta matibabu, wanaambiwa kuwa hakuna njia ya kutibiwa kwa sababu ugonjwa umeenea sana. Kwa sasa, HIV/AIDS ni afadhali kwa sababu kumepatikana madawa ya kusaidia watu kwa muda mrefu. Ingefaa tuwe na njia ya kupima watu mapema ili waanze kutibiwa. Tumeleta watu wetu wengi Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta lakini mara nyingi, madaktari wanasema ...
view
23 Mar 2016 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika wa Muda, vile vile, kuna ugonjwa wa figo ambao pia umezidi. Unaathiri hata watoto wadogo wa miaka mitatu na mine. Unapata kwamba figo zote zimeathiriwa. Ningependa kushukuru dadangu Mhe. Wanga kwa kuleta Hoja hii. Magonjwa yamekuwa mengi sana. Kwa mfano, kuna ugonjwa wa figo, ugonjwa wa kisukari na ugonjwa wa shinikizo The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
23 Mar 2016 in National Assembly:
za damu. Tunafaa kufanya uchunguzi wa magonjwa haya kwa sababu labda yanatokana na vyakula ambavyo tunavila. Mwanzoni, hakukuwa na magonjwa kama haya. Lakini wakati huu, hata mtoto mdogo wa miaka sita, 10 na hata 15 anaweza kupatikana na ugonjwa wa moyo. Serikali inafaa kuchunguza magonjwa hao yanatokana na nini. Sisi ni wafugaji na siku hizi, tunaambiwa kule mahospitalini kuwa kuna magonjwa ya nyama na maziwa. Watu wamekuwa wakinywa maziwa kutoka zamani. Kwa hivyo, tuunge mkono Hoja hii ya saratani ili watu waanze kupimwa na kujua hali yao mapema. Zahanati pia zijengwe katika kila mahali ili watu wahudumiwe. Pia, naunga mkono ...
view