Maison Leshoomo

Parties & Coalitions

Born

1962

Post

Parliament Buildings
Parliament Rd.
P.O Box 41842 – 00100
Nairobi, Kenya

Email

laikipiawest@parliament.go.ke

Telephone

0724958726

Maison Leshoomo

The fact that she received limited education doesn’t stop her from pursuing her dreams. As a victim of retrogressive culture, Leshoomo vows to help other girls to be educated to beat cultural norms that act as a hurdle. Maison’s political journey arose out of a gutsy choice she made to attend public meetings against her husband’s orders. The move opened the door for her to become a nominated councilor in 1992 a position she maintained for 10 years. She joined Maendeleo ya Wanawake in 1995 and rose to become the chairperson in Maralal District. In 2008, the Party of National Unity (PNU) nominated her to parliament. As a long serving member of the Samburu District Peace Committee, she has taken it upon herself to promote peace between the Samburu and the neighbouring communities.

All parliamentary appearances

Entries 261 to 270 of 314.

  • 16 Feb 2011 in National Assembly: Hoja ya nidhamu, Bw. Naibu wa Spika. Waziri Msaidizi amesema kwamba malori yametumwa. Mwaka uliopita, lori la AP lilitumwa huko, na hivi sasa halina magurudumu. Lori hilo limeegezwa juu ya mawe. Kwa hivyo, ni afadhali azungumzie kile kitu ambacho kiko. view
  • 2 Feb 2011 in National Assembly: Bw. Spika, ningependa kumwambia Naibu wa Waziri Mkuu na Waziri wa Serikali za Wilaya kwamba wakati tunazungumzia mambo ya njaa, yasichangwe na mambo mengine kwa sababu watu wako na njaa. Mahali ninapotoka, watu wangu wanakosa chakula. Msafara wa Prime Minister haukutembelea wananchi kuangalia ni nani anastahili kupewa chakula ama ni nani hastahili. view
  • 2 Feb 2011 in National Assembly: Nipe nafasi ili nimalize kuuliza swali langu halafu mtauliza yenu! Nasema hivyo kwa sababu tunatoka pahali watu wanaumia; tunatoka pahali watu wanadanganywa kila siku. Mkisema boreholes zitajengwa, magari ya jeshi yanaenda na wananchi wanayaangalia hayo magari na hakuna kitu ambacho kinafanyika. Kwa hivyo, tunaomba kujua kama kuna chakula ama hakuna. Serikali inasaidia watu wachache. Tunataka waache kudanganya hapa kwamba chakula na maji yatapelekwa huko wakati ambapo hakuna kitu kinachotendeka. Watu wanaumia! Wanafunzi hawaendi shule. Wale wanaotarajia kwenda Form I, hawataenda kwa sababu ya taabu. Kwa hivyo, ningependa kuuunga mkono kwamba kutembea kwa Prime Minister sehemu zile ni kutembelea watu wake ... view
  • 25 Aug 2010 in National Assembly: alimuuliza Waziri wa Barabara:- (a) kama ana habari ya kwamba barabara ya Rumuruti- Maralal haipitiki kwa sasa; na, (b) hatua ambayo Serikali itachukua ili kuhakikisha kwamba barabara hiyo imewekwa lami. view
  • 25 Aug 2010 in National Assembly: Bw. Naibu Spika, ninashukuru Waziri kwa kukubali kwamba barabara hiyo ni mbaya. Tumezungumza sana juu ya Barabara ya Rumuruti-Maralal. Hii barabara haipitiki tangu mvua inyeshe na watu wanalala huko kwa sababu hakuna barabara nyingine ya kupitia. Mwenye kupewa kandarasi alimwaga maram na hakuitandaza. Kama mwanye kupewa kandarasi alimwaga maram, inakuaje Wizara inatoa tingatinga ya kumwaga maram? Ningependa Waziri ajibu maswali hayo kwa sababu kuna shida. view
  • 25 Aug 2010 in National Assembly: Asante, Bwana Naibu Spika. Nashukuru Waziri kwa kukubali kwamba barabara hiyo iko katika hali mbaya. Waziri amesema kwamba wataweka barabara hiyo mchanga mpaka Naibor. Kwa nini Wizara haiwezi kutengeneza barabara hii mpaka Maralal? Pia, ningeuliza Waziri atengeneze barabara hiyo wakati huu kwa sababu ni mbaya zaidi. Je,Waziri atachukua hatua gani ili kuhakikisha kuwa wananchi wanasafiri salama kwa sababu kuna majambazi wengi katika barabara hiyo? Watu wengi wameuawa katika barabara hiyo na wengine kuporwa mali zao. Pia, kuna wanyama pori katika barabara hiyo. Juzi, wanafunzi ambao walikuwa wanatoka hapa waliponea kifo. Wanafunzi hao walivamiwa na simba ambao walizuia basi lao. Kwa ... view
  • 25 Aug 2010 in National Assembly: Niko tayari,Bwana Naibu Spika, kwenda hata leo! view
  • 19 Aug 2010 in National Assembly: Jambo la nidhamu, Bw. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kumkumbusha Waziri Msaidizi kwamba masuala kuhusu usalama wa wananchi yanapaswa kuchukuliwa hatua mwafaka ili ukweli ujulikane. Waziri Msaidizi ametuambia kwamba ni lazima atachukua hatua. Ni hatua gani ambayo amechukua tangu tulipoanza kuzungumzia masuala haya ya usalama? Ninamwomba atie juhudi kubwa katika masuala ya usalama. view
  • 18 Aug 2010 in National Assembly: alimuuliza Waziri wa Uhamiaji na Usajili wa Watu:- (a) ikiwa ana habari kwamba watu wengi wa jamii zilizotengwa nchini (marginalised communities) hawajasajiliwa na kupatiwa vitambulisho vya kitaifa; na (b) ni hatua gani kabambe Serikali inachukua kuhakikisha ya kwamba watu hawa wamefikiwa na huduma hiyo. view
  • 18 Aug 2010 in National Assembly: Bw. Naibu Spika, ningependa kumshukuru Waziri Msaidizi kwa kutueleza kwamba hakuna watu wametengwa kuhusiana na vitambulisho. Ni muhimu Wakenya wawe na vitambulisho. Katika maeneo kama hayo utamkuta mtu ana umri wa miaka 60 lakini hana kitambulisho. Pia, watu wengi hutembea kilomita 70 kutafuta kitambulisho, kwa mfano, kutoka Baragoi hadi Maralal kwa sababu hakuna magari ya kusafirisha. Utafika huko namna gani? Katika harakati zangu za kutafuta amani, nimekutana na vijana wengi ambao hawana vitambulisho. Huu muda wote tumelia kwamba watu wetu hawana vitambulisho, je, Waziri Msaidizi anaweza kutueleza ina maana gani kusemekana kwamba sharti kila Mkenya awe na kitambulisho ilhali Serikali ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus