Maison Leshoomo

Parties & Coalitions

Born

1962

Post

Parliament Buildings
Parliament Rd.
P.O Box 41842 – 00100
Nairobi, Kenya

Email

laikipiawest@parliament.go.ke

Telephone

0724958726

Maison Leshoomo

The fact that she received limited education doesn’t stop her from pursuing her dreams. As a victim of retrogressive culture, Leshoomo vows to help other girls to be educated to beat cultural norms that act as a hurdle. Maison’s political journey arose out of a gutsy choice she made to attend public meetings against her husband’s orders. The move opened the door for her to become a nominated councilor in 1992 a position she maintained for 10 years. She joined Maendeleo ya Wanawake in 1995 and rose to become the chairperson in Maralal District. In 2008, the Party of National Unity (PNU) nominated her to parliament. As a long serving member of the Samburu District Peace Committee, she has taken it upon herself to promote peace between the Samburu and the neighbouring communities.

All parliamentary appearances

Entries 191 to 200 of 314.

  • 25 Sep 2013 in National Assembly: Ningesema tu kwamba kile Mh.e Lentoimaga ameuliza ni hawa askari wa nyumbani wapate pesa kidogo ili waanze kufanya kazi. Kazi ile wanafanya katika maeneo yetu ni kazi ya askari. Kila wakati wako mpakani wakichunga mifugo na wananchi; wanatembea usiku na mchana na hawana chochote. Serikali yetu imekubali kuwapatia bunduki. Kama Serikali imekubali kufanya hivyo ndio wapate kuangalia maeneo yao, tunaomba pia wapate pesa kidogo za kujisaidia. view
  • 25 Sep 2013 in National Assembly: Mhe Naibu Spika wa Muda, wakati wa Rais wetu Kenyatta aliyefariki zamani--- view
  • 25 Sep 2013 in National Assembly: Niliwaambia Kiswahili si lugha yangu. Wacha tu nikoroge kile naelewa. view
  • 25 Sep 2013 in National Assembly: Wakati huo Wasamburu, Turkana na Pokot walikuwa wanachunga mpaka bila hata nguo. Hao ndio walikuwa askari wakati huo na ndio unaona Kenya yetu imesimama mpaka tangu wakati wa kupata Uhuru mpaka sasa. Hii ni kwa sababu ya hawa watu. Kwa hivyo, hawa ni askari wa nyumbani. Serikali imekubali kuwapatia bunduki kwasababu wanaelewa ni watu ambao wanaweza kuchunga watu wengine. Kwa hivyo, tunaomba wapewe pesa kidogo kwa kufanya hiyo kazi. Pia inafaa wapewe mavazi na magari ndio wakisikia kitu waanze kukimbia wakienda pale. view
  • 25 Sep 2013 in National Assembly: Mhe Naibu Spika wa Muda, mnajua kama kungekuwa na home guards wa kutosha katika maeneo yote ambayo mwenzangu ametaja mauaji yalitokea, hayangetokea. Tunaomba wapewe pesa hizi kwa sababu tunaishi katika maeneo ya milima na mabonde. Askari wa kutoka hapa akipelekwa kuchunga kule hawezi kuchunga huko kwa sababu hajui barabara. Hakuzaliwa huko. Hajui hii milima na pia hajui apitie wapi. Yule anayeishi pale ndiye anajua maeneo yapi ya kupitia au maeneo gani wakora watatokea. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 25 Sep 2013 in National Assembly: Tunaomba katika mipaka yetu yote askari wapelekwe ambao wanaweza kuchunga, hata kama ni home guard, polisi, Administration Police (AP) na jeshi. Tunaomba hawa watoto waandikwe na mutaona vile Kenya itachungwa kwasababu wanaelewa mipaka yote. Ukiniambia eti nitoe mtoto ambaye amezaliwa Nairobi na nimpeleka Lokichoggio, ataenda kufanya nini? Ataenda lakini atashindwa kufanya kazi kwa sababu ya jua kali. Hakuna maji lakini wenyeji wamejua kuishi huko. view
  • 25 Sep 2013 in National Assembly: Naibu Spika wa Muda, kwa hivyo ninasema Serikali yetu ijaribu kusaidia hawa askari wa reserve . Tunataka wapewe pesa, magari, mavazi na kila kitu ndio wachunge maeneo hayo. Hata wizi wa ng’ombe hautatokea tena wakiandikwa. Ngamia na punda hawataibwa tena wakipewa nafasi hii kwasababu wanaelewa maeneo hayo. Wizi wa mifugo utaisha. Kwa hivyo, Wabunge pia watajua watu wao ni wangapi. Hatutaenda kwa wakubwa wa polisi kama OCPD kuwahoji. Tutaenda kwa hawa askari. Watachunga mipaka na wizi wa mifugo utaisha. view
  • 25 Sep 2013 in National Assembly: Nasema nashukuru Wabunge wote ambao wamechangia Hoja hii. Nashukuru kwasababu tuna shida kubwa sana katika mpaka. Kwa hivyo, tupitishe Hoja hii na tusaidiane. Asante. view
  • 11 Jul 2013 in National Assembly: Asante sana mhe. Spika kwa kunipatia nafasi hii. Nafikiri mambo kuhusu gavana ninaona kwamba ni sheria ambayo haikuwekwa sawa sawa. Kwa ukweli, kila mtu anafikiria ni kwake pekee kuna shida lakini ni kila pahali. Kitu cha kwanza, tuna First Lady mmoja tu; Mrs. Uhuru Kenyatta. Lakini kule ukikuta gavana anasema “First Lady wangu yuko hapa”, sijui nani wangu ako hapa! Kwa hivyo, ningeomba tujaribu tuangalie sheria ile inaweza kusaidia Kenya yetu. Kama Katiba haikuangalia pande zote ni afadhali iletwe Bunge tupitishe yale mambo yatasaidia Kenya. Mambo kuhusu gavana ni taabu. Tunajua Rais ni mmoja na First Lady ni mmoja hatujui ... view
  • 10 Jul 2013 in National Assembly: Mhe. Naibu Spika wakati mwingine uangalie watu wengine ili waweze kusema neno hata moja. Tangu tuingie hapa wengine wetu hatujapata nafasi. Haya mambo ya miraa yanadhuru kila mahali. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus