Maison Leshoomo

Parties & Coalitions

Born

1962

Post

Parliament Buildings
Parliament Rd.
P.O Box 41842 – 00100
Nairobi, Kenya

Email

laikipiawest@parliament.go.ke

Telephone

0724958726

Maison Leshoomo

The fact that she received limited education doesn’t stop her from pursuing her dreams. As a victim of retrogressive culture, Leshoomo vows to help other girls to be educated to beat cultural norms that act as a hurdle. Maison’s political journey arose out of a gutsy choice she made to attend public meetings against her husband’s orders. The move opened the door for her to become a nominated councilor in 1992 a position she maintained for 10 years. She joined Maendeleo ya Wanawake in 1995 and rose to become the chairperson in Maralal District. In 2008, the Party of National Unity (PNU) nominated her to parliament. As a long serving member of the Samburu District Peace Committee, she has taken it upon herself to promote peace between the Samburu and the neighbouring communities.

All parliamentary appearances

Entries 151 to 160 of 314.

  • 25 Nov 2014 in National Assembly: Bwana Naibu Spika wa Muda, yangu ni kupeana pole kwa familia za wenzetu ambao waliuliwa kule Mandera. view
  • 25 Nov 2014 in National Assembly: Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Usalama si kitu cha kupigia kelele ama kuongea mengi. Tunafaa kungalia ni njia gani tunaweza kuwaokoa Wakenya. Tumesikia uchungu sana kuona vile wenzetu waliuliwa. Kuna kifo ambacho hakina uchungu, lakini wenzetu waliuliwa kwa uchungu sana. Tunafaa kujua ni The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 25 Nov 2014 in National Assembly: kitu gani kimefanyika ndio mambo kama hayo yatokee. Tunasikia kuwa wananchi walitolewa kwa basi na wakagawanya kati ya Wakristo na Waislamu. Ni lazima kuyaangalia mambo hayo. Kuongea na kusema ni nani atafutwa kazi au ni nani hatafutwa, ni lazima tuyaangalie kwa sababu si ukweli kuwa watu walipatikana na magaidi ghafla. Gaidi ni nani? Gaidi ni yule mtu ambaye tunakaa naye kwa nyumba. Ni lazima tuangalie hawa magaidi ni akina nani. Sisi wafugaji tunasema kuwa vijana wetu wanaenda kuiba, lakini inajulikana wakienda kupigana. Kwa nini haijulikani hawa magaidi wanatoka wapi na wanaenda wapi? Tungeomba kujua haya mambo yote kwa sababu kwa ... view
  • 23 Oct 2014 in National Assembly: Asante sana, Bi. Naibu Spika wa Muda. Ninaunga mkono Hoja hii kuhusu maji. Kama wenzangu walivyosema, maji ni uhai. Sijui ni sheria gani ambayo itatumiwa ili Wakenya wote wapate maji. Shida ya maji iko kila mahali. Ukipita popote katika Kenya, kuna shida ya maji. Shida hii ni kubwa katika jamii ya wafugaji. Mtu ambaye ameteseka katika Kenya hii ni mama mfugaji. Mpaka wakati huu, utakuta watu wanatembea kwa siku tatu kutafuta maji. Akina mama wanazunguka na punda wakitafuta maji. Hata hivyo, ni vigumu sana kutoa maji kwa shimo na watu wanne ndio wanaweza kutoa maji kutoka ndani ya shimo. Kaunti ... view
  • 23 Oct 2014 in National Assembly: maji wangekuza chakula chao. Kuna sehemu nyingine ambazo zina mchanga mzuri lakini hazina maji. Kwa hivyo, sheria, au njia yoyote, itafutwe kuhakikisha kuwa maji ya mvua yamezuiliwa kila mahali. Wakenya wote inafaa kupata maji. Wafugaji wakilia kuwa hawapati maji, watu wa Nairobi pia wanalia hawana maji. Ni kama hakuna mtu ambaye ana maji. Hapo mbeleni, tulikuwa tukisema kuwa Ukambani ndiko hakuna maji. Lakini sasa hivi, kila mtu anasema hana maji. Inafaa tutafute njia yoyote ile Wakenya wote wapate maji safi. Kwenye mabwawa ya kuzuilia maji ambayo bado yanatumika, unakuta maji yameharibika mpaka yamebadilika rangi, lakini watu bado wanayakunyua. Hawana njia ... view
  • 14 Oct 2014 in National Assembly: Mhe. Spika, naungana na wenzangu pia kuhusu Harambee. Kwa kweli, Harambee zinasaidia Wakenya ambao hawajiwezi. Hii ni kwa sababu sisi kina mama wa kaunti tunatumia mifuko yetu. Hatuna ndururu katika CDF ama pesa za kaunti; kwa hivyo, Harambee ziendelee ndipo kile kidogo tulicho nacho kisaidie wale ambao hawajiwezi. Tuna watoto mayatima; tuna watoto hawajiwezi; tuna watoto wanafukuzwa shuleni. Kwa hivyo, nimeungana na wenzangu kusema ni muhimu tuendelee na Harambee. Kwa kweli pesa ambazo zinatoka CDF kama bursary na za kaunti hazitoshi. Hospitali zina wagonjwa na hawana pa kuelekea na ni lazima wawe na Harambee. Tukifunga Harambee, hao wagonjwa watasaidikaje? Watoto ... view
  • 1 Jul 2014 in National Assembly: Asante sana, Bw. Spika. Ningependa kuuliza Mwenyekiti wa Kamati--- Kila mmoja wao anasema wiki mbili, wiki tatu au wiki nne. Hatuelewi kama hizi ni ripoti zinaletwa ama ni mchezo tu. Kwa sababu kila anayeamka anasema wiki mbili. Ukiangalia mambo kuhusu mashambulizi ya Lamu, Meru nakadhalika, pahali wananchi wanakufa na mali yao kuharibiwa wakati tunaka kujua ni nini kinafanyika, wenyeviti wanasema wiki mbili. Bw. Spika tusaidie tupate ukweli. view
  • 25 Jun 2014 in National Assembly: Ahsante, Mhe. Spika. Ningeomba tu kuwe na usawa kwa sababu inaonekana unalalia upande mmoja. view
  • 25 Jun 2014 in National Assembly: Ahsante, Mhe. Spika. Ningeomba tu kuwe na usawa kwa sababu inaonekana unalalia upande mmoja. view
  • 25 Jun 2014 in National Assembly: Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Tunaunga mkono Mswada huu ambao umeletwa na Mhe. Chachu kuhusu ukame. Hii si mara ya kwanza tunazungumza kuhusu mambo ya ukame. Jambo hili lilizungumzwa katika Bunge la Tisa na la Kumi na bado jawabu halikupatikana. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus