The fact that she received limited education doesn’t stop her from pursuing her dreams. As a victim of retrogressive culture, Leshoomo vows to help other girls to be educated to beat cultural norms that act as a hurdle. Maison’s political journey arose out of a gutsy choice she made to attend public meetings against her husband’s orders. The move opened the door for her to become a nominated councilor in 1992 a position she maintained for 10 years. She joined Maendeleo ya Wanawake in 1995 and rose to become the chairperson in Maralal District. In 2008, the Party of National Unity (PNU) nominated her to parliament. As a long serving member of the Samburu District Peace Committee, she has taken it upon herself to promote peace between the Samburu and the neighbouring communities.
25 Jun 2014 in National Assembly:
kwa bei ambayo inafaa kwa sababu wakati mwingine bei yao inashuka kwa sababu wafugaji hawana soko. Njaa ni mbaya na ni lazima tutafute namna tutasaidika.
view
26 Mar 2014 in National Assembly:
Asante sana, Naibu Spika. Ninaunga mkono wenzangu kuhusu hii Ripoti. Tungezungumzia kitu ambacho kinaweza kuwasaidia Wakenya kuliko kuongea kuhusu kitu ambacho hakiwezi kusaidia Mkenya. Naibu Spika, ningezungumza kuhusu usalama ambalo ni jambo tunaweza kulitafuta katika Kenya yetu kwa njia yoyote ile. Hii ni kwa sababu tumepoteza wananchi katika kila pembe ya nchi. Kile kinachonishangaza mimi Leshoomo ni mambo ya AlShabaab . Ni nani anitwa Al Shabaab na ana sura gani? Ninauliza swali hili kwa sababu
view
26 Mar 2014 in National Assembly:
hajulikani. Kama kuna wale wanafahamu Al Shabaab, ni vizuri wajitokeze watuambie sura ya AlShabaab ni hii ili Wakenya wajue. Mtu yeyote akibeba bunduki, anaitwa Al Shabaab . Ninasema hivyo kwa sababu nilikuwa katika kamati ya usalama katika Bunge la Kumi, watoto wetu walichukuliwa na kwenda kufunzwa--- Tulitoka hapa tukaelekea Voi na tukapata watoto zaidi ya 600 wanafunzwa pale. Siku hiyo walitoka watoto kama---
view
26 Mar 2014 in National Assembly:
Tafadhali nipe nafasi. Naibu Spika, nisaidie. Nafikiri ninaongea jambo muhimu na tuelewe ni kitu gani kinasumbua Kenya yetu. Tulienda na tukatoa watoto karibu 300 na wote ni Wakenya. Wote wako na vitambulisho vya Kenya na walikuwa wanafunzwa huko Voi. Kama ni hao ndio wamekuja kuwa Al Shabaab, ni muhimu tutafute njia ya kumaliza shida hii.
view
26 Mar 2014 in National Assembly:
Naibu Spika, kuhusu mambo ya Westgate ninashukuru hao watu waliofanya upelelezi. Walipeana Ripoti yao. Zaidi ya hayo, kila mtu hapa ni mupelelezi. Hata huyo ambaye anatembea bila viatu kwa barabara ana umuhimu. Wale watu ambao wanaitwa majasusi hawapati maneno kutoka mbinguni ama chini. Wanapata maneno kutoka wale masikini ambao wanatembea kwa barabara. Ni hao ndio wanapeana hizo ripoti. Tungesema kama viongozi kwamba tutachukua njia gani ndio hii ripoti ijulikane na ifanyike kwa njia inayotakikana?
view
26 Mar 2014 in National Assembly:
Nilisema mambo ya kaunti yangu ya Baragoi hapa. Watu arobaini walikufa. Waliuawa na Al Shabaab? Kwa hivyo nasema tutafute njia ya kumaliza usalama katika Kenya yetu. Tukiongea mambo ya usalama tusiiweke kama mashindano. Tujue tutamaliza namna gani hii mambo ya usalama ili tusipoteze Mkenya tena kwa sababu ya mtu mungine.
view
26 Mar 2014 in National Assembly:
Naibu Spika, yangu ni hayo na ningesema sisi viongozi tusiweke mambo ya usalama katika Kenya kama mashindano, siasa ama kichama. Tushikane tujue tutaimaliza namna gani kwa sababu tunaumia. Tusipendeze fulani lakini tutajaribu tuweke njia ya kusaidia Mkenya.
view
26 Mar 2014 in National Assembly:
Naunga mkono hii Ripoti na Kamati warudi waitengeneze. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
12 Nov 2013 in National Assembly:
Bi. Naibu wa Spika, kwa idhini ya Kipengele 44(2)(c) cha kanuni za Bunge, ningependa kuomba taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa Kamati ya Usalama kuhusu kuzorota kwa usalama katika eneo la Samburu. Wizi wa mifugo umezidi huko Samburu. Watu wameuawa kwa njia isiyoeleweka. Hali ya usalama imezorota huko Samburu kwa sababu ya wizi wa ng’ombe na hii imechangiwa na biashara haramu ya hao mifugo. Kwa mfano tarehe 26 Oktoba, 2013 ng’ombe 23 walipatikana wakiwa wamebebwa kwenye lori. Mifugo hao walikuwa wakienda kuuzwa. Suala hili lilihusisha maafisa wa usalama. Katika taarifa hiyo ningependa nielezwe yafuatayo:- (i) mpango gani Serikali iko nao ili ...
view
10 Oct 2013 in National Assembly:
Ahsante sana Naibu Spika wa Muda. Ninaunga mkono Hoja hii ya usalama. Tunapoongea kuhusu usalama katika nchi ya Kenya, kila mtu anaona kwamba kuna shida mahali fulani. Kuna shida kwa sababu hakuna mahali hapa nchini hakujatokea janga kama hili tunalolizungumzia kuhusu Baragoi.
view