Maison Leshoomo

Parties & Coalitions

Born

1962

Post

Parliament Buildings
Parliament Rd.
P.O Box 41842 – 00100
Nairobi, Kenya

Email

laikipiawest@parliament.go.ke

Telephone

0724958726

Maison Leshoomo

The fact that she received limited education doesn’t stop her from pursuing her dreams. As a victim of retrogressive culture, Leshoomo vows to help other girls to be educated to beat cultural norms that act as a hurdle. Maison’s political journey arose out of a gutsy choice she made to attend public meetings against her husband’s orders. The move opened the door for her to become a nominated councilor in 1992 a position she maintained for 10 years. She joined Maendeleo ya Wanawake in 1995 and rose to become the chairperson in Maralal District. In 2008, the Party of National Unity (PNU) nominated her to parliament. As a long serving member of the Samburu District Peace Committee, she has taken it upon herself to promote peace between the Samburu and the neighbouring communities.

All parliamentary appearances

Entries 291 to 300 of 314.

  • 26 Aug 2009 in National Assembly: kumuuliza Waziri wa Utawala wa Mikoa na Usalama wa Ndani:- (a) Je, Waziri ana habari kuhusu vita kati ya jamii za Samburu na Pokot mnamo tarehe 7/8/2009 katika tarafa ya Poro, Wilayani Samburu, ambapo watu watatu walipoteza maisha, wanne kulazwa hospitalini na majeraha mabaya na mifugo kadhaa kuibwa? (b) Je, Serikali inachukua hatua gani kukomesha vita baina ya jamii hizi mbili, ambavyo vimeendelea kwa miaka mingi? view
  • 26 Aug 2009 in National Assembly: Asante sana, Naibu wa Spika. Ningependa kuomba msamaha. Nimechelewa barabarani. view
  • 26 Aug 2009 in National Assembly: Bw. Naibu Spika, naomba kumuuliza Waziri wa Utawala wa Mikoa na Usalama wa Ndani Swali la Dharura lifuatalo. (a) Je, Waziri ana habari kuhusu vita kati ya jamii za Samburu na Pokot vilivyotokea mnamo tarehe 7.8.2009 katika tarafa ya Poro, Wilayani Samburu, ambapo watu watatu walipoteza maisha yao, wanne kulazwa hospitalini na majeraha mabaya na mifugo kadhaa kuibwa? view
  • 26 Aug 2009 in National Assembly: (b) Je, Serikali inachukua hatua gani kukomesha vita baina ya jamii hizi mbili ambavyo vimeeendelea kwa miaka mingi? view
  • 26 Aug 2009 in National Assembly: Bw. Naibu Spika, sijasikia kile alichosema. Ningeomba arudie. view
  • 26 Aug 2009 in National Assembly: Bw. Naibu Spika, nimekubali lakini ningeomba asichukulie jambo hili ambalo linahusu vifo vya watu kama jambo lisilo na maana. view
  • 24 Jun 2009 in National Assembly: alimuuliza Waziri wa Ulinzi:- (a) ikiwa Waziri ana habari kuhusu mlipuko wa bomu tarehe 13/6/09 katika eneo la Nairoborkeu, tarafa ya Loroki, wilaya ya Samburu ambapo mtoto wa miaka 12 aliuawa; na, (b) hatua zinazochukuliwa na Serikali kuzuia milipuko ya mara kwa mara, ikizingatiwa kwamba tangu mwaka wa 1990, mabomu yamekuwa yakilipuka na view
  • 24 Jun 2009 in National Assembly: Ahsante sana, Bw. Naibu Spika. Kwa ukweli, Naibu wa Waziri ametambua mambo yaliyotokea tarehe 13, lakini nasikitika sana kwa sababu tangu miaka ya 1990s, mabomu hayo yako hapo. Jambo hilo limeripotiwa kwa muda mrefu sana ili wanajeshi wetu wa Kenya waende wakayatoe mabomu hayo. Lakini hadi sasa, hakuna hatua iliyochukuliwa. Ningemuomba Naibu wa Waziri ajibidiishe kwa njia ya ukweli kwa sababu hayo ni maeneo ambayo watu wanaishi na mabomu. Mabomu hayo yamesababisha maafa ya watu 13, zikiwemo ngamia, mbuzi, ng’ombe na binadamu. Mabomu hayo pia yamechanganyika na yale ya wanajeshi wa ng’ambo. Bw. Naibu Spika, kwa ukweli--- view
  • 24 Jun 2009 in National Assembly: Mabomu hayo yatatolewa lini? Kuna kijana mmoja anayeitwa Betro Loronkiya ambaye amepiga ripoti mara nyingi. Alipoenda kupiga ripoti kwa polisi, aliwekwa ndani. Sasa, ninataka Naibu Waziri athibitishe jambo hilo kwa sababu tuko na stakabathi za kutosha. view
  • 24 Jun 2009 in National Assembly: Bw. Naibu Spika, ningependa kumwomba Waziri Msaidizi asiseme eti ni bomu moja liko huko kwa sababu mabomu mengi yako huko. Nina thibitisho kwamba mabomu yameonekana katika eneo hilo la Nairoborkeu . Je, hii familia iliyoathirika italipwa kwa njia gani? Je, mali iliyoharibika italipwa? Kuna watu wengi ambao wamehama mashamba yao kwa sababu ya mabomu yaliyomo ardhini. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus