Maison Leshoomo

Parties & Coalitions

Born

1962

Post

Parliament Buildings
Parliament Rd.
P.O Box 41842 – 00100
Nairobi, Kenya

Email

laikipiawest@parliament.go.ke

Telephone

0724958726

Maison Leshoomo

The fact that she received limited education doesn’t stop her from pursuing her dreams. As a victim of retrogressive culture, Leshoomo vows to help other girls to be educated to beat cultural norms that act as a hurdle. Maison’s political journey arose out of a gutsy choice she made to attend public meetings against her husband’s orders. The move opened the door for her to become a nominated councilor in 1992 a position she maintained for 10 years. She joined Maendeleo ya Wanawake in 1995 and rose to become the chairperson in Maralal District. In 2008, the Party of National Unity (PNU) nominated her to parliament. As a long serving member of the Samburu District Peace Committee, she has taken it upon herself to promote peace between the Samburu and the neighbouring communities.

All parliamentary appearances

Entries 271 to 280 of 314.

  • 18 Aug 2010 in National Assembly: Bw. Naibu Spika, inaonekana kwamba kuna shida katika shughuli za kuwasajili watu wetu ili wapate vitambulisho. Ningeomba Waziri Msaidizi ajaribu kuzipatia nguvu idara ambazo ziko kwa wilaya ili kila mtu apate kitambulisho. Naibu Waziri angetueleza vile tunaweza kupata idara ambayo ni mobile ambayo inaweza kuzunguka katika kila kata ili kuwasajili watu. Tukiuliza Swali na mambo hayo hayatekelezwi, haisaidii. Ningeomba Idara ya Usajili wa Watu iimarishwe. Hii ni kwa sababu utapata mtoto anashtakiwa kwa kukosa kitambulisho. Je, ni nini itaonyesha kuwa yeye ni Mkenya kama hana kitambulisho? Kwa hivyo Idara ya Usajili wa Watu ingefanya juhudi zaidi kuhakikisha kuwa Wakenya wote ... view
  • 18 Aug 2010 in National Assembly: Asante sana Bw. Naibu Spika wa Muda. Naunga mkono Hoja hii. Kuhusu mambo ya wizi wa ng’ombe, ninamshukuru mwenyekiti wa Kamati hii kwa kuleta Hoja hii mbele ya Bunge. Jambo la wizi wa ng’ombe ni jambo ambalo lingeangaliwa kwa njia ambayo inaweza kusaidia wafugaji. Hili ni jambo ambalo limeleta hasara sana na tumepoteza watu wengi. Tumetembea Isiolo na Samburu East na tukaona chanzo cha shida hiyo. Mimi ninaona kwamba ingekuwa muhimu ili tutengeneze sheria ambayo itaweza kutatua shida hiyo. Tumeona mengi kule Isiolo na Samburu East. Hayo mambo yalikuwa yanafanyika hivi; vijana wakienda kuiba ng’ombe upande wa Samburu, upande wa ... view
  • 18 Aug 2010 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda hapa ingawa tunazungumzia jambo hili wale watu ambao wanaumia ni wamama na watoto kwa sababu mama atapoteza mtoto wake kwa wizi wa mifugo. Mama pia atakosa chakukla cha kulisha yule mtoto wake. Hili jambo la wizi wa ng’ombe lingekuwa linachukuliwa kama jambo zito sana kwa sababu maisha ya watu wengi yamepotea. Mimi ninaonelea kwamba hili jambo silo la Isiolo na Samburu East peke yake bali linajumulisha jamii ya wafugaji wote. Ukiangalia mambo ya Pokot na Samburu, tulipoteza watu 30 kwa siku moja. Watu 30 kufa siku moja na kuzikwa katika kaburi moja ni jambo ambalo ... view
  • 18 Aug 2010 in National Assembly: jambo la wizi wa ng’ombe linafaa liangaliwe sana kwa sababu linaweza kuwa hata sio wizi wa ng’ombe bali pengine kuna mpango mwingine. view
  • 18 Aug 2010 in National Assembly: Mimi ninashukuru “peace caravan” ambayo tulianzisha na vijana kutoka pande zote. Wakati tuliingilia kati na kuuliza wananchi kwa nini vita vinazuka tulipata ukweli. Kuna wananchi ambao walituambia kwamba hawajasalimiana kwa miaka mitano. Mara nyingi wanaenda kusalimia wenzao na bunduki. Kwa hivyo unaweza kujiuliza ni jambo gani linaloendelea. Unaweza kupata kwamba ile habari ambayo inafika kwa Serikali ni tofauti na ukweli. Kwa hivyo, ingekuwa muhimu kama tungepata ukweli. Sisi tunaunga mkono hii ripoti kwa sababu inaweza kusaidia. view
  • 18 Aug 2010 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, mimi pia najiuliza, katika Isiolo na Samburu East, wakati ng’ombe 4,000 walichukuliwa na kila mtu kupatiwa mji--- view
  • 18 Aug 2010 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, ningeomba unisaidie niseme machache tu. Wakati hao ng’ombe walichukuliwa, hawakuchunguza kama walikuwa wametokana na wizi ama ni wa mama maskini ambaye hana kitu kingine, ama ni wa mzee ambaye mtoto wake hakuwa ameenda kuiba. Hao ng’ombe walikusanywa na watu kupatiwa. Sasa utashangaa ni kwa nini wasifuate wezi mpaka mahali wameenda. Kwa sababu hao wezi hawatoki nchi nyingine bali ni sehemu hiyo tu. Kwa hivyo, ingechunguzwa ili ijulikane wizi umetoka wapi na wezi wafuatwe. Ninawashukuru vijana wetu kwa sababu wamesema kwamba wanataka kazi. Mimi ningeomba kwamba hao vijana wapewe kazi. Hiyo ndio shida iliyoko katika jamii ... view
  • 18 Aug 2010 in National Assembly: Kwa hayo machache ,ninaunga mkono Hoja hii. view
  • 12 Aug 2010 in National Assembly: Ahsante, Madam Naibu Spika wa Muda. Mimi pia nataka kuchangia mambo ya ardhi. Ingekuwa muhimu kuongezea pesa mambo ya ardhi. Nafikiri sehemu zote zina shida; hasa shida za vyeti vya kumiliki mashamba. Kama pahali nimetoka, hakuna mtu ako na cheti cha kumiliki ardhi. Ningemwomba Waziri ajaribu kupanga semina ya kufunza watu mambo yanayohusu ardhi hasa kwa watu ambao wako chini ya miradi ya group ranches. Kwetu kuna group ranches na watu wana shida kubwa kupata title deeds. Pesa zinazohitajika ili watu wagawanyiwe ardhi ni nyingi sana. Watu wameshindwa kulipa. Kwa hivyo, mimi pia ningeomba Waziri ajaribu kufanya semina katika sehemu ... view
  • 12 Aug 2010 in National Assembly: Kwa hivyo, yangu ni hayo tu. Naunga mkono. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus