Boy Juma Boy

Died

13th February 2017

Telephone

0713 242955

All parliamentary appearances

Entries 51 to 60 of 98.

  • 19 Nov 2014 in Senate: Asante sana, Bw. Spika wa Muda. Kwanza, ningependa kutoa rambi rambi zangu kwa familia, Wabunge, Seneti naviongozi wote wa CORD ambao wamepoteza shujaa wao. Kuna mwimbaji wa Tanzania ambaye aliimba wimbo unaoitwa kifo; anaitwa Remi Ongala. Alisema kama angejua kifo kitakuja namna gani angaliweza kukihonga. Kwa nini nasema hivyo? Nasema hivyo kwa sababu tulikuwa tumezoea kukaa pamoja na Sen. Kajwang. Hata wote mnajua kwamba sisi wazee wawili tunakaa pamoja na kwa jina maarufu tunajulikana kama Back benchers. Jana alipofika, tuliongea juu ya kufuzu kwa kakake kule Kampala. Tukazungumza kirefu na akanieleza kwa nini hakuhudhuria sherehe za kufuzu za kakake. Tulizungumza ... view
  • 13 Nov 2014 in Senate: Mr. Speaker, Sir, now that Sen. (Prof.) Lonyangapuo has clearly said that the Commissioner has already given the names to the security forces and the security forces are pursuing the raiders in vain. Could the operation be called off and follow up with the names that have been given? view
  • 25 Sep 2014 in Senate: Asante sana, Bw. Naibu Spika. Kwanza ningependa kumsifu Sen. Ongoro kwa kuleta Hoja hii ambayo ni muhimu. Ukiangalia kwa undani, utaona kwamba Hoja hii ina mambo muhimu sana. Ina mambo yanayohusu watoto ambao wanakuwa wazazi wakiwa na umri mdogo. Hili ni tatizo ambalo sisi kama viongozi ni lazima tulivalie njuga. Lakini kwanza, tutafute sababu. Tukubaliane ya kwamba hivi sasa mazingira yamebadilika na sio yale ya zamani. Huu ndio ukweli wa maneno. Mfumo wa digital na dot-com unaleta haya. Hivi sasa kuna simu na mitandao. Wanafunzi wanafahamu kila jambo. Kuna kitu kinachoitwa Facebook. Pia kuna kitu kinaitwa WhatsApp . Haya ndio ... view
  • 24 Sep 2014 in Senate: Asante sana, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili nizungumzie Hoja hii. Kwanza, ningependa kuchukua nafasi hii kumsifu Mwenyekiti wa Kamati hii, Sen. (Dr.) Zani, na Maseneta wenzangu ambao ni wanachama wa Kamati hii. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 11 Jun 2014 in Senate: Bw. Spika wa Muda, kwa niaba ya Kamati ya Elimu na Teknolojia, ningependa kuleta Hoja hii mbele ya Seneti hii, kuhusu Ripoti ambayo ilitayarishwa na Kamati hii baada ya kutembelea baadhi ya kaunti. Nawasilisha Ripoti hii mbele ya Seneti ili iweze kupitishwa kikamilifu. Bw. Spika wa Muda, kwa mujibu wa kipengee Nambari 96 ya Katiba na Kanuni Nambari 177 ya Seneti, Kamati ilikuwa na mujibu wa kusimamia maswala ya elimu--- view
  • 11 Jun 2014 in Senate: Mr. Temporary Speaker, Sir, I beg to move the following Motion. THAT, the Senate adopts the Report of the Standing Committee on Education, Information and Technology on the County Oversight and Networking Engagement (CONE) to Lamu, Tana River, Kilifi, Mombasa and Kwale Counties on 29th August – 5th September, 2013 laid on the Table of the Senate on Thursday, 3rd April, 2014. Bw. Spika wa Muda, hiyo ndio Hoja ambayo nilikuwa nawasilisha. Kwa mujibu wa Katiba, Kamati hii ilitembelea kaunti ambazo nimezitaja, zikiwemo kaunti za Lamu, Tana River, Kilifi, Mombasa na Kwale, kuanzia tarehe 29 Agosti mpaka tarehe 5 Septemba, ... view
  • 11 Jun 2014 in Senate: Tulioyaona ni hali ya kuhuzunisha. Miaka 50 bado katika--- view
  • 11 Jun 2014 in Senate: Bw. Spika wa Muda, ndugu wa hatari na danger, ni lipi ambalo hajafahamu? Sijakanganua lugha bali nimeileza kama ilivyo. Huyu hatari ndugu yake ni danger. view
  • 11 Jun 2014 in Senate: Bw. Naibu Spika, simlaumu Sen. Murkomen. Ukweli ni kwamba wakati mwingine hatupendi lugha zingine na huo ndio ukweli. Sasa ninachozungumzia ni kwamba tuanzie katika shule za chekechea. Hii ni muhimu sana kwa mtoto. Hamna haja ya kuanzia juu ukiteremka chini. Kule chini hata hakuna fedha na walimu wa kutosha. Hakuna madarasa ya kutosha ambao watawahudumia wanafunzi. Hakuna syllabus ambayo inaweza kueleweka. Kama hujafika Nairobi, utaendaje London? Hii ndio maana tukasema kwamba kazi ya Kamati hii kuenda katika kaunti ilikuwa ni muhimu sana ili tujionee wenyewe. Tunasema kwamba haya ni mambo ambayo yasingekuwepo baada ya miaka 50 tangu tupate Uhuru. Tungekuwa ... view
  • 11 Jun 2014 in Senate: Nafurahishwa na Mwenyekiti wangu kwa sababu uzuri wake ni kwamba anayasikia maneno yangu pamoja na yale yanayozungumzwa nyuma yangu! view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus