Maison Leshoomo

Parties & Coalitions

Born

1962

Post

Parliament Buildings
Parliament Rd.
P.O Box 41842 – 00100
Nairobi, Kenya

Email

laikipiawest@parliament.go.ke

Telephone

0724958726

Maison Leshoomo

The fact that she received limited education doesn’t stop her from pursuing her dreams. As a victim of retrogressive culture, Leshoomo vows to help other girls to be educated to beat cultural norms that act as a hurdle. Maison’s political journey arose out of a gutsy choice she made to attend public meetings against her husband’s orders. The move opened the door for her to become a nominated councilor in 1992 a position she maintained for 10 years. She joined Maendeleo ya Wanawake in 1995 and rose to become the chairperson in Maralal District. In 2008, the Party of National Unity (PNU) nominated her to parliament. As a long serving member of the Samburu District Peace Committee, she has taken it upon herself to promote peace between the Samburu and the neighbouring communities.

All parliamentary appearances

Entries 251 to 260 of 314.

  • 18 May 2011 in National Assembly: Asante sana, Bw. Naibu Spika kwa kunipa nafasi hii ili niseme machache juu ya Hoja hii. Ninamshukuru Mbunge ambaye ameleta Hoja hii katika Bunge hili. Hii ni kwa sababu wazee wengi wana shida nyingi sana. Ikiwa tutaipitisha Hoja hii, wazee wengi kule mashinani watafaidika. Tumeelezwa kuwa kuna wazee katika nchi hii ambao wamekuwa wakipata msaada huo. Msaada huo umeleta shida kwa viongozi wengi. Wazee wetu ambao hawapati pesa hizi wanadhani sisi hatuwatetei. Ninaunga mkono Hoja hii kwa sababu wazee wengi watafaidika kutokana na pesa hizi. Ninataka pia akina mama wazee nao pia wasaidiwe kwa sababu wana shida nyingi. Pesa hizi ... view
  • 17 May 2011 in National Assembly: Ahsante Bwana Spika. Ugonywa huu wa ng’ombe hauadhiri sehemu ya Engilai peke yake. Ugonjwa huo umetambaa kila mahali. Waziri Msaidizi anajua kwamba sisi ni watu wa kuhama. Kwa hivyo, ugonjwa huo unafaa kukomeshwa mahali ulipo kabla haujaenea kila mahali. view
  • 5 Apr 2011 in National Assembly: Jambo la nidhamu, Bw. Naibu Spika wa Muda. Ni wazi kwamba Waziri Msaidizi hajawahi kufika huko ili aelewe shida ya watu wetu ambayo imeletwa na wanajeshi wa Uingereza. Wanawake wengi hunajisiwa na wanajeshi hawa. Pia watu wengi wamepoteza maisha yao na wengine kujeruhiwa. view
  • 5 Apr 2011 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, ningependa Waziri Msaidizi atembelee eneo hilo ili athibitishe vile hali ilivyo. Hakuna haja ya kuja hapa na kujibu Swali kabla ya kuzuru eneo hilo. Hali ni mbaya sana! view
  • 23 Feb 2011 in National Assembly: alimuuliza Waziri wa Uchukuzi:- (a) kama ana habari kwamba uwanja mdogo wa ndege wa Baragoi katika Wilaya ya Samburu Kaskazini uko katika hali mbaya; na, (b) hatua atakayochukua kuhakikisha kuwa uwanja huo umerekebishwa. view
  • 23 Feb 2011 in National Assembly: Asante, Bw. Naibu Spika. view
  • 16 Feb 2011 in National Assembly: alimuuliza Waziri wa Maji na Unyunyizaji:- (a) Je, ana habari ya kwamba wakazi wa eneo la Samburu wamekumbwa na shida kubwa ya uhaba wa maji; na, (b) Serikali inapanga kuchukua hatua gani kabambe kuhakikisha ya kwamba wakazi wa wilaya hiyo wamepata maji. view
  • 16 Feb 2011 in National Assembly: Bw. Naibu Spika, inaonekana Waziri Msaidizi hajaelewa kabisa kuwa watu wako na shida ya maji. Sehemu hizi zote ziko na shida ya maji. Kwa sasa, watu hawana njia yo yote ya kupata maji. Lori ambazo Waziri Msaidizi amesema kuwa zinatumiwa kupeleka maji, hazijaonekana. Kuna sehemu ambayo hata chakula ikipelekwa sasa hii, watu hawana njia yo yote ya kupata maji. Mifugo inakufa kwa sababu ya kukosa maji. Hakuna lori yo yote ambayo inasambaza maji na visima vimekauka vyote. Ningemuomba Waziri Msaidizi aelezee kwa njia ambayo inaeleweka. view
  • 16 Feb 2011 in National Assembly: Bw. Naibu wa Spika, Waziri Msaidizi amesema kwamba amepeleka AIE, na tunajua kwamba AIE ni karatasi. Ninaomba atuthibitishie iwapo ametuma pesa ama kartasi. view
  • 16 Feb 2011 in National Assembly: Pili, alisema kwamba magari yatakombolewa. Je, angependa kusema kwamba wamepeleka huko “kartasi” hiyo kama idhini kwa maafisa wao kukomboa magari? Wasipopewa idhini, maafisa kwenye kaunti hawawezi kukomboa magari. Waziri Msaidizi angethibitisha kwamba wamekubali kukomboa magari, na kwamba pesa zimefika Maralal ili tuelewe. Kusema AIE imetumwa hakusaidii. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus