The fact that she received limited education doesn’t stop her from pursuing her dreams. As a victim of retrogressive culture, Leshoomo vows to help other girls to be educated to beat cultural norms that act as a hurdle. Maison’s political journey arose out of a gutsy choice she made to attend public meetings against her husband’s orders. The move opened the door for her to become a nominated councilor in 1992 a position she maintained for 10 years. She joined Maendeleo ya Wanawake in 1995 and rose to become the chairperson in Maralal District. In 2008, the Party of National Unity (PNU) nominated her to parliament. As a long serving member of the Samburu District Peace Committee, she has taken it upon herself to promote peace between the Samburu and the neighbouring communities.
1 Apr 2015 in National Assembly:
. Ningesema ni vyema ijulikane ni kwa nini shida inatokea katika pande hizo za wafugaji kila wakati. Kuna mambo ya ukame. Ingefaa tuliangalie jambo la ukame kwa sababu ukame uko kila mwaka. Tunategemea mvua ya Mwenyezi Mungu. Ingefaa pia hayo mambo ya ukame yaangaliwe kwa sababu watu wanaenda kuzunguka kutafuta nyasi. Wakati wananchi wanaenda kutafuta nyasi, jambo hili linaleta shida. Kwa hiyvo, ninaunga mkono. Tunaambia Rais asimame hivyo na aendelee hivyo. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
1 Apr 2015 in National Assembly:
Mambo ya ufisadi na wizi yanafaa yaangaliwe zaidi. Ningeomba na kusema ya kwamba tusiyachukue haya kuwa ni mambo ya ukabila. Kama una ufisadi ni afadhali uangaliwe zaidi. Isichukuliwe kama kuna wale wanadhulumiwa. Hakuna mtu anadhulumiwa. Kama mtu ni mfisadi lazima aangaliwe. Wakenya wote wanamuunga mkono Rais. Kwa vituo vya Huduma pia tunashukuru sana. Vituo vya Huduma vinaletea Wakenya manufaa kwa sababu huduma zote ziko karibu. Wale watu hawawezi kufika Nairobi watapata huduma yao karibu.
view
1 Apr 2015 in National Assembly:
Mambo ya ufisadi na wizi yanafaa yaangaliwe zaidi. Ningeomba na kusema ya kwamba tusiyachukue haya kuwa ni mambo ya ukabila. Kama una ufisadi ni afadhali uangaliwe zaidi. Isichukuliwe kama kuna wale wanadhulumiwa. Hakuna mtu anadhulumiwa. Kama mtu ni mfisadi lazima aangaliwe. Wakenya wote wanamuunga mkono Rais. Kwa vituo vya Huduma pia tunashukuru sana. Vituo vya Huduma vinaletea Wakenya manufaa kwa sababu huduma zote ziko karibu. Wale watu hawawezi kufika Nairobi watapata huduma yao karibu.
view
24 Mar 2015 in National Assembly:
Asante sana Naibu wa Spika kwa kunipatia hii nafasi ili name nichangie Hoja hii. Nashukuru mheshimiwa Musimba kwa kunipatia hii nafasi ijapokuwa napinga hii Hoja. Kwa ukweli sisi sote ni viongozi. Ni sisi tulimchagua huyu Spika. Sisi wenyewe inatupasa tujiheshimu kwanza kabla ya kwanza kumtaja Spika. Kufuatana na yale ambayo tumekuwa tukiona, sidhani tumeonyesha Wakenya heshima katika Bunge hili. Kile ambacho tumeonyesha ni kibaya. Tumejikosesha adabu sana. Tumeona wenzetu wakichukuwa chupa na kumwagia Naibu Spika maji usoni mwake. Kwa hivyo, sisi kama viongozi tujiheshimu kwa vile tumechaguliwa na wananchi ambao wanatuheshimu. Kuhusu hii Hoja, Mheshimiwa Musimba angechukua nafasi ya kukaa ...
view
25 Feb 2015 in National Assembly:
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii hata mimi nimshukuru Mhe. Wangamati kwa kuleta Hoja hii. Nafikiri tunazungumzia mambo ya wazungu wakoloni. Nafikiri kila mahali katika Kenya ilipata shida kwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
25 Feb 2015 in National Assembly:
sababu watu waliteswa. Mahali nimetoka kama Samburu, Wakenya wote wanajua wakati Jomo Kenyatta aliletwa huko kufungwa. Watu wanajua yale mateso Wasamburu walipata wakati huo. Ni mateso hata babu zetu wakituambia leo, tunatoa machozi hata kama hutukuona.
view
25 Feb 2015 in National Assembly:
Maajabu yalifanyika. Haikujulikana vile wananchi walifanyiwa wakati huo. Haswa ukienda Samburu, kuna mzee mmoja kwetu anaitwa Leaduma. Ukitaka kumpiga mwanamke au mtoto unamwambia: “Nitakupeleka mahali Leaduma alipelekwa.” Lakini hatujui Leaduma alipelekwa wapi. Kwa hivyo, wale wenzetu waliopigania Uhuru wa Kenya, nafikiri ni Wakenya wote. Hakuna pembe haikuteswa ama kuwa na waliopigania Uhuru na kuteswa. Tuna mzee mmoja, marehemu, alikuwa anaitwa Lekalja. Ndiye alimlisha marehemu Jomo Kenyatta katika Samburu. Wakati alikuwa anaenda kupeleka maziwa ama nyama yake, ile taabu alipata ilikuwa ni ya maajabu sana. Hadi sasa, familia ya Lekalja ama familia ya Leaduma tunavyosikia bado wanafuata historia ya baba zao ...
view
25 Feb 2015 in National Assembly:
Wakenya wengi au wazee waliopigania Uhuru wamekufa na familia zao bado wanafuatilia historia za familia zao. Serikali yetu ingeangalia hizo familia na kuona vile zitasaidiwa. Ama wakoloni – sisi tunawaita makaburu – wasaidie hizo familia . Ukiangalia mambo ya ardhi, kutoka kwetu hadi Laikipia, hao mabeberu bado wameisimamia. Bado hayo mashamba ni yao. Hata sasa tukitaka nyasi, hatupati. Ile taabu tunayo sasa ni kuwa wamechukua ardhi yote katika Laikipia. Hata nyasi hatupati. Bado wanawatesa watu wetu wakienda kutafuta nyasi. Bado wanawatesa watu wetu hata wakienda kutafuta maji kwa sababu wamechukua ardhi yote. Kwa hivyo, haya mambo ya
view
25 Feb 2015 in National Assembly:
yalikuwa ya Wakenya wote. Wote walipigania Uhuru wetu.
view
25 Feb 2015 in National Assembly:
Kwa hivyo, Serikali ingeangalia wale mabeberu wamebaki hapa - hata kama wanasema wao ni Wakenya - bado wanawaona Wakenya ni kama wako katika ukoloni. Hii ni kwa sababu tunaona watoto wetu wakipigwa wakipatikana wakifuga ng’ombe katika mashamba ya wazungu. Bado unapigwa, unateswa na unapigwa risasi. Hakuna kitu hatufanyiwi wa wale walibaki. Kwa hivyo, ningetaka kusema warudishwe kwao. Bado tuna uchungu sana. Yangu ni kusema tu tunaunga mkono na tunamshukuru Mhe. Wangamati kwa kuleta Hoja hii. Napendekeza kamati iundwe kutoka Bunge ili izunguke na kuyachukua majina ya familia ya wale waliopigania Uhuru. Pia, wale waliopigana katika Vita vya Pili vya Dunia, ...
view