The fact that she received limited education doesn’t stop her from pursuing her dreams. As a victim of retrogressive culture, Leshoomo vows to help other girls to be educated to beat cultural norms that act as a hurdle. Maison’s political journey arose out of a gutsy choice she made to attend public meetings against her husband’s orders. The move opened the door for her to become a nominated councilor in 1992 a position she maintained for 10 years. She joined Maendeleo ya Wanawake in 1995 and rose to become the chairperson in Maralal District. In 2008, the Party of National Unity (PNU) nominated her to parliament. As a long serving member of the Samburu District Peace Committee, she has taken it upon herself to promote peace between the Samburu and the neighbouring communities.
7 Aug 2012 in National Assembly:
Asante Bwana Spika. Ningependa kumuuliza Waziri maswali matatu. Swali la kwanza---
view
7 Aug 2012 in National Assembly:
Bwana Spika, ningependa kumuuliza Waziri kuhusu mambo ya vitambulisho. Nimetoka Samburu leo na nilikuwa huko kwa siku nne. Wasamburu ambao hawana vitambulisho ni 8,000. Hawa watu watakuwa 8,000 vipi na kila siku katika magazeti, tunasoma kwamba Waziri ameshapeana vitambulisho? Pia, kwa nini watu wengine ambao wamewasilisha maombi ya vitambulisho wamekaa miaka miwili sasa na cheti cha kungoja?
view
19 Jun 2012 in National Assembly:
Asante sana, Bw. Naibu Spika. Ningependa kumuuliza Waziri Msaidizi kama binadamu ni wa maana kuliko wanyama pori. Wakati ndovu wanauwawa na kutolewa pembe ama wanyama wengine wanauwawa, maofisa wa Kenya Wildlife
view
30 May 2012 in National Assembly:
alimuuliza Waziri wa Maji na Unyunyizaji:-
view
30 May 2012 in National Assembly:
(a) ana mipango gani ya uvunaji wa maji kule Samburu wakati huu wa mvua; na,
view
30 May 2012 in National Assembly:
(b) mabwawa mangapi yamefunikwa na mchanga katika eneo la Samburu.
view
30 May 2012 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika, ninamshukuru Waziri Msaidizi kwa jibu lake. Hata hivyo, kuna mabwawa 93 lakini si yote ambayo yanatumiwa kuvuna maji na kuhifadhi maji. Ni mabwawa 15 ambayo inatumiwa kuvuna na kuhifadhi maji. Mabwawa mengine yote yamejaa mchanga. Je, Bw. Waziri Msaidizi anaweza kuzuru eneo hili la Samburu na kujionea mwenyewe jinsi mabwawa hayo yamejaa mchanga?
view
30 May 2012 in National Assembly:
Swali hili linalenga maeneo mengine nchini ambapo mabwawa yake yamejaa mchanga na hayawezi kutumiwa katika kuvuna maji wakati huu wa masika. Wakati huu mvua ni nyingi sana na inasababisha vifo vya watu na wanyama wengi. Pia inasababisha harasa kubwa ya mali ya wananchi wa taifa hili. Ni mikakati gani mwafaka Wizara hii imeweka ili kuzuia hasara inayosababishwa na mvua katika maeneo mbalimbali nchini? Tumeshuhudia nyumba za watu na majengo mengine yakibomolewa na mafuriko ya maji. Mifugo na watu wengi wamepoteza maisha yao. Miaka nenda, miaka rudi, tunashuhudia mafuriko na baada ya miezi miwili ukame unaingia. Pia ukame husababisha hasara kubwa ...
view
30 May 2012 in National Assembly:
Bwana Naibu Spika, kwanza, sikubaliani na yale ambayo Waziri Msaidizi amesema hapa kwa sababu Wizara haijapeleka gari la kubeba maji kule Samburu. Pili, ni uongo Waziri Msaidizi anaposema kwamba ni lazima apate likizo ndio atembee huko. Angeenda huko kabla ya wiki ijao ili ajue ni nini anaweza kufanya. Inafaa Waziri Msaidizi achukue hatua na aache kudanganya kwa kusema kwamba ataenda Samburu tukienda likizo. Hakuna magari ya kubeba maji huko. Pesa ambazo ametenga hazijafika Samburu.
view
30 May 2012 in National Assembly:
Asante, Bwana Naibu Spika. Nitaenda.
view