The fact that she received limited education doesn’t stop her from pursuing her dreams. As a victim of retrogressive culture, Leshoomo vows to help other girls to be educated to beat cultural norms that act as a hurdle. Maison’s political journey arose out of a gutsy choice she made to attend public meetings against her husband’s orders. The move opened the door for her to become a nominated councilor in 1992 a position she maintained for 10 years. She joined Maendeleo ya Wanawake in 1995 and rose to become the chairperson in Maralal District. In 2008, the Party of National Unity (PNU) nominated her to parliament. As a long serving member of the Samburu District Peace Committee, she has taken it upon herself to promote peace between the Samburu and the neighbouring communities.
10 Oct 2013 in National Assembly:
Ningependa kusema kwamba ikiwa sisi viongozi tunaona mahali shida iko inafaa tujiulize shida hii inatokea kwa nini na tutafanya nini. Kwa nini ninauliza haya masuali? Hii ni kwa sababu nimeona mengi katika Bunge la Kumi na hili la Kumi na Moja.
view
10 Oct 2013 in National Assembly:
Ningependa kusema kwamba kuna shida kubwa huko Baragoi, vile wenzangu wamesema. Ni uchungu sana kwa sababu hata maafisa wa usalama waliuawa.
view
10 Oct 2013 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika wa Muda, ninamuunga mkono mhe. Nkaissery kwa sababu hili ni jambo la kusikitisha na linawaadhiri Wakenya wote. Mambo yote tunayosema hapa, yanaenda wapi? Yatajibiwa na nani? Ni masikitiko makubwa. Siweza kurudia yale yaliyosemwa na mhe. Lentoimaga kwa sababu ametaja kila kitu. Nitagusia tu machache ya mambo ambayo hajayazungumzia.
view
10 Oct 2013 in National Assembly:
Nilishuhudia mimi mwenyewe kile kilichofanyika kwenye mauaji ya halaiki ya watu kule Baragoi lakini tulipokuwa tukiulizana ni kitu gani kilifanyika, nilipelekwa kwenye afisi ya CID kwa sabau niliongea kuhusu jambo hilo. Ikiwa watu wako The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
10 Oct 2013 in National Assembly:
wamekufa, na umeona; akiwemo mtoto wa ndugu yako, ukiwa kiongozi, utanyamaza? Ninaomba hivi. Sisi tuko katika Serikali; hatuko nje ya Serikali. Kenya ni yetu. Hakuna mahali tunaenda. Kenya ni yetu, na ni lazima tuseme ukweli ili makosa yarekebishwe.
view
10 Oct 2013 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika wa Muda, tukio la tarehe 2.10.2013 lilinishangaza sana. Kama alivyoeleza mhe. Lentoimaga, watoto waliuawa na ng’ombe kuibiwa. Jambo la kushangaza ni kwamba ripoti rasmi ya Serikali iliyoletwa Nairobi inasema kwamba hakuna mtu aliyeuawa ama ng’ombe kuibiwa. Ripoti hiyo ilitumwa Nairobi licha ya kwamba maiti za waathiriwa zilikuwa bado hazijazikwa. Hali hiyo inanikera sana. Tulifanya kampeini ya amani miongoni mwa wakazi wa sehemu hiyo, na watu wakarudiana na kuanza kukaa pamoja kwa amani. Hatujui vita vilianzia wapi tena. Swali ambalo ningependa kuuliza ni: Ng’ombe hao wanapelekwa wapi?
view
10 Oct 2013 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika wa Muda, ninauliza, ng’ombe hao wanapelekwa wapi, ndiyo tujue. Zile bunduki za Serikali zilizopotea zinatumiwa kuwaua raia. Makosa yako wapi katika Serikali? Ningependa wale ambao wako na makosa Serikalini wachukuliwe hatua. Kuna endelea nini katika kitengo cha usalama? Hali ya usalama imezorota zaidi. Nikizungumza hivi sasa, nimearifiwa kwamba hakuna watu Baragoi. Watu wote wamehamia kwenye milima. Watoto wametolewa shuleni. Sasa tutafanya nini?
view
25 Sep 2013 in National Assembly:
Asante sana mhe Naibu Spika wa Muda. Mimi pia naunga mkono Hoja hii. Ningesema tu ukweli ni kwamba hawa homeguard s ama policereservists ni askari ambao sisi tuko nao. Askari wa Serikali ni wachache. Wengine pia wanachunga maeneo wanakopelekwa, na ndio maana tunamshukuru Mhe Lentoimaga kwa kuleta Hoja hii; kwa kweli eneo lake linahitaji hawa askari wa nyumbani. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
25 Sep 2013 in National Assembly:
Mhe Naibu Spika wa Muda, ningesema hivi, sisi tumeona mengi na washa hii inauliza---
view
25 Sep 2013 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika wa Muda hiyo ni sawa. Ninamshukuru Mhe. Mbunge kwa kunirekebisha, lakini Kiswahili si lugha yangu. Ningemwongelesha kwa Kisamburu ndio angenielewa vizuri.
view