The fact that she received limited education doesn’t stop her from pursuing her dreams. As a victim of retrogressive culture, Leshoomo vows to help other girls to be educated to beat cultural norms that act as a hurdle. Maison’s political journey arose out of a gutsy choice she made to attend public meetings against her husband’s orders. The move opened the door for her to become a nominated councilor in 1992 a position she maintained for 10 years. She joined Maendeleo ya Wanawake in 1995 and rose to become the chairperson in Maralal District. In 2008, the Party of National Unity (PNU) nominated her to parliament. As a long serving member of the Samburu District Peace Committee, she has taken it upon herself to promote peace between the Samburu and the neighbouring communities.
10 Jul 2013 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika wakati mwingine uangalie watu wengine ili waweze kusema neno hata moja. Tangu tuingie hapa wengine wetu hatujapata nafasi. Haya mambo ya miraa yanadhuru kila mahali.
view
10 Jul 2013 in National Assembly:
Ahsante mhe. Naibu Spika. Naunga mkono haya mambo ya miraa . Hii kamati sharti ichunguze miraa ina sections ngapi. Hii ni kwa sababu kuna ile inaitwa kangeta, muguka, giza na kadhalika. Hii ambayo inaitwa kata ndiyo inakata wanaume.
view
10 Jul 2013 in National Assembly:
Ahsante mhe. Naibu Spika. Naunga mkono haya mambo ya miraa . Hii kamati sharti ichunguze miraa ina sections ngapi. Hii ni kwa sababu kuna ile inaitwa kangeta, muguka, giza na kadhalika. Hii ambayo inaitwa kata ndiyo inakata wanaume.
view
10 Jul 2013 in National Assembly:
Tungependa tujue gani kati ya hizo ndiyo mbaya. Miraa ni kama ngâombe kwa Wameru kwa sababu wanaitumia kusomesha watoto wao. Sharti tujue gani mbaya na gani nzuri. Miraa sasa inatumika na Wakenya wote. Watoto wote wanakula hii miraa . Kamati itupatie habari kamili.
view
10 Jul 2013 in National Assembly:
Tungependa tujue gani kati ya hizo ndiyo mbaya. Miraa ni kama ngâombe kwa Wameru kwa sababu wanaitumia kusomesha watoto wao. Sharti tujue gani mbaya na gani nzuri. Miraa sasa inatumika na Wakenya wote. Watoto wote wanakula hii miraa . Kamati itupatie habari kamili.
view
28 May 2013 in National Assembly:
Ashante sana Naibu Spika. Hata mimi ninaunga mkono Hoja hii kuhusu Bw. Kimemia. Kwa kweli mimi sijui ni watu gani katika Kenya tunataka! Ukiangalia ile kazi Bw. Kimemia amefanya katika nchi hii, nafikiri ni mtu ambaye anastahili kupatiwa kazi hii. Badala ya kuongea mengi, tungepitisha Hoja kwa sababu naona kila mtu hapa ni rafiki ya Bw. Kimemia. Yafaa tuseme kwamba tunajua kazi yake. Kwa kweli ni mtu mwenye roho safi; hata ukiwa na shida, kama sisi ambao tuna shida ya usalama, na umpigie simu saa tisa usiku atachakua. Ukimweleza shida zako, atafanya kile wakenya wanataka. Kwa hivyo, ninaonelea kwamba, badala ...
view
22 May 2013 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika kwa kunipa nafasi hii ili nami nichangie Hoja hii. Namshukuru mhe. Ganya kwa kuleta Hoja hii katika Bunge hili ili tuizungumzie. Mambo ya wanyama wa pori yanafaa tuyazungumzie kwa sababu sisi ndiyo tunaishi nao. Tulizaliwa na kuishi na hao wanyama na tumewachunga kama vile tunawachunga ngâombe na mbuzi wetu. Lakini ajabu ni moja. Wale wanaowachunga na wale wanaoangalia, hakuna faida wanayopata kutokana na wanyama hao. Kuua ndovu ama mnyama yeyote wa pori--- Wenzangu wamepata soko kubwa na ingefaa ijulikane ni ya nani. Sheria ingewekwa ili tujue soko hiyo ni ya nani.
view
22 May 2013 in National Assembly:
Hiyo ni kwa sababu soko ya meno ya ndovu imewaangamisha watu wengi. Soko hilo linafanya wenyeji wa eneo letu la Samburu, Wamaasai na wafugaji wote kuumia kwa sababu ndovu wanauliwa na kutolewa meno. Wakazi kama sisi hatukuli nyama ya ndovu. Kwa hivyo, unapata ndovu kama 20 wameuawa na wenye wanaowachunga. Hujui wanauliwa namna gani. Kwa hivyo, ningesema kwamba, sisi wengine tunaumia kwa sababu vifaro pia wameisha. Wamebaki kwa wazungu na katika mashamba makubwa. Ukienda katika hifadhi za wanyama wa pori kama vile Hifadhi ya Wanyama ya Samburu, hutapata ndovu. Ukipata, labda mbili au tatu ukibahati. Mhe. Naibu Spika, mashamba ya ...
view
2 May 2013 in National Assembly:
Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuchangia Hoja hii. Ningependa kusema---
view
2 May 2013 in National Assembly:
Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuunga mkono Hoja hii kuhusu ukosefu wa usalama. Si watu wa Kaunti ya Bungoma ambao wanaathiriwa na ukosefu wa usalama bali ni sisi sote. Nilikuwa ninachangia mambo ya Peace Caravan katika eneo letu. Ningependa kuwapa pole watu wa Kaunti ya Bungoma. Sisi zote tumepitia mambo haya na inafaa tushirikiane ili wauwaji waweze kupatikana haraka. Pia, inafaa viongozi wote wa mashinani washirikiane ili maafisa wa Serikali waweze kujua ukweli kwa sababu maafisa hawajui waelekee wapi. Sisi watu tunaotoka Baragoi, tumeathiriwa kutokana na ukosefu wa usalama tangu 2009. Watu 40 waliuwawa na kukatwa shingo ...
view