Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1751 to 1760 of 2263.

  • 12 Jun 2018 in Senate: Bw. Spika. hivi karibuni tumeona kwamba, mhe. Rais baada ya kusalimiana kwa mkono na kupigana pambaja na mhe. Raila Amolo Odinga, waliipa kipaumbele swala la kupigana na ufisadi. Jambo hili la kutengeza mabasi laonekana limechukuliwa kabla ya Rais mwenyewe kuchukua hatua ya kupigana na ufisadi. Hivi sasa, kuna watu ambao kabla ya amri hii ya kupigana na ufisadi kikamilifu, wao walikuwa na mipango ya kuiba; walikuwa na mipango ya kufanya ufisadi ndani ya ofisi ili wapate pesa kutoka kwa umma. Ikiwa hili ndilo jambo ambalo walikuwa wanalidhania hawa wafisadi, basi nafikiria, mhe. Rais sasa hivi, ni wakati wake wa kuchukua ... view
  • 12 Jun 2018 in Senate: Bw. Spika, ningependa kuongea kidogo kuhusu kauli ambayo Sen. Faki ametoa. Hivi karibuni, tabia ya polisi imekuwa ya kusikitisha sana, haswa ukizingatia ya kwamba wanapigana na majambazi. Katika maeneo ya Pwani, vijana wengi sana wamekuwa wakishikwa na kuitishwa vitambulisho. Akiwa nacho, anaamrishwa aingie ndani ya gari, kisha aende kujibu mashtaka mbele. Yule asiyekuwa na kitambulisho atapona tu akitoa Ksh200 au Ksh300 ili aweze kupata uhuru wake. Tunaona tabia kama hizi zinaanza kuingia katika polisi wetu hapa Kenya. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from ... view
  • 12 Jun 2018 in Senate: Asante, Bwana Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia Mswada huu. Hususan Mswada huu unahusu pesa za uzeeni wakati mtu amestaafu. Ni jambo la muhimu kuwa na Shirika ambalo muajiriwa anaweza kuchanga pesa za kustaafu. Vile vile muajiri anafaa kulipa kiwango fulani kwa hazina hiyo. Katika muhula wa Seneti uliopita, nilikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya kuangalia maswala ya wafanyikazi. Hata hivyo, kwa sababu mara nyingi sisi tuliegemea upande moja au mwingine, hatukupitisha Mswada huu katika muhula huo. Ilisikitisha kuona Wabunge wakiegemea pande mbali mbali. Sasa Mswada huu uko hapa na vile vile katika Bunge la Kitaifa. Mswada huu ... view
  • 28 Mar 2018 in Senate: Asante Bw. Spika kwa kunipa nafasi. Siku ya Ijumaa ni siku muhimu sana haswa kwa jamii ya Waislamu lakini viongozi hao wawili sio Waislamu. Cha kushangaza ni kuwa walikutana siku ya Ijumaa na Mwenyezi Mungu aliibariki siku hiyo. Nachukua nafasi hii vilevile kuwapa kongole kwa ujasiri wao kukutana licha ya kuwa walikuwa wapinzani. Kuna baadhi ya Wakenya waliopoteza maisha yao kutokana na vita. Nina furaha kwamba Kiongozi wa Wachache katika Seneti alieongea na sikuona mtu yeyote upande ule mwingine akitoa hoja ya nidhani na hiyo si kawaida. Natumai kuanzia leo hoja za nidhamu hazitakuepo. Jambo la muhimu ni kwamba sote ... view
  • 28 Mar 2018 in Senate: Wanasema kwamba palipo na wazee, hapaharibiki neno. Mheshimiwa Uhuru Kenyatta na Mhemshimiwa Raila Odinga hatimaye walikutana. Kiongozi wa muungano wa wafanyakazi Bw. Francis Atwoli aliwaambia kuwa haina haja kutuambia siku, saa na wapi. Alitaka wakutane kisiri ama kiwazi lakini waongee peke yao na nchi hii itakuwa na amani. Msemo huo umetokea kuwa kweli. Nawapongeza watu wa dini, mawakili na watu wote katika nchi ya Kenya kwa kuhimiza viongozi hao wawili kukutana. view
  • 21 Mar 2018 in Senate: Asante Bw. Spika wa Muda. Jambo la kwanza, nasimama kupinga ripoti hii. Tunaelewa kwamba katika maisha ya binadamu, urefu, ufupi na miaka ya kuishi katika ulimwengu ni ya Mwenyezi Mungu. Katika maisha, huwezi hata kidogo kumbaguwa mtu kwa sababu yeye ni mfupi au mrefu. Hayo ni majaliwa ya Mwenyezi Mungu. Tukiangalia ripoti, tunaona kwamba Sen. Melly ni kijana mdogo sana. Lakini, kuwa kijana haimaanishi hana akili na ndio maana aliitwa katika mahojiano na baada ya hayo, mwenyekiti, naibu wake na kamati nzima tunayoifahamu na tuliipa jukumu hilo walimualika na baadaye wakahakikisha ameibuka mshindi. Hivi leo ni jambo la kusikitisha kabisa ... view
  • 21 Mar 2018 in Senate: Maoni yangu ya mwisho, nataka bwana Chairman --- view
  • 21 Mar 2018 in Senate: Nashukuru, Bw. Spika wa Muda. Unaweza kuona kwamba kijana kama Sen. Cheruiyot anaweza kuleta maoni kama hayo. Namshukuru kwa sababu ameweza kutueleza sote hapa ndani ya Seneti. La mwisho, Bw. Spika wa Muda, ni kumuomba Mwenyekiti wa Kamati hii achukue ripoti yake. Nyumba hii ya Seneti iko na uwezo wa kuchukua hatua hiyo hivi sasa na kugeuza repoti hii ili tuidhinishe yule ambaye amekuwa wa kwanza katika mahojiano hayo. Tunaweza kumtuma Mwenyekiti aende huko, akae na aregeshe ripoti hii hapa akisema ya kwamba Sen. Melly ndiye amechukua nafasi ya kwanza. Asante sana, Bw. Spika wa Muda. view
  • 20 Mar 2018 in Senate: On point of order, Mr. Speaker, Sir. view
  • 20 Mar 2018 in Senate: Mr. Speaker, Sir, is it in order for one Senator to stand up when another one is on the Floor, and the Senators who were standing were not consulting? It is in that regard that I am asking whether it is in order for two Senators to address you at the same time. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus