Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 2231 to 2240 of 2266.

  • 23 Jul 2014 in Senate: Yes, Mr. Deputy Speaker, Sir. view
  • 17 Jun 2014 in Senate: Hoja ya nidhamu, Bw. Naibu Spika. Je, ni haki kwa Sen. Elachi, akiwa Kiranja wa Wengi katika Seneti, kutaja kabila fulani? Seneti hii yaongea kuhusu Wakenya waliokufa na si watu wa kabila fulani. Ikiwa mambo yataenda hivyo, kati ya waliokufa huko Lamu pia kuna Waislamu na Wakristu. view
  • 17 Jun 2014 in Senate: Bw. Naibu Spika, je, ni haki kwa Sen. Elachi kulitaja kabila fulani na kusema wao peke yao ndiyo waliokufa? view
  • 17 Jun 2014 in Senate: Bw. Naibu Spika, kwa niaba ya watu wa Kilifi, Pwani na Kenya kwa jumla, ningependa kutoa rambirambi zangu kwa wananchi wa Lamu waliopatikana na mkasa huu, hasa wale wa Mpeketoni na vitongoji vyake. Bw. Naibu Spika, ningependa vilevile kukubaliana na wale wenzangu waliotangulia kusema ya kwamba wale ambao wamezembea kazini, hasa kwa upande wa ulinzi waachishwe kazi mara moja. Maisha ya Mkenya akiwa Lamu, Kisumu, Mombasa, Kilifi au sehemu yoyote ya Kenya ni muhimu sana katika nchi hii. Leo itakuwa ni aibu tukisimama na kujidai kama Wakenya ilhali ndugu zetu wanaweza kupoteza maisha kirahisi na kiholelaholela. Vifo hivi vinavyotokea mahali ... view
  • 13 May 2014 in Senate: Mr. Speaker, Sir, on behalf of the people of Kilifi County, I vote yes on count “a,” yes on count “b” and yes on count “c.” view
  • 6 May 2014 in Senate: Bw. Spika, asante kwa kunipa nafasi hii ili nipinge Hoja hii. Kitu cha kwanza, hii Hoja imetolewa na majina ya wale Maseneta ambao kwa upande wangu nina hakika wanaweza kufanya kazi hii. Katika wale Maseneta 11 waliowekwa na Kiongozi wa Walio Wengi, hakuna hata Seneta mmoja ambaye hawezi kuifanya kazi. Wote wana uwezo wa kuifanya hiyo kazi lakini katika akili yangu, je wale Maseneta The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 6 May 2014 in Senate: Ni sawa kwa ndugu yangu kunieleza. view
  • 6 May 2014 in Senate: Asante ndugu yangu Sonko lakini ningependa kukueleza kwamba mshtakiwa ana njia mbili katika sheria. Mshtakiwa anaweza kukubali ama kukata rufaa. Kwa hivyo, jukumu hilo ni lake. Ningependa kusema kwamba sisi kama Seneti, ni Bunge ambalo linaheshimiwa katika Kenya nzima. Ikiwa kuna Mkenya ambaye haki yake haitatimizwa kwa sababu tumeamua ni lazima mambo yawe hivyo, kwa maoni yangu, naona haki haitatimizwa ikiwa tutaweka majina haya vile yalivyokuwa. Kuna umuhimu wa Maseneta hawa 11 kujiondoa ili Seneti iwachague wengine ambao akili zao hazijaamua. Hii ni kwa sababu kisheria, akili zao zimeshaamua na zinajua mwelekeo zinaotaka kufuata. Maseneta wengine wanafaa kuchaguliwa kuchunguza swala ... view
  • 17 Apr 2014 in Senate: Bw. Spika, asante kwa kunipa nafasi hii. Jambo la kwanza ni kwamba nataka kuunga mkono Hoja hii na kumpatia heko Rais kwa kufikiria mpango huu wa Katiba wa kujadiliana ili kupeleka majeshi katika nchi ya South Sudan. Pia, The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 11 Mar 2014 in Senate: Asante sana, Bw. Spika wa Muda. Kwanza, nataka kumtumia heko sana aliyekuwa Mkuu wa Sheria katika nchi yetu ya Kenya, Sen. Wako, kwa Hoja hii. Kwanza, ni kwamba wananchi wa Kenya mpaka hivi sasa tokea tugeuze Serikali yetu iende mashinani, yaani, serikali ya ugatuzi, wengi hawajaelewa maana ya serikali za ugatuzi. Kwa hivyo, kunao umuhimu kwa Serikali kufanya juhudi ya aina yoyote ili watu waelewe uongozi na maana ya ugatuzi katika serikali za mashinani. Mimi nataka kuuliza tu kwamba wananchi wengi wanajua kwamba kuna seneta, gavana, mbunge wa maeneo na vile vile wabunge katika serikali za mashinani. Wananchi wengi hawaelewi ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus