The fact that she received limited education doesn’t stop her from pursuing her dreams. As a victim of retrogressive culture, Leshoomo vows to help other girls to be educated to beat cultural norms that act as a hurdle. Maison’s political journey arose out of a gutsy choice she made to attend public meetings against her husband’s orders. The move opened the door for her to become a nominated councilor in 1992 a position she maintained for 10 years. She joined Maendeleo ya Wanawake in 1995 and rose to become the chairperson in Maralal District. In 2008, the Party of National Unity (PNU) nominated her to parliament. As a long serving member of the Samburu District Peace Committee, she has taken it upon herself to promote peace between the Samburu and the neighbouring communities.
30 Jun 2010 in National Assembly:
Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Kwanza, ningependa kumshukuru sana mhe. Lekuton kwa kuleta Mswada huu hapa Bungeni. Sisi sote tunaunga mkono Mswada huu. Huu ni Mswada ambao utawasaidia sana wafugaji wa mifugo. Ni jambo la kuhuzunisha mno kuwa tangu Uhuru hatujawahi kama nchi kuwa na sheria kama hii inayopendekezwa na Mswada huu. Ninaomba kila mhe. Mbunge katika Bunge hili kuunga mkono kikamilifu Mswada huu kwa sababu wafugaji wamekuwa na shida nyingi tangu Uhuru. Wizi wa mifugo umeleta madhara makubwa kwa wafugaji na wanyama wao. Wanyama wetu huhaangaishwa sana na wezi wa mifugo. Wanaibwa kutoka wilaya moja hadi nyingine. ...
view
30 Jun 2010 in National Assembly:
Kwa hayo machache, ninaunga mkono Mswada huu.
view
1 Apr 2010 in National Assembly:
Asante sana Bw. Spika. Hata mini ninaunga mkono hilo pendekezo. Msichana akiolewa akiwa na miaka 11 au 12, au mvulana pia akioa mama mzee--- Ingekuwa muhimu kuwa na sheria ili tusaidie jamii zingine kama jamii ya wafugaji, ambao hawana hii habari. Kwa hivyo, kunatakikana kuwe na sheria ya kukataza jambo hili.
view
9 Dec 2009 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, Waziri Msaidizi anawaomba watu warudishe bunduki lakini ni bunduki gani inarudishwa wakati watu wanaangamizwa katika operesheni? Kwa nini operesheni inafanywa katika jamii fulani pekee yake?
view
16 Sep 2009 in National Assembly:
Bw. Spika, ninaomba Taarifa kutoka kwa Waziri wa Utawala wa Mikoa na Usalama wa Ndani kuhusu vita vilivyotokea jana huko Samburu. Waziri anaweza kutuambia ni watu wangapi, waliopata majeraha na ni ngâombe wangapi waliokufa jana? Pia, anaweza kujulisha Bunge hili wale waliohusika walitoka upande gani? Ni hatua gani Waziri atachukua kuhakikisha kwamba usalama unapatikana huko Samburu? Hakuna kitu kibaya kama mauaji yaliyotokea jana kule Samburu.
view
16 Sep 2009 in National Assembly:
Pia, Waziri anaweza kuliambia Bunge watoto na akina mama walikuwa na hatia gani ili wau awe kama wanyama? Tunaongea mambo yanayohusu usalama katika Bunge kila wakati lakini hatuoni hatua zikichukuliwa za kuwasaidia Wakenya kupunguza hali ya ukosefu wa usalama, hasa katika Samburu. Kama Waziri angekuwa hapa ningemuomba atoe Taarifa ya kweli ambayo inaweza kusikika na Wakenya wote.
view
2 Sep 2009 in National Assembly:
Asante sana, Bw. Naibu Spika. Nimenyamaza na kusikiza sana. Niko tayari kuunga mkono Hoja hii. Kile kimenishangaza ni vile wenzangu wanaongea.
view
1 Sep 2009 in National Assembly:
Bw. Spika, naomba kumuuliza Waziri wa Afya ya Uma na Usafi Swali maalum lifuatalo. (a) Je, Waziri ana habari kuhusu kuzuka kwa ugonjwa wa uvimbe wa tando za uti wa mgongo (yaani Meningitis) Wilayani Samburu,ambapo katika wiki tatu zilizopita umesababisha vifo vya watu watatu? (b) Ni hatua gani za dharura Serikali imechukua kukabiliana na ugonjwa huu?
view
1 Sep 2009 in National Assembly:
Bw. Spika, Waziri Msaidizi amesema ya kwamba hana habari kuhusu huo ugonjwa. Hata hivyo, kuna dhibitisho tosha kuwa watu watatu walifariki kutokana na ugonjwa wa meningitis. Watu hawa wanajulikana kuwa walikufa kutokana na ugonjwa huu. Watu wengi wanakufa kutokana na ugonjwa huu. Waziri Msaidizi atafanya nini kudhibitisha ukweli wa mambo haya?
view
1 Sep 2009 in National Assembly:
Bw. Spika, nimeshangaa sana kusikia ya kwamba walikufa kutokana na UKIMWI. UKIMWI ni tofauti sana na ugonjwa wa meningitis .Ni aibu kuona ya kwamba hospitali ya Serikali inashindwa kusema kilichosababisha vifo hivyo. Kijana Lambushona alipimwa katika Wamba Mission Hospital na kugunduliwa kuwa alikuwa anaugua meningitis . Ni hatua gani atachukua kuwasaidia watu wetu? Je, wana mipango gani ya kuwaajiri madaktari wengi?
view